General health

Nikiungua Moto Nichukue Hatua Gani za Mapema?

Jamii ina utaratibu wake wa kufanya pale mtu anapoungua. Wewe unajua upi? Kwenye utamaduni wangu nimekuwa nikiona mtu akiungua anamwagiwa mkojo kwenye sehemu aliyoungua na imekuwa ikiaminika kwamba inasaidia.   Wengine huwa wanawahi kuweka asali sehemu iliyoungua wakiamini ni msaada mkubwa.  Wengine mafuta ya taa, petroli na kadhalika. Ninyi kwenu huwa  mnafanyaje?  Kuungua ni tukio […]

Nikiungua Moto Nichukue Hatua Gani za Mapema? Read More »

Mkojo Unakataa Kutoka? Tezi Inaweza Kuwa Sababu!

Tezi dume ni nini? Kila mwanaume huzaliwa na tezi. Tezi hii ni kiungo katika mfumo wa mkojo ambacho hufanya kazi ya kutoa majimaji (semens) ambayo husaidia shahawa za kiume kuogelea wakati wa  kutoka nje kupitia kwenye njia ya mkojo.  Pia maji hayo husaidia kuandaa njia ya mkojo kuondoa ule utindikali na hivyo kusaidia shahawa kupita

Mkojo Unakataa Kutoka? Tezi Inaweza Kuwa Sababu! Read More »

Madhara ya Kutomwambia Ukweli Daktari Wako

Mara nyingi tunapoenda hospitali hatusemi ukweli aslimia 100. Huenda unaogopa kumwambia daktari wako juu ya dalili zote ulizopitia, au muda ulioumwa, au kama umeshatumia mitishamba au dawa yoyote nyumbani kabla ya kwenda kumuona daktari.  Je, unajua madhara ya kutosema ukweli? Kunapoteza Muda Wako! Nimeshuhudia wagonjwa wengi wakipoteza muda hospitalini kwa kitu kidogo tu ambacho hawakusema

Madhara ya Kutomwambia Ukweli Daktari Wako Read More »

Kiharusi: Nini Hutokea Baada ya Kukipata? 

Bila shaka huwa una tabia ya kujifunza namna ya kuepuka magonjwa mbalimbali kama malaria, UKIMWI, kaswende, kansa, n.k. Lakini ulishawahi kujifunza namna ya kujikinga na kiharusi (stroke)?   Kama bado basi nakusihi uanze sasa kujua namna gani ya kujikinga na changamoto ya kiharusi kwasababau sio ugonjwa mzuri na una matokeo hasi sana ikiwa utaupata.   

Kiharusi: Nini Hutokea Baada ya Kukipata?  Read More »

Njia Kuu 4 za Kujikinga na Malaria

“Mwaka 2015 mtoto wetu wa miaka 6 alifariki kwa sababu ya ugonjwa wa malaria.” Alisema mama mmoja kwa uchungu wakati tukizungumza mawili matatu.   “Hatukuwahi kabisa kuzingatia maagizo ya afya ya kujikinga na malaria na ndio sababu.” Aliongezea mama huyo huku machozi yakimlenga.   Ni rahisi sana kupuuzia maagizo ya wataalam kuhusu namna ya kujikinga

Njia Kuu 4 za Kujikinga na Malaria Read More »

Faida za Kiafya za Kupunguza Uzito Wako 

Unapoweka malengo ya kupunguza uzito huwa unalenga nini hasa?   Je unataka muonekano mzuri? Unataka kuongeza ujasiri (confidence)? Au unataka kumfurahisha mchumba wako? Wengine hupunguza uzito ili waigize filamu au watoe wimbo fulani.  Kwa bahati mbaya asilimia 95% ya watu wanaojaribu kupunguza uzito hushindwa. Kama umeweza basi kuna sababu ya ziada na ya kipekee iliyokusaidia

Faida za Kiafya za Kupunguza Uzito Wako  Read More »

Njia 3 za Kiafya za Kuwa Mbunifu

Ubunifu ni kitu gani? Kuna haja ya kuwa mbunifu?   Wanasayansi wanaelezea  ubunifu kama uwezo wa kuzalisha mawazo mapya yenye kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya kila siku. Kama wewe ni mdadisi wa mambo utakubaliana na mimi kwamba, kwa sehemu kubwa, maisha magumu uletwa na ukosefu wa ubunifu.   Maana yake, kushindwa kuzalisha na kufanyia kazi mawazo

Njia 3 za Kiafya za Kuwa Mbunifu Read More »

Madhara Matano ya Uzito Mdogo 

Mara nyingi tukiongelea uzito watu wengi huangalia uzito mkubwa kama tishio kwenye afya.   Ulishawahi kujiuliza mtu akiwa na uzito mdogo kupita kawaida ina athari gani kwenye afya? Usiumize kichwa sana kwasababu makala hii itakupa majibu ya swahi hilo.    Uzito kiasi gani huesabika kama uzito mdogo? Jibu ni kwamba hakuna uzito maalum unaohesabika kama

Madhara Matano ya Uzito Mdogo  Read More »

en_USEN