Ansbert Mutashobya, MD

Chief Content Officer (CCO) at Abite Afya I'm responsible for overseeing the entire content strategy, ensuring that all published materials align with the blog’s mission, audience needs, and business goals.

Nani Mwenye Jukumu la kudhibiti Malaria Kwenye Jamii Yangu?

“Kama Baba Mateso angekuwa ananunua dawa ya mbu ya kuchoma mara kwa mara, familia hii tusingekuwa na Malaria!”  Mama Mateso akiwa analalamika.  Unatamani umuulize swali: Jukumu la kukinga familia dhidi ya malaria ni la nani?   Mama Mateso ni mama wa familia na Mwenyekiti wa Mtaa wa kiongoleni, Kata ya Goba. Familia yake inawindwa sana na […]

Nani Mwenye Jukumu la kudhibiti Malaria Kwenye Jamii Yangu? Read More »

Bima ya Afya kwa Wote

Kuanzishwa kwa “Bima ya Afya kwa Wote” Tanzania: Itanisaidiaje?

Tanzania imeanza utekelezaji rasmi wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote (UHI Act, 2023)  mwanzoni mwa mwaka huu wa 2026. Haya ni mapinduzi katika sekta ya afya yanayolenga kumgusa kila mtanzania. Kabla ya kutazama kwa undani tuanzie hapa: Watanzania tuko katika makundi mawili: Kuna wale ambao wakiumwa hawana wasiwasi, wanajua bima yao ipo. Watu

Kuanzishwa kwa “Bima ya Afya kwa Wote” Tanzania: Itanisaidiaje? Read More »

Jinsi Ukosefu wa Elimu ya Dharula Unavyogharimu Maisha ya Watanzania

Kila mtu atakufa, hilo halina ubishi kabisa. Swali ni kwamba, utakufa lini? Utakufaje ? Katika mazingira yapi? Je, unaamini kuna vifo vinavyosababishwa na ukosefu wa elimu?  Leo hii ukipatwa na dharula ya mtu wako kuanguka ghafla au ukikutana na mtu amedondoka ghafla utachukua hatua gani? Kuwa mkweli, utaita gari ya dharula au utamuitia bajaji?  Katika familia nyingi za kitanzania, mgonjwa akianguka au kuzidiwa ghafla huwa hawakumbuki gari ya dharula (ambulance) bali watampakia haraka kwenye gari au boda na kumkimbiza  hospitali.  Kulingana na makadirio ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa mwaka 2025/2026, takriban watu 10,000  hupoteza maisha kila mwaka nchini Tanzania kutokana na ajali za barabarani.  Ripoti ya World Bank na UN Road Safety Fund (2024) inaonyesha kuwa idadi kubwa ya vifo  hivi  hutokea  kabla  ya kufika hospitalini (pre-hospital deaths).  Wagonjwa wengi husafirishwa kwa kutumia bodaboda, taksi, au magari ya polisi ambayo hayana vifaa  vya kuimarisha hali ya mgonjwa (resuscitation equipment) wala watumishi wenye ujuzi.  Udhaifu  mkubwa wa mpango wa dharula kuanzia kwenye elimu kwa jamii, mpango mzima wa kuchukua hatua za mapema, ukosefu wa elimu ya huduma ya kwanza (First Aid) kwa madereva  na miundombinu kama barabara ambayo sio rafiki kwa dharula ni vyanzo vikubwa vya vifo hivi. Tanzania imechukua hatua gani katika kuongeza ufanisi wa huduma za dharula? Tanzania kupitia Wizara ya Afya inafanya juhudi kubwa kuhakikisha inaboresha kitengo cha dharula lengo likiwa ni kupunguza idadi ya vifo nchini. Baadhi ya mambo ambayo Wizara ya Afya inafanya kazi kubwa kuboresha katika idara ya dharula ni kama ifuatavyo: 

Jinsi Ukosefu wa Elimu ya Dharula Unavyogharimu Maisha ya Watanzania Read More »

Nasumbuliwa na UTI Kila Mara, Nifanyeje?

Bila shaka swali kama hili sio geni kwako au inawezekana na wewe ni muhanga wa changamoto hii. Unapambana nayo vipi? Au unaishi nayo tu kama kawaida? Binafsi kama daktari nimekutana na wagonjwa wa namna hii mara kwa mara na nimekuwa nakijitahidi kutoa elimu ili kuhakikisha kila ninayekutana nae anapata msaada.   Kama wewe ni miongoni mwa watu ambao wanahisi UTI yao haiponi na inajirudia mara kwa mara basi usiache kusoma makala hii mpaka mwisho. Itakusaidia kupata njia sahihi ya kupita; njia namba tano itakushangaza.  Neno UTI ni kifupisho cha neno la kiingereza lijulikanalo kama Urinary Tract Infection, yaani maambukizi ya njia ya mkojo. Maambukizi haya, mara nyingi, husababishwa na bakteria mbalimbali

Nasumbuliwa na UTI Kila Mara, Nifanyeje? Read More »

Nikiungua Moto Nichukue Hatua Gani za Mapema?

Jamii ina utaratibu wake wa kufanya pale mtu anapoungua. Wewe unajua upi? Kwenye utamaduni wangu nimekuwa nikiona mtu akiungua anamwagiwa mkojo kwenye sehemu aliyoungua na imekuwa ikiaminika kwamba inasaidia.   Wengine huwa wanawahi kuweka asali sehemu iliyoungua wakiamini ni msaada mkubwa.  Wengine mafuta ya taa, petroli na kadhalika. Ninyi kwenu huwa  mnafanyaje?  Kuungua ni tukio

Nikiungua Moto Nichukue Hatua Gani za Mapema? Read More »

Mkojo Unakataa Kutoka? Tezi Inaweza Kuwa Sababu!

Tezi dume ni nini? Kila mwanaume huzaliwa na tezi. Tezi hii ni kiungo katika mfumo wa mkojo ambacho hufanya kazi ya kutoa majimaji (semens) ambayo husaidia shahawa za kiume kuogelea wakati wa  kutoka nje kupitia kwenye njia ya mkojo.  Pia maji hayo husaidia kuandaa njia ya mkojo kuondoa ule utindikali na hivyo kusaidia shahawa kupita

Mkojo Unakataa Kutoka? Tezi Inaweza Kuwa Sababu! Read More »

Nitagunduaje Dalili za Mapema za Malaria?

“Sio kila homa ni malaria bhana” ni kampeni maarufu sana ambayo Wizara ya Afya imekuwa ikiitumia mara kwa mara kuwakumbusha wananchi kuacha kununua dawa na kujitibu kiholela na pia kwenda mapema kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kupima ili kuthibitisha uwepo wa vimelea kabla ya kutumia dawa ili kuepuka changamoto kubwa zinawoweza kujitokeza kwani

Nitagunduaje Dalili za Mapema za Malaria? Read More »

“Sitaacha tena kutumia chandarua chenye dawa maishani mwangu”

Nilipokuwa mdogo nilikuwa nashangaa kwanini tusipoweka chandaru baba anatugombeza sana! Mzee alihakikisha anapita chumbani kila usiku na kama chndarua hakijawekwa vizuri alikuwa anakirekebisha na kuhakikisha tuko ndani ya vyandarua.     Na kweli kwa wakati huo sikumbuki lini nimelazwa hospitali kwasababu ya malaria.   Mwaka 2012 nilipojiunga na Chuo Kikuu, nilikutana na utaratibu tofauti: rafiki

“Sitaacha tena kutumia chandarua chenye dawa maishani mwangu” Read More »

Kiharusi: Nini Hutokea Baada ya Kukipata? 

Bila shaka huwa una tabia ya kujifunza namna ya kuepuka magonjwa mbalimbali kama malaria, UKIMWI, kaswende, kansa, n.k. Lakini ulishawahi kujifunza namna ya kujikinga na kiharusi (stroke)?   Kama bado basi nakusihi uanze sasa kujua namna gani ya kujikinga na changamoto ya kiharusi kwasababau sio ugonjwa mzuri na una matokeo hasi sana ikiwa utaupata.   

Kiharusi: Nini Hutokea Baada ya Kukipata?  Read More »

en_USEN