Kwanini Nashindwa Kupata Ujauzito?

Je, unatamani kushika ujauzito? Au uko kwenye safari ya kushika ujauzito, kupandikiza mtoto (IVF) au kupata mimba kwa njia asilia? Unafahamu kuhusu ubora wa yai (egg quality)?

 

 

Kuwa na yai lenye ubora unaotakikana (quality egg/sperm) ndio jibu na njia ya mafanikio. Wengi katika safari ya ugumba au kujaribu kushika mimba naturally au kujaribu kuzaa tena baada ya muda au baada ya kutumia uzazi wa mpango wanakutana na dhoruba ya kuharibika kwa mimba, au kuchukua muda mrefu, kuandikiwa dawa nyingi, kushauriwa kutumia virutubishi mbali mbali, na kadhalika.

 

Haya yote yanasaidia lakini wengi tunasahau kuangalia na kuzingatia ubora wa mayai yetu kabla ya kuendea jambo la kujaribu kushika ujauzito.

 

Makala hii haitakusudia kutoa ushauri wa kitaalamu, inashauriwa kumuona mtaalamu wa uzazi na magonjwa ya akina mama hasa wabobezi katika embryology.

 

Back to the egg quality…

More often than not, matibabu ya ugumba yanajikita sana katika kuhakikisha yai linakomaa na kutoka kwenye ovari, kuhakikisha mbegu ya kiume inachavusha yai la kike kwa wakati na kutayarisha mji wa mimba ili kushika ujauzito, ili kupata mtoto.

 

Lakini, kama yai linaweza kukomaa na kuchavushwa na mbegu ya kiume lakini ikawa ngumu mimba kutunga basi hali ya yai au mbegu ya kiume sio nzuri.

 

Inaaminika kuwa wanawake tunazaliwa na mayai yote tutayoishi nayo mpaka kufa, wakati Wanaume wanatengeneza mbegu zao baada ya kubalehe hadi kufa. Hii ni kweli kabisa lakini mayai ya wanawake huwa hayajakomaa yote au hayakomai yote kwa wakati mmoja, inachukua takribani miezi mitatu au minne kukomaa yai kabla halijatoka kwenye ovari na kuchavishwa na mbegu ya kiume.

 

Katika miezi hiyo ni muhimu sana yai kuendelea na process ya kutengeneza vinasaba (DNA) na kuwa katika quality nzuri ili apatikane kijusi (embryo) mwenye afya ambaye ataweza kukua na kujishika katika mji wa mimba vizuri na kukua kuwa kiumbe kamili.

 

Nini kitatokea ikitokea hitilafu yoyote?

Hitilafu yoyote katika kipindi hicho itasababisha kijusi (embryo) mwenye mapungufu ya vinasaba na kusababisha kuharibika kwa mimba ndani ya miezi mitatu ya kwanza au mtoto mwenye shida.

 

Kwa watu wanaojaribu kufanya IVF, hii hupelekea poor quality embryos ambao hawawezi kupandikizwa au embryo ambaye anashindwa kuishi kwenye mji wa mimba wa mama au surrogate, which ends up into negative pregnancy test after two weeks of embryo transfer.

 

Na tafiti zinaonesha mpaka asilimia 70% ya kufeli kwa upandikizi wa kijusi unajirudia kwa wanawake.

 

Pia, hitilafu hizi za vinasaba zinazotokea kipindi yai linakomaa zinapelekea kuharibika kwa mimba na mara nyingi mimba inatoka kabla ya mwanamke kujigundua kwamba ni mjamzito. Inakaridiwa ni zaidi ya asilimia 50 ya mimba zinazotoka katika theluthi ya kwanza ya ujauzito zinasababishwa na hitilafu za vinasaba (chromosomal abnormalities).

Na nyingi kati ya hizi hitilafu zinasababishwa na mitindo ya maisha, lishe na mazingira mtu anayoishi hasa kipindi ambacho yai linaanza mchakato kwa kukomaaa na kupevuka katika mzunguko wa hedhi ya mwanamke.

Uhusiano kati ya ubora wa mayai na upungufu/wingi wa mayai

Ili hali inajulikana kisayansi kuwa wanawake wa zaidi ya miaka 40, mayai yao yamepungua sana (reduced ovarian reserve), hii ni tofauti na ubora wa mayai (egg quality) kwa kuwa inawezekana kabisa kuwa na mayai machache lakini yenye ubora mzuri.

 

On the contrary, msichana wa miaka 20 anakua na mayai mengi ya kutosha lakini kama ana poor egg quality bado itakuwa changamoto kwake kushika mimba. Kwa hivyo, ni muhimu kutofautisha kati ya wingi wa mayai (ovarian researve) na ubora wa mayai (egg quality) ili kuelewa namna gani unaweza kuongeza nafasi yako au ya mwenza wako kushika mimba.

 

Uhusiano kati ya kuharibika kwa mimba na vinasaba

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa wanawake wenye umri zaidi ya miaka 40, nusu ya mayai yao tayari yana hitilafu za vinasaba kwa asilimia 70-80%. Lakini, hata wenye umri chini ya miaka 35, karibu robo ya mayai yote walionayo yana hitilafu za vinasaba.

 

So, the chances are wakati wa mzunguko wa hedhi mayai yanayokua na hitilafu za vinasaba yanakaribiana kuchavushwa na yale yasio na hitilafu. Kumbuka kuwa yenye hitilafu ni ngumu sana kutengeneza kijusi, na haya yasio na hitilafu kama hayana ubora mzuri pia ni ngumu kutengeneza kijusi na ndio maana inakua ni ngumu kwa baadhi ya wanawake kushika mimba.

 

Ugumu unaongezeka zaidi kadri umri unavyozidi, na ni ngumu zaidi kwa wanaojaribu kupata mtoto kupitia upandikizaji kwani asilimia 24-30% ya mimba zinazoharibika kwa wanaopandikiza ni kwa sababu ya hitilafu za vinasaba.

 

Haitoshi tu ukuaji wa kijusi kutosha kuwa ni sababu ya kupandikiza bali pia ubora wa kijusi chenyewe kwa maana vinasaba vyake ni muhimu zaidi kuzingatiwa ili apatikane mtoto mwenye afya.

 

Utafiti uliofanyika kuangalia uhusiano kati ya kuharibika kwa mimba na vinasaba ulionyesha kuwa hitilafu za vinasaba ilikua mkubwa kwa vijusi vya kiume kwa asilimia 54.14% na vinasaba venye hitilafu vilionekana zaidi kwenye mfuko wa yai pekee (yolk sac) karibu mara mbili zaidi ya kundi lingine.

 

Hii ni wazi kuwa mayai ya mwanamke yakichafuliwa (contaminated), yasipokua na ubora unaotakiwa wakati wa kuchavulisha (fertilization), chances are mimba itabaki kuwa ni ndoto kwa familia nyingi.

 

Vitu vya kuzingatia kabla hujaanza kutafuta mtoto kwa njia ya kupandikiza

Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa vijusi vyenye vinasaba sahihi/kamili ndio vyenye nafasi ya kujishikiza katika mji wa mimba na kukua mpaka mtoto kuzaliwa. Na hasa wanaopandikiza au kutarajia kupandikiza, bila ya kufanya uchunguzi wa vinasaba vya vijusi, yawezekana kupandikiza kijusi chenye hitilafu za vinasaba na kuhatarisha uwezekano wa kushika ujauzito.

 

Katika wengi wanaofanikiwa na zoezi la IVF, inawezakanaa wanaopata changamoto ya kutopata ujauuzito ni sababu ya ubora hafifu wa kijusi unaotokana na ubora hafifu wa mayai aidha ya mama au baba.

 

Na hata wanaojaribu kupata mimba kwa njia ya kawaida, bado ubora wa mayai unahitajika kwa kiasi kikubwa. Msisitizo wa IVF na egg quality ni shauri ya gharama kimwili, kiakili, kifedha na kijamii katika kuhakikisha mtoto anapatikana.

 

Hata hivyo, tukumbuke kuwa uhusiano wa ubora wa kijusi na ubora wa mayai na hitilafu za vinasaba vinaweza kutokea kwa mtu yeyote wa umri wowote as oppose to ovarian reserve. Inategemea mazingira, aina ya maisha, chakula, exposure ya sumu na mambo mengine mengi katika maisha ya kila siku.

 

Wanawake wawili wa umri unaolingana wanaweza kuwa na ovarian reserve tofauti na egg quality tofauti na pia wenza wao wanaweza kuwa na umri sawa na kuwa na quality ya sperm tofauti. Ndio maana hata couples of the same age trying to concieve at the same intervals and time wanaweza kupata matokeo tofauti ya ujauzito ikizingatiwa lifestyle wanayoishi na sababu zingine za kibaolojia.

 

Je, inakuaje mpaka yai linapoteza ubora wake ili kupata kijusi na hatimaye mtoto mwenye afya?

 

Tukutane kwenye makala ijayo itakayoelezea kwa kina sababu mbalimbali zinazoweza kupelekea ubora hafifu wa yai.

Leave a Comment

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

swSW