Calvin ni kijana wa miaka 28, afisa mifugo anayeishi Sanawali Arusha. Katika maisha yake amekuwa na mikasa sana na wanawake. Kila akipata demu mpya, baada ya mwezi mimba! Mpaka sasa ana watoto 6 mtaani achana na wale ambao mademu zake waliamua kutoa mimba.
Nilikutana nae maeneo ya Players Hotel, Njiro Arusha, na wakati tunapata moja moto, ndipo akanisimulia baada ya kugundua mimi ni Daktari.
Baada ya kusimuliwa msala wake nikagundua hii inshu ni janga kubwa ambalo linawakumba vijana wengi mjini. Je tatizo ni nini? Vijana wanakwama wapi? Ni vitu gani vinaweza kusababisha mikasa hii ya kina Calvin?
1. Kukosa nidhamu ya maisha
Kukosa nidhamu haimaanishi haueshimu watu, bali hauishi kulingana na misingi ambayo ina heri. Embu jiulize umekutana na demu siku ya kwanza au hata ndani ya mwezi na umefanya naye sex bila kinga. Hiyo ina maana gani? Uwezo wako wa kujenga hoja kichwani na uwezo wa kuendesha hisia zako ni mdogo.
Hali hii husababishwa na kukosa nidhamu ya maisha. Katika maisha kila mtu huwa na ndoto, na ndoto ulizonazo lazma uziwekee mazingira ya kuzilinda kwa kujiwekea kanuni ambazo zitakukinga kushindwa kufikia malengo yako.
Usipokuwa na kanuni hizo basi hujikuta unafanya mambo ambayo huja kuharibu maisha yako ya baadaye.
Kabla hujafanya sex na mwanamke bila kondomu jua yafuatayo:
Kwanza, wanawake wengi hawajui kusoma siku zao za hatari, hivyo kufanya sex kavu unakuwa na asilimia zaidi ya 60 ya kumpa mimba.
Pili, kupata watoto wengi mapema inaweza kuwa chanzo cha umaskini katika maisha yako. Unapaswa kuwa na nidhamu ya maisha kwa kujitengenezea kanuni salama na sahihi, na kuweka mbele malengo yako kuliko hisia.
Nawezaje kuwa na nidhamu ya maisha?
Nidhamu ya maisha ni namna ya kuishi katika misingi fulani kwa ajili ya kuyafanya maisha yako yawe na mtiririko mzuri. Kuwa na nidhamu ya maisha ni pamoja na kuweza kutawala hisia zako. Unajua kwamba asilimia 90 ya mambo unayofanya yanatokana na hisia zako?
Sasa kuna muda hisia zako zinazidi utashi wako na hapo ndipo unajikuta umefanya mambo yasiyo sawa.
Nikuulize swali? Ulishawahi kujinyima kitu gani muhimu katika maisha yako ambacho roho inatamani ila kwa ajili ya kuepusha majanga ukakipotezea?
Ulishawahi kufunga kula walau kwa masaa 12? Au kujinyima kununua pombe kwa ajili ya kutunza pesa? Ni kitu gani uliwahi kujinyima?
Basi huu ndio mfano wa nidhamu katika maisha. Maana yake uwe na uwezo wa kukataa au kupunguza au kujinyima kabisa kitu muhimu au kitamu au kinachokupa raha kwa manufaa ya baadaye.
Ni kweli kufanya sex bila condom kuna utamu zaidi, lakini ukilinganisha utamu ule na kulea mtoto asietarajiwa, hapo ndipo unapoamua kupunguza utamu kidogo kwa kuvaa condom ili kuepuka madhara ya baadaye. Kuweka starehe mbele kuliko matokeo ya starehe ni ukosefu wa nidhamu ya maisha na lazima itakugharimu.
Mfano, ulishawahi kukutana na mtu mahali, mkaelewana, na ndani ya muda mfupi mkafanya sex bila kinga? Mkiwa mnafanya mnafurahia sana lakini huwa unajisikiaje baada ya kumwaga? Nafsi yako huwa inaanza kukusuta na hofu inakuingia unaanza kuwaza: Kama nimempa mimba je? Itakuwaje kama nikipata magonjwa?
Hali kama hii ndiyo watu wanaoamua kufanya ngono salama huwa wanaikwepa. Majuto baada ya tendo. Baada ya tendo unapaswa ujiskie furaha, sio huzuni. Mwili siku zote unapenda raha, lakini raha kamili huja pale unapokuwa na uwezo wa kuzitawala hisia zako.
Anza kujenga nidhamu yako kwa kufanya yafuatayo
- Kufunga kula walau kwa masaa 10 mpaka 16 ndani ya masaa 24 kila siku. Ukiweza hilo utagundua kwamba uwezo wako wa kujinyima vitu vingine utaongezeka. Kama unaweza kujinyima chakula, amini, unaweza kujinyima na starehe zingine kama ngono.
- Anza kuamka mapema mfano saa 11 alfajiri. Itakujengea nidhamu Pia. Hakuna kitu kitamu kama usingizi wa asubuhi, hivyo ukiweza kujitesa katika style hiyo, utakuja kugundua kwamba uwezo wako wa kujitawala umeongezeka.
Muhimu: Ongeza lengo kwenye kuamka, kama kujisomea kitabu au kuandaa mipango ya siku mpya, sio kuamka saa 11 alfajiri kwenda TikTok – huo utakua ni upotevu wa muda.
- Anza mazoezi ya gym au kukimbia. Unajua maumivu yanayotokana na gym? Misuli kuuma na uchovu wa mwili. Ukiweza kuvumilia maumivu hayo basi utajikuta umejenga subira kubwa na itakupa uwezo wa kuzitawala hisia zako.
Ukiweza kuwa na nidhamu ya chakula, usingizi na mazoezi basi uwezo wa utashi wako utaongezeka. Utaanza kuzitawala hisia zako na utaanza kuyatawala mawazo ya mapenzi. Pia itakusaidia kufanya maamuzi sahihi ya kujilinda na maradhi na kuzikwepa mimba ziszo na mpango.
2. Kondomu iwe kawaida kwako
Jiwekee standard kwamba kondomu ni lazima. Tembea nazo kwenye gari, begi, ofisini au popote pale. Jiwekee marufuku kufanya mapenzi bila kondomu. Ni maamuzi tu na ukifanya mazoea itakuwa tabia yako na utaona kawaida tu.
Unataka kupima uwezo wako wa kutawala hisia zako? Unataka kupima kama wewe ni mtu mwenye nidhamu na malengo? Angalia unatumia kondomu mara ngapi ukikutana na mwanamke? Kama wewe ni kanyaga twende basi nikwambie tu utalea watoto wengi wasio wako na utatumia gharama kubwa kutoa mimba au kutibu gono.
Hebu piga hesabu, kondomu Tshs 1,000 mpaka 3,000 wakti kutoa mimba sio chini ya TShs 70,000 au kutibu gono sio chini ya TShs 25,000. Piga picha ungeweka kawaida kwa kutumia kondomu, ungeruka vihunzi vyote hvyo.
Unajua kutumia kondomu vizuri?
Matumizi sahihi ya kondomu ni muhimu katika swala zima la kujilinda na kutowapa wanawake mimba zisizotarajiwa. Vitu vinavyoweza kusababisa kumpa mwanamke mimba ni pamoja na kondomu kupasuka wakati wa tendo. Unapokuwa unatumia kondomu ni vema kuwa makini na kutofautisha msuguano.
Kondomu inaweza kupasuka kwa sababu mbalimbali mfano kutumia kondomu moja kwa muda mrefu au matumizi ya vilainishi kwenye kondomu kama mafuta ya Vaseline, mafuta ya uto na kadhalika.
Vilainishi pekee vinavyoweza kutumika ni vilainishi maji kama K-y gelly. Kuhusu mate sina uhakika, ila mate yanakuwa na bakteria wa mdomoni ambao ukiwahamishia kwenye uke inaweza kuleta madhara.
Ishu nyingine ni matumizi yasiyo sahihi ya kondomu. Mfano katika uvuaji wa kondomu ni vyema kuwa makini kushika vizuri juu na chini. Ukitaka kuvua kondomu, kaa mbali na uke wa mwanamke halafu vua kwa kuvuta ile chuchu ya kondomu na hakikisha hakuna shahawa zinazoruka kwenda kwenye uke.
Kumbuka: Shahawa zikimwagika hata kwenye paja la mwanamke bado zina uwezo wa kwenda kwenye uke na kusababisha mimba.
Ukimaliza kuvua, safisha mikono yako kabla hujavaa kondomu nyingine. Ukigundua kondomu yako umeigeuza wakati unajaribu kuivaa na sehemu iliyopaswa kwenda kwenye uke imegusa uume wako basi kondomu hiyo usiigeuze na kuitumia tena, itupe vaa mpya, inawezekana imebeba baadhi ya shahawa zako na ukigeuza na kuitumia inaweza kusababisha mimba.
Nikuibie siri…
Kondomu huweza kupunguza msuguano hivyo hukuchelewesha kidogo kumwaga ukilinganisha ukiwa haujavaa. Kuchelewa kidogo huku hukufanya umpe mwanamke kazi ya daraja la juu na ni rahisi kumfikisha kileleni kuliko ungefanya peku.
Pia kutumia kondomu kunaipa uume wako uwezo wa kusimama tena baada ya kumwaga, tofauti na ukimwaga peku ambapo unapoteza nguvu na shahawa nyingi hivyo huathiri uwezo wako wa kurudi raundi ya pili.
Kutumia kondomu pia humfanya mwanamke kurelax na hivyo atakupa utundu wote kwasababu anajua yuko salama. Moja ya hatari ya kufanya sex na mwanamke mwenye wasiwasi wa mimba au magonjwa huwa ni uke mkavu ambao huongeza hatari ya michubuko wakati wa tendo.
Siri nyingine, mwanamke akigundua unapenda kutumia kondomu basi atakuona mtu mwenye msimamo sana na hivyo atakuelewa na ukimcheki tena, hawezi kukataa kukupa. Sasa ukiwa mzee wa peku, next time atakuogopa maana anajua unakutana na wengine peku hivyo unaweza ukampa maradhi au mimba.
3. Jua mzunguko wa hedhi wa mwanamke wako
Kujua mzunguko wa mwenza wako na kuweza kutambua ni mida gani anakuwa hatarini kupata mimba ni muhimu sana. Jua kwanza mwenza wako ana mzunguko wa siku ngapi? Zihesabu na ujue anakuwa katikati wakati gani? Kumbuka siku ya kwanza ya mzunguko huwa ni ile siku ya kwanza ya hedhi.
Lazma ujue kama siku zake za mzunguko (menstruation cycle) zinafika 28 (mwezi mpaka mwezi) au siku 21, au siku 35.
Mfano: 1-2-3-4-5-6-7-8-9-10-11-12-13-14-15-16-17-18-19-20-21-22-23-24-25-26-27-28.
Unataka kujua siku ambayo yai lake litatoka (Ovulation)? Hesabu siku 15 kuanzia tarehe ya mwisho 28 kurudi nyuma, hiyo ndiyo tarehe ya hatari zaidi. Mfano hapo juu anzia 28 kurudi nyuma kwa kuhesabu siku 15, utaangukia tarehe 14.
Basi hii ndiyo siku yai la mwanamke hutolewa. Siku hii inaitwa ovulation day. Ndiyo siku hatari zaidi kwa mwanamke kupata mimba. Lakini kuwa makini na yafuatayo:
Mbegu ya mwanaume (shahawa) huweza kuishi siku tatu na zaidi kwenye mirija ya uzazi na yai lenyewe linapotolewa huwa linapaswa kukutana na mbegu ya kiume ndani ya masaa 24, baada ya hapo hufa.
Kutoka kwenye huo mzunguko hapo juu, ukifanya tendo kuanzia tarehe 10 kuna uwezekano mbegu zako zikawa bado ziko hai mpaka tarehe 14 yai likitoka hivyo kuna uwezekano wa kumpa mimba mwanamke wako. Lakini pia ukifanya tendo tarehe 15 bado uwezekano wa kupata mimba ni mkubwa kwasababu yai ndio kwaza lipo ndani ya masaa 24 toka lizalishwe.
Kwa haraka utagua kwamba kama unajua mzunguko haupaswi kufanya sex bila kondomu siku 4 kabla ya siku ya 14 na siku mbili baadaye. Walau hizo siku 6 unapaswa usifanye au utumie kondomu. Kwa kujua mzunguko huo unaweza kujua pia ni siku zipi unaweza kumpa mimba mwanamke kama mnatafuta mtoto. Kwa maelezo zaidi jaribu kuniuliza Baadaye.
Je kama mwanamke wangu hedhi yake huanza tarehe 8 na mzunguko wake ni siku 28?
Hapa hesabu kwanza siku 28 kutoka hiyo tarehe ili ikusaidie kujua ovulation day.
Mfano: 8-9-10-11-12-13-14-15-16-17-18-19-20-21-22-23-24-25-26-27-28-29-30-31-1-2-3-4
Hesabu kwanzia 4 tarakimu 15 kurudi nyuma, utagotea tarehe 21 ambayo sasa ni ovulation day. Maana yake hupaswi kufanya peku kuanzia tarehe 17, 18, 19, 20, 21, 22 (hizi ndizo siku za hatari).
Kwa wenye mzunguko wa tofauti mfano siku 21 au 35 ni vizuri kutumia njia zingine za mpango maana mahesabu yao huwa ni magumu na huweza kupata mimba hata wakiwa katika siku zao, kuwa makini.
Pamoja na kufahamu mzunguko, tatizo ni kwamba mzunguko unaweza kubadilika muda wowote. Hivyo mwanamke bado anaweza kupata ujauzito muda wowote bila kujali mzunguko, hivyo njia zingine za uzazi wa mpango kama kijiti au sindano ni muhimu.
Nikupe kaujanja kidogo…
Unapaswa uzijue dalili za mwanamke ambaye yuko kwenye siku za hatari. Kwanza huwa na hamu ya mapenzi iliyopo juu kuliko kawaida, atakutumia message za mapenzi siku nzima na atakwambia anakuhitaji sana, hapo kidume shtuka, nunua kondomu zako mapema kabisa, huyo yupo kwenye hatari.
Kuthibitisha hilo ukikutana naye ukimgusa tu utagundua mwili wake una joto zaidi yaani ni wa moto balaa! Weka kondomu zako karibu kama hatumii njia zingine za uzazi wa mpango.
Wakati unafanya romance utagundua kwamba sehemu za uke wake zimelowa sana – na ute mzito – na hata hujamchezea kivile. Shtuka vaa kondomu yako, huyu yuko kwenye hatari ya kubeba mimba.
Kiufupi ukiona siku mwanamke wako anakuhitaji sana na muda mwingi mko pamoja lakini siku hiyo hamu yake imezidi, kama hayuko kwenye uzazi wa mpango, tumia kondomu, mara nyingi atakuwa kwenye siku yake ya hatari, inahitaji udadisi na uzoefu kuyajua hayo na ndio maana nakupa Elimu.
4. Epuka matumizi ya vilevi kila unapokutana na mwanamke
Tafuta namna nyingine ya kujiamini na sio vilevi. Kama unavojua kilevi hupunguza uwezo wako wa kufikiri na hukuweka katika hatari ya kutotumia kinga hasa nyote mkiwa mmelewa. Tenganisha siku za kunywa ziwe tofauti na siku za kufanya mapenzi ili kuepuka majuto baadaye.
Nikigundua jana yake sikutumia kondomu na nilimwaga shahawa ndani, nifanyeje?
Shauriana na mwenza wako mkanunue kidonge cha emergency morning pill ambacho huzuia mimba kikimezwa ndani ya masaa 72 baada ya tendo. Dawa hii huwa na msaada mkubwa kuepuka mimba zisizotarajiwa. Utaisoma vizuri kwenye topic nyingine ya matumizi ya dawa za majira.
Mwisho
Hakuna kitu kinacholeta wasiwasi kama mimba isiyotarajiwa. Huleta msongo wa mawazo. Unaweza kuchanganyikiwa.
Lakini pia kuwapa wanawake mimba kiholela itakugharimu kimaisha. Wakikupeleka ustawi wa jamii lazma utayumba tu kiuchumi.
Kuwa mtu muwajibikaji. Kuwajibika kwa ajili ya afya yako, kwa ajili ya mwanamke wako na jamii inayokuzunguka kwa kufanya ngono salama.
Muhimu: Kuna njia nyingine za withdrawal method ambazo unaweza kujifunza na zikakusaidia – japo ni ngumu. Nitaziongelea kwenye mada zijazo.

Chief Content Officer (CCO) at Abite Afya
I’m responsible for overseeing the entire content strategy, ensuring that all published materials align with the blog’s mission, audience needs, and business goals.
Imekaa poa sana..
I’m not sure exactly why but this web site is loading extremely slow for me.
Is anyone else having this problem or is it a problem on my end?
I’ll check back later on and see if the problem still exists.
seraphina.top
Hey Saraphina.
Sorry for any inconvenience you’ve encountered. We had some maintenance to do on our site these last 2 weeks.
Speed will be back normal ASAP.
Sorry again…and thanks for checking our site.