Mambo Matatu Yanayofanya Wagonjwa Wamuamini Daktari 

Dunia inakwenda kasi sana na mambo yanabadilika, lakini katika taaaluma ya udaktari kuna mambo hayapaswi kubadilika mpaka mwisho wa dunia.

 

“Heshima ya mgonjwa au ndugu wa mgonjwa kwa daktari” 

 

Ulishawahi kuheshimiwa na mgonjwa au ndugu zake? Ile hisia ya heshima inaweza kukufanya ujione daktari bora kabisa na hata zile shule ulizozisahau zinaanza kurudi zenyewe kichwani. 

 

Ulishawahi kudharauliwa na mgonjwa au ndugu yake? Unaweza kujiona wa bure kabisa na pengine hata kujuta kwanini umekuwa daktari. 

 

Asikudanganye mtu, heshima ya wagonjwa au ndugu zao kwako ni jambo muhimu sana na lazima uitengeneze. Yafuatayo ni mambo matano ambayo ni lazima kwako ili uheshimike kama daktari: 

 

1. Muonekano  

Daktari muonekano wako ukoje? Unavaa koti la aina gani? Lina viwango? Kuwa daktari sio jambo la kubeza, lina hadhi yake. Sasa kama unavaa matambala unakosea sana.

 

 

Kutokana na ubize wa daktari ni lazima uwe na makoti mazuri mawili ambayo unabadili kila baada ya siku mbili. Koti liwe refu kidogo na jeupe kabisa linakupa uhuru wa kumtibu mgonjwa na kufunika mavazi yako vizuri. 

Kiatu chako kiwe kizuri sio kilichoisha sole. Viatu vilivyoisha sole huonyesha ugumu wa maisha ulionao na hivyo mgonjwa anaweza kukufokea akijua ni kapuku.

Vaa kiatu kizuri; kama huna kiatu kizuri bora uvae hata crocks. 

 

Una scrab? Scrab nayo ni muhimu na lazima kwa daktari yeyote.

Sio lazima kila siku uning’inie na makoti hasa ukiwa idara kama Opd na Causality. Hizi ni idara zinazohitaji uharaka, pia ni rahisi kurukiwa na damu na/au matapishi.  

 

Ukiwa na scrab nguo zako hazitachafuka na unaweza kuzirudia tena siku ya pili. Ukiwa nazo kama rangi mbili tofauti itakupa muonekano tofauti na kila siku utaonekana mpya.  

 

Hii inawafanya watu wanaokuzunguka kama wagonjwa na manesi wapende kukuona mara kwa mara na kazi yako itakuwa rahisi sana. Vyote hivi vitakupa kujiamini. 

 

Napata wapi koti zuri na scrab? 

JG Heritage wanatengeneza makoti na scrub za kisasa kwa bei nzuri. Zaidi wanakuwekea na jina lako kabisa (embroidery) kuepusha nguo zako kupotea. 

 

Unaweza kuwasiliana nao kwa njia ya simu kupitia namba +255 759 892 615. Kwa kuangalia kazi zao walizozifanya, tembelea kurasa yao ya Instagram hapa. 

 

2. Vitendea kazi  

Vitendea kazi vyenye uhimara vinampa daktari kujiamini na kufanya kazi yake kwa uhakika. Daktari wa kisasa ni muhimu kuwa na Litman stethoscope walau class 3.  

 

Litman stethoscope

 

Hii mashine itakufanya upate details zako vizuri na kutoa majibu yako kwa kujiamini. Daktari mzima bado unatumia vile vi’stethoscope vidogo kuiskia mpaka ubonyeze kwenye maskio? Sio sawa kabisa!

 

Class 3 Litman unapata sauti hata ukiweka tu juu ya kifua na hivyo hutumii nguvu kupata details.

 

Embu daktari jitutumue walau nawewe uwakilishe vizuri na utoe majibu ya usahihi. Hii iyambatane na kuwa na BP machine yako binafsi; thermometer pulse oximeter.

 

Imagine jirani zako wanajua wewe ni Daktari, wanakuita mama hajisikii vizuri halafu wewe huna hata BP mchine, huna pulse oximeter wala thermometer, utajiskiaje? Utajitetea sana lakini ni aibu tu.

 

Hakuna mvuvi anayekosa ndoana nyumbani kwake. Jenga heshima yako kwa kuwa na walau vifaa vichache kama hivi. 

 

Nitapata wapi vifaa kama hivi? 

Jibu ni moja tu, JG Heritage! Wamebobea sana kwenye vifaa tofauti tofauti  vya madaktari.  

Kwa taaarifa zaidi, tembelea kurasa yao ya Instagram hapa. 

 

3. Elimu  

Siri kubwa ya Daktari anayeamininika huwa ni kujielimisha kila mara na kuweza kuwa na uwezo wa kutatua changamoto ndogondogo za wagonjwa na watumishi wenzake.

 

Mfano, kujua dozi au vipimo fulani. Kama wewe ni mvivu kabisa nakushauri walau meza ile “Tanzania Guideline”, itakuheshimisha sana. 

 

Muonekano mzuri, vitendea kazi vizuri na elimu ya kutosha vitakupa heshima kubwa kama daktari kabla hata ya maujuzi mengine kama oparesheni. Kumbuka, first impression matters a lot! 

 

Mwisho

Heshima inajengwa na ni wajibu wako kuijenga kwa mikono yako ili kuweka mazingira mazuri kiutendaji. 

 

Una mahitaji yanayohusu vifaa vya kufanyia kazi kama daktari? Basi tembelea ofisi za JG Heritage enterprises zilizopo maeneo ya Muhimbili (nearby Simba Supermarket) pamoja na Makumbusho Royal Street kwa huduma nzuri za vifaa mbalimbali na ushauri wa namna ya kuvitumia. 

#!trpst#trp-gettext data-trpgettextoriginal=11#!trpen#Leave a Comment#!trpst#/trp-gettext#!trpen#

#!trpst#trp-gettext data-trpgettextoriginal=723#!trpen#Your email address will not be published.#!trpst#/trp-gettext#!trpen# #!trpst#trp-gettext data-trpgettextoriginal=715#!trpen#Required fields are marked *#!trpst#/trp-gettext#!trpen#

en_USEN