Faida Tano za Kutofanya Mapenzi kwa Muda Mrefu

Kufanya mapenzi ni sehemu ya maisha, na ina faida nyingi za kiafya na kijamii. Mojawapo ikiwa ni kupata watoto, lakini pia ni sehemu ya starehe ya wanyama.

 

Kufanya mapenzi huwa na msaada wa kisaikolojia, kuleta muunganiko wa upendo kati ya wapendanao. Mahusiano yasiyojumuisha kufanya mapenzi yaweza kuharibika haraka sana kwakuwa hayana msingi imara.

 

Kwa mwanaume, uwezo wa kufanya mapenzi vizuri – mara kwa mara – huweza kutafsiriwa kama uwezo mkubwa wa nguvu za kiume na humpa mwanaume sifa kubwa na heshima kwa wanawake.

 

Mwanaume ambaye hafanyi mapenzi mara nyingi huweza kutafsiriwa kama uwezo mdogo au matatizo ya nguvu za kiume na kadhalika.

 

Maneno ‘kufanya mapenzi’ yana maana gani?

Kufanya mapenzi kwa mwanaume huusisha utoaji shahawa pale anapofika kileleni. Utoaji huu unaweza kuwa kwa njia ya ngono (sex) au punyeto (masturbation).

 

Hizi shahawa ni seli za mwili zinazotengenezwa katika korodani za mwanaume; huwa na mchanganyiko wa vitu mbalimbali katika mwili.

 

Mshindo mmoja wa kilele unakadiriwa kupoteza kalori (nguvu ya mwili) kiasi cha kuanzia kalori 60 mpaka 100. Punyeto huweza kupoteza mpaka kalori 300 kwa mshindo mmoja.

 

Hivyo ukienda mishindo mitatu unaweza kuchoma mpaka kalori 180 hadi 300 kwa siku, ukifanya mara nne kwa wiki ni sawa na kuchoma kalori 500 mpaka 1200!

 

Sasa kutofanya mapenzi kwa muda mrefu kuna faida gani za kiafya?

1. Hukupa nguvu kubwa ya mwili

Kwanza shahawa huwa na vitamini aina ya B12 ambayo ina faida mwilini hasa kwenye kuongeza utendaji wa kazi za mwili. Huupa mwili uwezo mkubwa wa kubadili chakula unachokula kwenda kwenye nguvu (energy) ambayo mwili wako hutumia.

 

Pia husaidia mishipa ya fahamu kuwa imara na kupunguza uwezekano wa kuwa na damu chache.

Unapomwaga shahawa huwa unaipoteza hii vitamini, na ukifanya hivyo mara nyingi huwa unachangia mwili kukosa stamina na kuwa na nguvu kidogo. Maana yake, kutofanya mapenzi hufanya mwili uwe na nguvu zaidi.

Pili kutofanya mapenzi kwa muda husaidia mwili kutunza homoni ya testesterone – kiasi cha kutosha. Kutunza shahawa zako bila kuzitoa mara kwa mara huweza kuboost homoni yako kwa asilimia 45 kwa kipindi fulani, japo huwa inarudi katika kiwango cha kawaida baada ya muda fulani.

 

Homoni hii inapokuwa katika kiwango kikubwa huweza kuupa mwili wako nguvu, uwezo mkubwa wa kufanya mapenzi na nguvu kubwa ya kiume. Kupoteza homoni hii mara kwa mara hufanya mwili wako kuwa mchovu na kupunguza nguvu za kiume.

 

Ndio maana ukifanya mapenzi kwa mara ya kwanza ndani ya wiki unakuwa na uwezo mkubwa, lakini ukifanya kwa mara ya tano ndani ya wiki utagundua uwezo na nguvu zako za kiume zimepungua (pamoja na hamu ya kufanya Mapenzi).

Hii inasababishwa na kupoteza vitu hivyo viwili hapo juu.

 

Tip: Ulishawahi kujiuliza kwanini wanamichezo huzuiwa kufanya mapenzi walau siku 3 mpaka 4 kabla ya michezo? Sayansi yake ni kama nilivoeleza hapo juu.

 

Kwa kutofanya mapenzi walau siku tatu, nne au wiki huweza kuwapa nguvu na hamu ya kupambana, kwa maana ya kwamba ile hamu ya mapenzi huamia kwenye hamu ya kushindana na kushinda.

 

Stori ya ‘the baddest man on the planet’

Katika historia ya bondia, Mike Tyson alitumia njia hii kuwa bondia namba moja duniani. Tyson aliwahi kukaa miaka mitano bila kuwa na mwanamke, na kwa mara ya kwanza alipoanza mapambano ya ulingo, akiwa na miaka 20 tu alishinda pambana lake la Dunia.

 

Aliweza kufanya hivi kwa kushinda KOs (knockouts) 19 mfululizo huku knockouts 12 zikiwa katika round ya kwanza, na kuweka rekodi ya bondia mdogo zaidi kushinda taji la uzito wa juu la dunia. Ndipo akapewa jina la utani la “The baddest man on the planet”.

 

Moja ya sababu iliyochangia mafanikio yake ilikuwa ni nguvu kubwa aliyokuwa nayo. Kisayansi ilitokana na kutunza nguvu zake kwa kutofanya mapenzi na mwanamke au kupiga punyeto.

 

Wewe unaweza ukaitumia sayansi hii kwa faida. Ni dhahiri mwili wako ukiwa na nguvu ya kutosha unaweza kufanya mambo mengi ndani ya muda mfupi na kupata mafanikio.

 

Simaanishi usifanye mapenzi ila kama una shughuli ya kuandaa na inahitaji nguvu kubwa ya kufikiria na akili, basi unaweza kutofanya ngono kwa kipindi hicho; uwezekano wa kufanikisha unakuwa mkubwa kwa sababu ubongo na mwili wako unakuwa na nguvu ya kutosha.

 

2. Hukuongezea uwezo wa kujitawala (self-control)

Kupiga punyeto na kufanya mapenzi husababisha ubongo kutoa homoni za zawadi, homoni za mzuka, homoni zinazokufanya ujiskia raha. Hutengeneza hisia sawa kama mtu mwenye uteja. Hormones hizo (aina ya dopamine) ndizo zinazohusishwa na uteja mbali mbali kama madawa ya kulevya, pombe na kadhalika.

 

Bila shaka unajua raha unayoisikia wakati unamwaga shahawa unapofika kileleni. Ile hamu ya kupata ile hisia mara kwa mara hupunguza uwezo wako wa kufanya maamuzi, kujitawala, na kutokuwa na subira.

 

Sasa kwa kutofanya mapenzi mara kwa mara na kuziacha shahawa ndani ya mwili kwa muda mrefu hukupa uwezo wa kujitawala (self-control). Maana yake unapata uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kwa kuendesha hisia zako mwenyewe. Kujiamini pia kunaongezeka.

 

Utafiti unaonyesha mtu asiyeweza kudhibiti hamu na hisia za mapenzi hawezi pia kudhibiti mambo mengi muhimu kwenye maisha yake. Mfano kuogopa na kushindwa kufanya maamuzi magumu, pamoja na kutakua na msimamo kwenye mambo nyeti.

Mtu anaweza kuhonga gari au simu ya gharama kwa ajili ya raha ya siku moja tu!

Pia mwanaume mwenye tabia ya kupiga punyeto au kufanya mapenzi mara kwa mara huwa na uwezekano wa kujihusisha na tabia zingine hasi, mfano kucheza kamari, ulevi wa pombe, dawa za kulevya, na matumizi mabaya ya fedha.

 

Tabia zote hapo juu huusisha ‘homoni ya dopamine’ inayozalishwa kwenye ubongo ambayo hukupa mzuka wa muda mfupi, na ukiruhusu itolewe mara kwa mara (kupitia kumwaga shahawa) basi utajikuta unaingia kwenye tabia zingine zenye effect kama hiyo. Na hapo ndipo unapopoteza uwezo wako wa kujitawala.

 

Nitapata faida gani nikiweza kutawala hisia zangu?

Moja kati ya faida za kutawala hisia zako ni kuongeza uwezo wa kuwacontrol watu. Mwanaume asiyeweka mapenzi mbele huweza kuwacontrol wanawake na kuwa na msimamo thabiti, vile vile kwa mwanamke asiye na njaa za kimapenzi.

 

Ndio maana huwezi kumuamini mtu malaya, anaweza kukuuza kwa maamuzi mepesi ndani ya dakika 5 tu.

 

Wewe unaweza kuitumia njia hiyo ya kutofanya mapenzi mara kwa mara kujijenga self-control yako. Kama huwezi kukaa wiki bila kufanya mapenzi, utagundua huwezi kukaa wiki bila kutumia hela yako vibaya!

 

Muhimu: Kutofanya mapenzi hakupaswi kuwa kwa sababu hujapata mtu, unapaswa kuwa ni utashi wako.

 

3. Uwezo mkubwa wa kumbukumbu

Shahawa huwa na utajiri wa madini ya phosphorus na zinc ambayo huusika kukupa kumbukumbu imara na kufanya ubongo wako kuwa mwepesi na wenye afya. Kwa kutunza shahawa zako, unaweza kuwa na faida ya kuwa na uwezo mkubwa wa kumbukumbu na kufikiri.

 

Uwezo huu unaweza kukupa faida katika mambo mbalimbali hasa kwenye kujifunza na kazi. Ulishawahi kujiuliza kwanini wanafunzi wakiwa bado shule – za msingi na sekondari – huwa na uwezo mkubwa wa kukariri vitu vingi, kugundua mambo mapya, na kuwaza ndoto kubwa? Sababu inaweza kuwa ni hiyo.

 

Wakiashafika vyuoni tu na kuanza kufanya ngono, tafiti zinaonyesha uwezo wao huwa unashuka.

 

Wewe unaweza kuitumia hii kama advantage kwako. Jitahidi kutofanya mapenzi kama wiki, utagundua uwezo wako wa kumbukumbu utakavyoongezeka.

 

4. Huongeza nguvu za kiume

Utafiti unaonyesha watu ambao hawajihusishi na kupiga punyeto au kufanya mapenzi kila mara huwa na nguvu kubwa ya kiume. Uwezo wao wa kusimamisha uume huwa mkubwa pamoja na uwezo wa kufanya mapenzi muda mrefu kutokana na kutunza nguvu zao mwilini.

 

Watu kama hawa huweza kuwaridhisha wapenzi wao kwa kipindi kirefu. Kuna uwalakini katika mtu anayefanya mapenzi kila siku, inawezekana hawaridhishani inavyopaswa hivyo kutaka kurudiarudia mara kwa mara.

 

Wewe Unaweza kuitumia hii kama faida kwako, Mfano wapenzi wanaokaa mbali, siku saba kabla ya kumtembelea mwenzako, tunza shahawa zako. Ukikutana naye utagundua una nguvu ya kutosha kumridhisha.

 

Muhimu: Kuamua kufanya mapenzi mara chache huwa ni changamoto ukiwa na mwenza ndani. Lakini kwa kuzingatia faida yake, unaweza kumzoesha mwenza wako; kwa maana hata kama unafanya mara mbili, fanya kwa ubora ambao utamfanya aridhike siku zinazofuata, huku wewe ukipata nafasi ya kufocus kwenye mambo mengine ya msingi.

 

5. Huongeza uwezo wa kufanya maamuzi magumu (Risk taking)

Kuwa na kiasi kikubwa cha testosterone mwilini hufanya mwanaume kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi makubwa. Maamuzi magumu haimaanishi wizi, ugomvi au kuua, bali maamuzi ya kujenga vitu vikubwa na kutengeneza mandeleo endelevu.

 

Mfano wa watu maarufu waliokuwa wanatunza shahawa zao kwa muda (seen retention) ni Steve Jobs (muanzilishi wa kampuni ya Apple) na David Haye (mpigana masumbwi wa zamani wa uzito wa juu).

 

Steve Jobs alikua na uwezo mkubwa wa kutambua na kutumia fursa zinazokuja katika maisha yake ya kila siku. Pia akili na uwezo wa kufungua biashara na kufanikiwa, vitendo ambavyo uhitaji kujitoa sadaka za kifedha na raha za kila siku.

 

David Haye yeye aliwahi kufananisha mtu anayetunza shahawa kama simba ambaye hajala chochote kwa muda fulani, Hali hii humfanya huyo simba kuwa mnyama hatari mawindoni.

 

HAYE alikua hafanyi mapenzi au kupiga punyeto wiki sita kabla ya pambano lake. Muda wa pambano ukifika anakuwa na nguvu kama zote ambazo ziko tayari kumwagwa kwenye ulingo.

 

Mimi pia wakati nasoma Chuo Kikuu (St. Francis University), nilikuwa goalkeeper wa timu ya Chuo toka mwaka wa kwanza. Katika kipindi hiki niliweza kugundua jambo muhimu sana.

Siku ambazo nilikutana na mwanamke au kupiga punyeto usiku wa kuamkia mechi, siku ya mechi nilifungwa magoli rahisi sana. Ujasiri wangu wa kutokea mipira hatarini na kuruka kwenye miguu ya adui ulikuwa mdogo, hivyo nilijikuta nafungwa sana tofauti na siku ambazo nlikuwa sijakutana na mwanamke au kujichua kabla ya mechi.

Kuna namna fulani unakuwa na kauvivu na uwoga mwilini ukiwa umepoteza shahawa, hivyo maamuzi yako golini yanakuwa hafifu na mabovu.

 

Ndipo nlipoamua kutokufanya mapenzi walau siku tano kabla ya mechi na baada ya kumaster hilo jambo nilikuja kuwa kipa bora sana pale chuoni hadi mtaani.

 

Mtu anayependa ngono na kufanya mapenzi mara kwa mara hutengeneza mazingira ya kuogopa maisha na kujificha nyuma anapokuwa katika mazingira ya kufanya maamuzi makubwa. Hii huchangiwa na kumiliki testosterone chache.

 

Ndio maana kuna kamsemo mtaani huwa kanasema, “kufanya mapenzi sana ni ishara ya umaskini!” Kuna namna unakuwa na tabia za kike na uwoga wa kujitoa muhanga. Unawaza ukifa utamuacha Mwajuma, Salome, Getruda au yule demu wako wa kimara.

 

6. Huongeza mvuto

Nikuulize swali, ulishawahi kumuona mnyama aliyehasiwa? Jinsi anavyokuwa amenona?

Unapotunza shahawa zako bila kuzimwaga, mwili wako huwa na store kubwa ya testosterone. Homoni hizi kwanza hukupa kujiamini, hivyo watu huvutiwa na wewe.

 

Ubora wako wa kuwa na nguvu za kiume huongezeka na unapofanya mapenzi mwenza wako huvutiwa na wewe (kwasababu mwenza wako huwa anagundua nguvu hii hata bila wewe kujua).

 

Mwisho

Kumbuka mwili upo kufuata utashi wako, mwili hauwezi kufanya jambo ambalo akili na utashi havijataka. Mwili wako ni chombo tu, ila maisha yako yanaendeshwa na utashi wa akili yako.

 

Swala sio kutofanya mapenzi, ni kufanya mara chache na kuhamisha nguvu iliyobaki katika mawazo chanya kwa kutumia mbinu za kiafya ulizozipata hapa.

 

Hakuna utafiti ulioweza kuthibitisha kwamba kutofanya mapenzi muda mrefu kunasababisha tezi dume au kuleta magonjwa ya moyo, SIO KWELI.

 

Kuna rafiki alikwambia kutofanya mapenzi mara kwa mara huleta msongo wa mawazo na mwili kuwa mzito? Hii ni kama unawaza na kuhitaji mapenzi bila kupata. Kama ukiamua kuhamisha mawazo yako ya mapenzi kwenda kwenye mambo mengine ya maana, utagundua hakuna msongo wa mawazo utakaoupata.

 

Kijana mwenzangu (wa jinsia yoyote), jaribu kudhibiti hisia zako za mapenzi na utaweza kuitawala Dunia kwa kufikia malengo yako. Jambo pekee linaloweza kukufanya usifikie malengo yako ni kuwa na afya mbovu ya mwili na akili.

Ubongo na mwili uliochoka huishia kufanya maamuzi ya kichovu na kumiliki mawazo madogo. Nguvu ya shahawa huwa na nyongeza ya kukupa uwezo zaidi. Zitunze, usizipoteze bila sababu.

 

Mada ijayo tutaona namna ya kutunza shahawa pamoja na njia za kutumia kupunguza hisia za kufanya mapenzi mara kwa mara.

 

Usisahau kutuandikia maoni yako na Barua pepe kwa ajili ya kupata taarifa zetu mpya kwenye inbox yako.

#!trpst#trp-gettext data-trpgettextoriginal=733#!trpen#14 thoughts on “<trp-post-container data-trp-post-id='708'>Faida Tano za Kutofanya Mapenzi kwa Muda Mrefu</trp-post-container>”#!trpst#/trp-gettext#!trpen#

  1. Whaat i do not understood is in reality how you are now not
    really much more well-appreciated than yoou may be now. You’re very intelligent.
    You understand therefore significantly in relation to this topic, produced me in myy view consider it from a lot of various angles.
    Its like men and wojen aren’t fascinated except it is something to do with Girl gaga!

    Your own stuffs outstanding. At all times take care oof iit up! https://Zeleniymis.Com.ua/

  2. Hakika mbarikiwe sana kwani mmenikimboa kiakili na kimwili nataka kuwa MD ndoto yangu Mungu awabariki nyote
    Pia njia zingine mojawapo ni kama vile
    1,zungumza,mithalu17;7,by Yolanda(hisia hadi au changa)
    2, Andika,
    Ayubu 10:10
    By illiana , umuhimu wake
    3,Sali
    Zaburi 55:22,
    By Jasmin na wengine wengi ,eg baddest man on the planet,seen retention ansebeta……

    MUNGU awe pamoja nanyi nyote 🙏
    samorambelele@gmail.com

#!trpst#trp-gettext data-trpgettextoriginal=11#!trpen#Leave a Comment#!trpst#/trp-gettext#!trpen#

#!trpst#trp-gettext data-trpgettextoriginal=723#!trpen#Your email address will not be published.#!trpst#/trp-gettext#!trpen# #!trpst#trp-gettext data-trpgettextoriginal=715#!trpen#Required fields are marked *#!trpst#/trp-gettext#!trpen#

en_USEN