Ukipata bawasili kwa mara ya kwanza unaweza kudhani ni kansa au ni utumbo unatoka nje. Hali hii hufanya mtu kuwaza mengi sana.
Wengi huja hospitali kuripoti kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa. Lakini ni asilimia 30 tu ya watu wenye bawasili ndio huja hospitali kuripoti hali hii.
Asilimia 10 huwa hawaji kabisa kwa kuogopa au aibu hivyo hujikuta na tatizo hili kwa muda mrefu sana.
Bawasili ni nini?
Ni hali ya kutokwa na kinyama katika njia ya haja kubwa. Kinyama hiki hutoka na kuingia ndani nyakati fulani au inaweza kubaki nje moja kwa moja ikiwa katika zile hatua kubwa.
Hali hii huwa sio kinyama kama ambavyo wengi hudhani bali ni mishipa ya damu ya haja kubwa ambayo inakuwa imejaa damu kutokana na presha kubwa katika mishipa ya damu ya tumbo. Kwa kuwa mishipa hii imefunikwa na ngozi laini ya haja kubwa, basi huonekana kama kinyama.
Dalili za Bawasili
- Uwepo wa kinyama sehemu ya haja kubwa ambacho kinaweza kuwa ndani au kuwa kinatoka nje.
- Yaweza kuja na maumivu au bila maumivu.
- Kutokwa damu hasa unapoenda kujisaidia.
- Hutoka mara nyingi ukiwa unasukuma chooni, unakohoa, unatembea au kusimama muda mrefu.
Nini Hasa Hupelekea Bawasili Kutokea?
Presha kubwa katika tumbo ndiyo hupelekea bawasili kutokea. Presha hii hufanya mgandamizo wadamu kuwa mkubwa na hivyo mishipa ya damu (veins) ya sehemu za utumbo mkubwa na puru kushindwa kusukuma damu kwenda juu.
Hii husababisha mishipa ya damu kupanuka au damu kuganda na kusababisha bawasili.
Presha hii inaletwa na mambo mengi ila mimi nimekuandikia baadhi tu hapa. Soma mpaka mwisho ili uelewe vizuri.
1. Ugumu wa kupata choo (constipation)
Bila shaka ulishawahi kuwa na ugumu wa kupata choo mara kadhaa. Nini huwa kinatokea ukiwa pale chooni?
Bila shaka unatumia nguvu kusukuma na hasa choo ikitoka na ikakwama pale katikati, nguvu unayotumia kusukuma huwa ni chanzo cha kuongeza presha kubwa tumboni.
Hali hii ikiendelea muda mrefu basi utaanza kuona bawasili ikianza kuchomoza kidogokidogo.
Ugumu wa choo huweza kusababishwa na mambo mengi kuanzia mlo mbovu mpaka magonjwa. Kinachotakiwa ni kutatua tatizo ulilonalo na kuondoa hatari ya bawasili.
Njia za kawaida kama kula vyakula vyenye nyuzi kama maembe, tikitimaji, kabeji, mlenda, ndizi bukoba na kadhalika.
Pia kunywa maji ya kutosha walau lita 3 kwa siku. Punguza kula wanga kila siku, jaribu kuchanganya na vyakula vingine vilaini kama ndizi.
Magonjwa mengine mfano stroke, cancer na shida ya utumbo ni changamoto lakini dawa za kulainisha choo na mazoezi vitasaidia kupunguza changamoto husika.
2. Mazoezi magumu bila mapumziko
Mazoezi ni muhimu sana hasa ya tumbo lakini yakizidi huweza kuongeza presha tumboni na kuleta bawasili.
Mazoezi yafanyike lakini kuwe na kipindi cha kupumzika, mfano mazoezi siku nne na siku mbili za mapumziko ili kutoa nafasi kwa viungo kukaa vizuri. Mazoezi makali ya kila siku yanaweza kuwa chanzo cha bawasili.
Baadhi ya mazoezi yanayoweza kuleta bawasili ni kubeba vyuma, kukimbia, kupiga pushups nyingi, na mpira.
Pale unapohisi kuna kitu kinatoka sehemu ya haja kubwa, jaribu kupata walau siku mbili za kupumzika na kuendelea baada ya hapo.
3. Kukaa na kusimama muda mrefu
Kukaa muda mwingi bila kutembea huweka presha kubwa tumboni na kupelekea bawasili. Pia kusimama muda mrefu mara kwa mara inaweza kuwa chanzo cha bawasili kwani hii pia huongeza presha kubwa tumboni hasa kwa watu wazima kuanzia miaka 45.
Kinachotakiwa hapa ni kuhakikisha unafanya mwendo (movement) kadhaa walau kila baada ya masaa mawili.
Kama unakaa sana ofisini, hakikisha kila baada ya dakika 90 unasimama na kushuka ngazi kidogo, kujinyoosha na kurudi kwa kiti. Hii itakusaidia sana kupunguza adha hii.
Kama kila unapokaa unahisi presha kubwa sana makalioni unaweza kutumia mto maalum wa kukalia ujulikanao kama coccyx pillow. Unaweza kutupigia simu ili tukuelekeze jinsi mto huu unavyoweza kukusaidia.
4. Ujauzito
Ndio! Unashangaaa nini? Mwanamke mjamzito ana asilimia 60% ya kupata bawasili. Hii ni kutokana na ujauzito kuongeza presha ya tumbo na kupelekea ugumu wa damu kurudi vizuri na hivyo hupata bawasili.
Hutokea zaidi kwa wajawazito wenye miili na uzito mkubwa; na wale wajawazito wenye uvivu wa kutembea.
Ukiwa mjamzito jaribu kuwa unafanya mazoezi, mfano, ya kutembea na kukalia mpira maalum wa kupunguza presha na mgandamizo mahala pa haja kubwa.
Gym ball na ujauzito
Kutokana na hatari hii ya bawasili, kukalia gym ball kipindi cha ujauzito imeonekana kuwa na msaada mkubwa sana. Mjamzito anapokalia mpira huu humsaidia kumsukuma mtoto juu kidogo na kupunguza presha katika mishipa ya damu.
Kufanya hivi mara kwa mara huondoa hatari ya bawasili na pia kuleta maendeleo mazuri wakati wa safari ya ujauzito.
5. Shida ya kupata mkojo
Watu wenye shida ya kupata mkojo pia wana hatari ya kupata bawasili kwasababau ya kutumia nguvu kusukuma mkojo na hii huongeza presha kubwa tumboni; kwahiyo ikiwa mara kwa mara huleta bawaili.
Kama unahisi hali ya mkojo kutoka kwa shida hasa kuanzia miaka 45 na kuendelea, basi unaweza kuwa na tezi dume na unapaswa kutibiwa mapema ili kupunguza changamoto za kupata bawasili.
Muhimu
Kikohozi cha muda mrefu kisichopona nacho ni chanzo cha kupata bawasili. Hakikisha unafanyiwa checkup na kupata matibabau ya kikohozi.
Nikipata bawasili nifanyeje?
Ni asilimia 10% tu ya wagonjwa wa bawasili huitaji upasuaji. Kwa walio wengi bawasili huondoka pale visababishi vinapoondolewa.
Bila kuondoa visababishi hata ukifanyiwa operation bado inaweza kurudi tu.
Siri ni nini? Fanya matibabu ya bawasili lakini hakikisha unaondoa chanzo chake na sio kutibu dalili. Daktari wako atakuongoza katika kujua chanzo.
Angalia kisababishi chako hapo ni kipi na jaribu kupambana nacho kwa mbinu tulizosema hapo juu.
Tuna habari njema kwako
Una bawasili kubwa na unasubiri operation au umefanyiwa operation tayari? Basi unahitaji mto maalum wa kukalia ujulikanao kama Round ring pillow.
Mto huu ni muhimu sana kwako, una tundu katikati ambalo hukupa nafasi ya kukaa bila kuumia na kutoa nafasi sehemu ya upasuaji na kidonda kupona haraka. Pia kama unasafiri umbali mrefu itakusaidia kukaa bila maumivu.
Mito hii inapatikana Abite Nyumbani, wasiliana nasi kwa maelezo zaidi kupitia hii namba: +255 767 226 702.

Chief Content Officer (CCO) at Abite Afya
I’m responsible for overseeing the entire content strategy, ensuring that all published materials align with the blog’s mission, audience needs, and business goals.