Vyakula Vinavyosaidia Ngozi Yako Kutozeeka

“Kadri miaka inavyoenda, ndivyo binadamu tunazidi kukua.”

 

Katika hali ya ukuaji kuna  mabadiliko mbalimbali ya kimwili hutokea na hivyo basi tunatakiwa kuzingatia ulaji bora ili tuwe na afya imara itakayotusaidia kuzuia hali za kupungukiwa nguvu kwa haraka sana.

 

 

Hii ni kwa sababu katika vipindi vya uzee kuna mabadiliko mbalimbali ya kimwili hutokea kama vile upungufu wa kinga mwilini, seli za mwili kufa, kuzeeka na pia kutokutengenezwa kwa seli mpya za mwili (kwa wingi kama katika vipindi vya utoto na ujana) na uchovu huu huanza kuonekana katika ngozi ya binadamu.

 

Mambo muhimu ya kufanya ili kusaidia ngozi yako kutokuchoka mapema

1. Kufanya mazoezi na kuepuka tabia bwete

Unaweza kufanya mazoezi yako kwa angalau nusu saa mpaka lisaa limoja kwa siku. Mazoezi haya yanaweza kujumuisha kutembea, kukimbia, push-ups, pull-ups, na kadhalika. 

 

2. Epuka kula vyakula vyenye calorie nyingi na anza kutumia vyakula vyenye vitamini na madini

Vyakula hivi ni vile vyenye wanga mwingi kama vile; ugali , wali, pizza, burger, chips na vyakula vyenye sukari nyingi kama vile soda pamoja na juisi zinazoongezewa sukari.

 

Ili uweze kufahamu namna ya kupunguza ulaji wa vyakula vyenye calorie nyingi ambavyo vingi huwa ni vyenye kirutubishi cha wanga (mfano viazi, ndizi, mahindi, n.k.), vyakula vyenye kirutubishi cha protini (samaki, nyama, mayai na kadhalika) pamoja na vyakula vyenye kirutubishi cha mafuta (kama vile mafuta yenyewe na mafuta yanayopatikana katika nyama na mimea/mbegu mbalimbali).

 

Unatakiwa kufanya mawasiliano na mtaalamu wako wa maswala ya lishe ili akae mezani na kukusaidia katika mpangilio wa mlo pamoja na kufanya mahesabu ya calorie zinazotakiwa katika mwili wako kutokana na umri, kazi unazofanya, jinsia, pamoja na uzito na urefu kwani vyote hivi vinachangia katika mahesabu hayo.

 

Mfano mcheza mpira ana mahitaji tofauti na mtu ambaye kazi zake za kila siku zinahusisha kukaa kwa vipindi virefu.

 

Vyakula/virutubishi vitakavyosaidia ngozi yako kutokuchoka mapema

1. MAJI

Maji husaidia katika kuleta hali ya uwiano kati ya ngozi na tissue. Hii ina maana gani?

Nitakujibu kwa mfano huu: Ngozi isiyokua na maji huwa na hali ya kukunjamana na katika mojawapo ya dalili za dehydration ni kukunjamana kwa ngozi.

 

Nadhani utakua unaukumbuka ule msemo wa “maji ni uhai“, basi maji huchangia kikubwa katika kuleta nuru ya ngozi yako.

 

2. Vyakula Vyenye Kirutubishi Cha PROTINI

Vyakula vya protini ni matofali ya kujengea mwili wako, nikimaanisha kwamba seli zote za mwili wako hutegemea protini. Hii unaipata kwenye samaki, kuku, mayai, maziwa na kadhalika.

 

Nikukumbushe tu kwamba hapo juu nilizungumzia kwamba protini ni chakula chenye calorie hivyo basi kinapaswa kuliwa kwa kiasi (0.8g/kg).

 

Ni muhimu kufahamu ule kiasi gani kwa kuwasiliana na mtaalamu wako wa maswala ya lishe aliyefuzu masomo hayo ya stashahada ili aweze kukupangia mlo wako.

 

Ukihitaji huduma hii, unaweza kunipigia kwenye simu namba +255 756 454 391.

 

3. Vyakula Vyenye VITAMIN D

Vyakula hivi husaidia katika kupunguza athari zinazotokea katika ngozi pale inapoumizwa na vitu mbalimbali kama vile jua, kuungua na  kadhalika.

 

Chanzo cha kwanza cha vitamini D ni kukaa katika jua kwa kiasi kidogo. Tafiti na machapisho mbalimbali yanasema kuanzia dakika 5 mpaka 15 za jua la kuanzia saa tano asubuhi mpaka saa 9 alasiri.

 

Pia ulaji wa vyakula kama vile samaki, mayai na maziwa vinasaidia kuongeza vitamini D mwilini.

 

4. Vyakuka Vyenye VITAMINI A Pamoja na VITAMINI C

Katika harakati za urembo kunakua na bidhaa mbalimbali katika soko la vipodozi ambazo nyingi hujaribu kutafuta namna za kutengeneza bidhaa zenye vitamini kama vile vitamin C au vitamin A – kwa ajili ya kupaka katika ngozi.

 

Bidhaa hizi huuzwa masoko ya vipodozi kwa bei za juu sana lakini inawezekana kupata virutubishi hivi kupitia vyakula na kuvitumia ili uweze kuimarisha afya ya ngozi yako.

 

 

Vyakula vyenye vitamin A na C ni kama vile mbogamboga za majani, machungwa, mananasi, maembe, mapapai, nyanya na vyakula vingine vingi.

 

5. VITAMIN E

Hii vitamini imekua ikitengenezwa katika mfumo wa vidonge pia na kuuzwa katika maduka ya dawa kwa sababu ya faida zake katika ngozi.

 

Kwa upande wa vyakula ambavyo vina vitamini E ni: Almonds (kwa kiswahili hujulikana kama Lozi), karanga, hoho zenye wekundu na parachichi.

 

Vyakula/vitu vya kuepukana navyo vinavyoharibu ngozi yako

1. Tumbaku

Utumiaji wa tumbaku huleta uwepesi katika ngozi; ngozi inaharibika katika ujazo na kuwa nyembamba na nyepesi.

 

Pia husababisha mabadiliko ya rangi kwa kusababisha weusi usio wa kawaida, lakini pia tumbaku hufifisha ngozi (hupunguza mng’ao wa ngozi).

 

2. Pombe

Unywaji wa pombe huleta madhara mengi mwilini kwa sababu haipo katika makundi ya virutubishi, mwalimu wangu wa astashahada ya utabibu aliwahi kutuambia pombe ni sumu.

 

Hivyo basi ni vyema kuepuka matumizi ya pombe kwani husababisha changamoto katika sehemu mbalimbali za mwili na mojawapo ni ngozi ambapo inaharibu mfumo wa uchujaji ambao upo katika ngozi na kupelekea uwekwaji wa mafuta mengi ambayo huleta athari kwa mtumiaji baada ya kipindi flani.

Leave a Comment

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

swSW