Wimbi la magonjwa mbalimbali, yasioambukiza na yanayoambukiza, linaendelea kuenea katika sehemu mbalimbali, hasa za mijini, na hali hii inapelekea watu kujiuliza wawe wanakula nini ili kuimarisha kinga ya mwili na kujiepusha kupata magonjwa haya.
Mfano wa magonjwa yasioambukiza ni kisukari, presha, kansa na magonywa ya moyo. Kifua kikuu (TB), Ukimwi, Corona, dengi, surua, homa ya ini ni baadhi ya magonjwa yanayoweza kuambukizwa kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa mtu asiyeumwa.
Wataalamu mbalimbali wa afya pamoja na wadau wa maswala ya kiafya wamekua wakiongelea mambo mbalimbali yanayopaswa kufanyika ili kupunguza mlipuko wa magonjwa haya kama vile kuzingatia swala na usafi (kwa magonjwa ya kuambukiza) na lishe bora (kwa magonjwa yasioambukiza).
Hivyo basi leo katika makala yanga nitaelezea na kupendekeza vyakula mbalimbali ambavyo vinapatikana katika mazingira yetu na vinaweza kukusaidia kuimarisha kinga ya mwili wako. Vyakula hivi ni kama ifuatavyo:
1. Matunda yenye vitamini C ambavyo viko jamii ya Citrus
Mifano ya matunda haya ni machungwa, malimao, ndimu, zabibu, tunda aina ya kiwi pamoja na strawberries.
Kazi ya vyakula hivi ni kusaidia katika mchakato wa kutengeneza seli hai nyeupe za kinga ambazo hutumika katika vipindi vya mapambano dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa kiasi cha vitamin C kinachofyonzwa na mwili ni miligramu 400 tu , na mtu mzima anaweza kutumia mpaka kiasi cha miligramu 1,000 kwa siku na hapaswi kuzidisha miligramu 2000 kwa siku.
Hivyo basi ukitumia miligramu 500 kwa siku itakua imetosha kabisa katika matumizi ya mwili ya siku.
Tip: Ili ufikishe kiasi cha miligramu 500 za vitamin C unaweza kula machungwa matano, malimao matatu na apples mbili .
2. Kula vyakula vyenye “probiotics”
Tuanze na probiotics ni nini? Probiotics ni vijidudu hai ambavyo vinakusudiwa kuwa na faida za kiafya vinapotumiwa na binadamu .
Vyakula hivi vya probiotics mara nyingi ni vile ambavyo vimechachushwa kama vile maziwa mtindi pamoja na kombucha. Ili ujue kama vyakula vina probiotics, mara nyingi hasa unavyokuta supermarket, unakuta vina maelezo kwamba vinakua na probiotics ndani yake hasa kwenye maziwa mtindi.
Kufahamu zaidi kuhusu vyakula vyenye probiotics, pitia makala hii.
3. Kula mboga za majani aina ya spinach
Mboga mboga hizi huwa na vurutubishi vingi ikiwemo kirutubishi aina ya folate ambacho kinafanya kazi ya kutengeneza seli mpya za mwili.
Muhimu: Fahamu kwamba miili yetu imejengwa na kitu kinachoitwa seli ambazo huwa na tabia ya kufa na kuzaliana kwa upya kwa hiyo kazi ya folate ni kuzalisha seli mpya lakini pia inafanya kazi ya kufanya matengenezo katika seli za vinasaba yaani DNA.
4. Orange peel sweet potatoes
Hivi ni vile viazi vyenye rangi ya orange ambavo vinakua na carotene ambayo ikiingia katika mwili hubadilika na kuwa vitamin A ambayo ni nzuri katika kupambana na magonjwa mbalimbali.
Mifano ya vyakula vingine vyenye carotene ambavyo vitakusaidia kuimarisha kinga ya mwili ni karoti, lettuce, nyanya, na spinachi – ambayo tumetoka kuiongelea hapo juu kwamba ina folate pamoja na brocolli.
Vyakula hivi vinapatikana katika masoko yetu hasa kipindi hichi ambacho kilimo cha mbogamboga kimeenea nchini.
5. Chai ya masala
Chai ya masala ni mojawapo ya kinywaji ambacho kinasaidia kupambana na molecules zinazoweza kusababisha cancer ambavyo ni free radicals.
Hii ni kwa sababu chai hii ina kitu kinachoitwa antioxidant ambazo hufanya kazi ya kukamata free radicals hizi na kuzuia madhara yanayotokana nazo kama vile saratani.
6. Vyakula vyenye magnesium kama vile dark chocolate ambayo inasaidia seli za kinga kukamata vimelea vya vijidudu vinavyosababisha magonjwa ndani ya mwili katika kipindi cha mapambano ya magonjwa.
7. Selenium ambacho ni kirutubishi kinachopatikana katika samaki pia huwa na kazi ya kusaidia ufanyaji kazi wa mfumo mzima wa kinga mwilini.
Hivyo basi ili mfumo wako wa kinga mwilini ufanye kazi vizuri inabidi uwe unakula vyakula vyenye selenium kama vile kuku, samaki na nyama pamoja na maharage.
Hivyo ni baadhi ya vitu vinavyoweza kuliwa ili kuongeza uimara wa hali ya kinga mwilini, hasa katika vipindi hivi ambavyo kuna mlipuko wa magonjwa mbalimbali. Asante sana kwa kusoma makala hii, tukutane tena katika makala ijayo ya maswala ya lishe.

Providing nutrition education and counselling in Tanzanian local communities, currently in Mkuranga – Pwani region. My goal is to raise awareness on how to improve our health through nutrition – in all human life stages.