Vifaa Tiba 10 vya Kuwa Navyo Nyumbani Kwako

Katika kutibu ugonjwa kuna njia nyingi, mojawapo (ambayo ni kubwa) ni matumizi ya dawa. Asilimia 90% ya wagonjwa wanapoumwa macho hukimbilia kwenye dawa wakiamini kwamba dawa pekeee ndiyo inaweza au inatakiwa kutibu au kufanya ugonjwa kuwa nafuu. 

 

Bahati mbaya matumizi ya dawa za maumivu kwa muda mrefu zimechangia kupata madhara mengine kama vidonda vya tumbo, kuvimba miguu, matatizo ya Ini, Moyo na Figo.  

 

Baada ya kufanya utafiti mbalimbali katika idara ya magonjwa nikagundua wagonjwa wengi wako majumbani na wanateseka sana kwa sababu ya jambo moja kubwa: Hawajui na hawatumii vifaa tiba kama njia mbadala ya kupunguza mateso ya magonjwa yao.  

 

Na hata kama wanavijua basi huwa wanadhani vinapatikana kanisani au kwa msaada maalaum. Kwa ujumla hawajui wavipate wapi.  

 

Vifaa tiba ni muhimu sana katika kuharakisha uponaji au kuleta nafuu kwa mgonjwa wa muda mrefu au kwa wale wenye matatizo yanayohitaji msaada wa watu kila siku. 

 

Stori ya Mgonjwa na Goti Lake

Mwaka 2023 nilikutana na Mzee mmoja aliyekuwa na matatizo ya goti la kulia pamoja na mgongo. Maumivu ya goti ndiyo yalitangulia na baada ya mwaka akaanza kuumwa mgongo.  Baada ya kumchunguza zaidi niligundua tatizo lilipoanzia.

 

Baada ya kuanza kuumwa goti alikuwa akitembea huku amepinda upande mmoja wa kulia, na kutokana na kutembea amepinda upande mmoja basi uti wa mgongo wake ukapinda kulia (kyphoscoliosis) na hivyo akaanza kupata maumivu makali ya mgongo.  

Alikosa huduma muhimu mwanzoni: Fimbo kwa ajili ya kuweza kutembea akiwa amenyooka.  

 

Hivi unajua kwamba inawezekana unateseka na maumivu au kushindwa kufanya shughuli zako za mara kwa mara kwa sababu huna kifaa tiba kinachotakiwa? Vifuatavyo ni vifaa tiba mbalimbali pamoja na matumizi yake: 

 

1. Walker

Kifaa hiki kinamsaidia mgonjwa ambaye ugonjwa wake unamfanya asiwe na balance ya kutembea mwemyewe lakini pia kama amechoka kukaa chini kusubiri mpaka kubebwa.

 

Walkers at Abite Nyumbani

 

Ukiwa na walker itakuwezesha kutembea ndani ya nyumba yako, kusogea chooni, kutembea toka chumbani mpaka sebuleni, na kadhalika.

 

Watu gani wanaweza kusaidiwa na “walker”? 

Wagonjwa wa moyo, wanaofanya mazoezi madogo baada ya ajali au upasuaji (rehabilitation), wazee wasio na nguvu, pamoja na wagonjwa walio na kiharusi wenye nguvu kidogo za kutembea hapa na pale.  

 

 2. Fimbo Tiba (Canes)

Una maumivu ya mguu, goti au kiuno na unahitaji support ya kutembea bila kupinda au kuanguka? Basi Fimbo tiba inakuhusu.

 

Canes at Abite Nyumbani

 

Bila fimbo tiba kwa wazee na watu wenye maumivu, kuanguka na kuvunjika ni rahisi sana. Fimbo zina miguu tofauti kulingana na mahitaji. Ni vizuri kupata ushauri kwanza kabla ya kununua.  

 

 3. Wheelchair (Kiti Chenye Matairi)

Kwa mgonjwa asiyeweza kwenda nje kutokana na magonjwa kama kiharusi, kisukari, ajali au operation, wheel chair ni muhimu ili kuweza kutembezwa nje, kupata upepo mzuri, kuwa na uhuru wa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

 

Epuka kumfungia mgonjwa ndani na kuzuia asipate nafasi ya kutoka nje. Ni vyema kuwanunulia wheel chair.

 

Wewe ungeambiwa ukae ndani bila kutoka nje mwaka mzima ungeweza?  

 

4. Kiti Chenye Choo

Umewahi kuona kiti chenye choo? Basi fahamu nacho ni kifaa tiba na huwasaidia wale wagonjwa ambao hawana kabisa nguvu za kutembea kwenda chooni. Kama gharama za kumjengea mgonjwa wako choo cha kukaa ni kubwa, basi nakushauri umnunulie kiti chenye choo.

 

Commode Chair at Abite Nyumbani

 

Hapa mgonjwa ataweza kujisaidia hata kama hana wasaidizi wengi na huondoa adha ya kuhitaji kumbeba mgonjwa kwenda chooni kila mara hasa watu wakiwa makazini.  

 

 5. Kiti Tiba Cha Mgongo (Curble Chair)

Kazi zako zinakufanya ukalie kiti kwa muda mrefu, lakini cha kushangaza ukikaa masaa mawili tu mgongo wote unauma na unalazimika kuacha kazi ili usimame?

 

Basi hiki kiti ni kwa ajili yako. Kitakusaidia ufanye kazi katika position inayotakiwa, mgongo ukiwa umenyooka na kuondoa kabisa maumivu yoyote ya mgongo. 

 

Zaidi kwa wale wamama wenye maumivu ya mgongo baada ya operation ya mtoto, kiti hiki kinawahusu sana; husaidia kukinga maumivu ya mgongo kwa badaye.  

 

 6. Mkanda wa Mgongo (Lumber belt)

Huu ni mkanda kwa ajili ya wale wenye maumivu endelevu ya mgongo. Maumivu haya husababishwa na kulika pingili, uzee, magonjwa, ajali au operation.

 

Faida ya mkanda huu ni kukupa ahueni ya maumivu wakati unaendelea na matibabu mengine ya dawa. Kutokana na faida hizi, mkanda wa mgongo husaidia sana kukupunguzia kiasi cha dawa ambazo ungemeza kila mara. 

 

 7. Godoro la Hewa (Air Mattress au Decubitus Mattress)

Hivi unajua kwamba wagonjwa waliolala muda mrefu kitandani bila kugeuzwa huishia kupata vidonda vya muda mrefu? Vidonda hivi husababishwa na mgandamizo (Pressure) wa muda mrefu kwenye mwili hasa mahala penye joint.

 

Medical Air Mattress at Abite Nyumbani

 

Kwa kawaida mgonjwa mahututi au ambaye hajiwezi hutakiwa kugeuzwa huku na kule kila baada ya masaa mawili (2). Kwa bahati mbaya, kutokana na ndugu kuwa busy kikazi inakuwa ngumu kukidhi kiwango hicho na hivyo kumpelekea mgonjwa kupata vidonda.  

 

Vidonda kama hivi ni kiashiria kibaya na hupoteza matumaini ya mgonjwa kurudi katika ubora wake kiafya. Mgonjwa akianza kulalia Godoro hili la hewa basi huondoka kwenye hatari ya vidonda na hivyo hata akipona huweza kurudi haraka katika ubora wake.  

 

Kumuacha mgonjwa wako akapata vidonda ni uzembe mkubwa utakaoujutia kila siku. Air mattress ndiyo suluhisho.  

 

8. Mpira wa Mazoezi (Gym Balls)

Kama wewe ni kijana wa kike au wa kiume na unataka kuwa na uwezo wa kufanya mazoezi mbalimbali nyumbani bila ya bugdha, basi milikimpira wako wa mazoezi. Unachotakiwa kujua ni mazoezi gani ufanye, basi!

 

 

Nilipokuwa mdogo nilidhani mipira hii ni kwa ajili ya wasanii tu lakini baadaye nilipopata fursa ya kuutumia ndipo nikagundua nilikuwa nakosa faida nyingi sana za mpira huu.

 

Mpira huu unaweza kufanyiwa mazoezi ya misuli ya tumbo, mgongo,kiuno, matako, mbavu, shingo, miguu, vigimbi, na kadhalika.

 

Wewe ni Mama mjamzito na unahitaji mazoezi ya mimba? Basi kuwa na mpira huu. Wewe ni binti na unahitaji kutanua matako yako? Basi mpira mazoezi utakufaa sana. 

 

 9. Kifaa cha kujifanyia massage (Transcutaneous Electrical Nerve Stimulator – TENS)

Kuna wakati unasumbuliwa na maumivu sugu ya mgongo, misuli, mabega na joint mbalimbali mbalimbali; dawa peke yake zinaweza zisitoshe ndio maana huduma ya massage ni nyongeza muhimu sana hasa kama una maumivu sugu.

 

Lakini shida ni moja, huna ujasiri wala muda wa kwenda kufanya massage japo unatamani sana. Basi kifaa hiki ni kwa ajili yako.

 

Wireless TENS at Abite Nyumbani

 

Kinatoa huduma ya mazoezi tiba (physiotherapy) na hapa unajifanyia mwemyewe. Ukiwa na kifaa hiki utajisikia sawa na mtu anayefanyiwa massage.

 

Unatakiwa tu kuweka sehemu yenye maumivu na kusikilizia kazi yake ya maajabu. Umuhimu wa kifaa hiki ni kutuliza maumivu kwa muda wa walau masaa 8 mpaka 24 hivyo hufanya mtu kutumia dawa chache za maumivu. Kama unahitaji huduma hii, basi unahitaji kifaa hiki nyumbani kwako. 

 

 10. Coccyx Pillow

Una maumivu makali ya mgongo wa chini kabisa juu ya makalio? Bila shaka una matatizo kwenye sehemu ya mwisho ya mfupa wa uti wa mgongo (coccyx).

 

Maumivu haya husababishwa na ajali, kusagika kwa sehemu ya mfupa, operation, kukaa kwenye kiti cha mbao kwa muda mrefu na matatizo mengine ya umri.

 

Coccyx Pillow at Abite Nyumbani

 

Kutokana na maumivu haya unaweza kushindwa kufanya kazi yako kwa muda mrefu na kulazimika kulala ubavu au kushindwa kabisa kuendelea na kazi. Coccyx Pillow ni mto tiba unaosaidia kupunguza maumivu haya kwa kiasi kikubwa. Hupunguza presha katika sehemu ya chini ya mgongo. 

 

Uzuri ni kwamba unaweza kutembea nao sehemu yoyote. Unaweza kuutumia kwenye gari, ofisini kwako au nyumbani kwa kuuweka juu ya kiti chako unachokalia.  

 

Wewe ni mjamzito? Basi mto huu unakuhusu kwa ajili ya kukukinga na maumivu ya mgongo.  

 

Unafanya kazi zinazohitaji kukaa muda mrefu? Kwa mto huu, umepata suluhisho!  

 

 11. Heating Pad

Hiki ni kifaa ambacho hutumia joto kupunguza maumivu ya mwili hasa joint. Zaidi, kama una matatizo ya hedhi yenye maumivu makali ya tumbo, basi heating pad inakuhusu.

 

Heating pad at Abite Nyumbani

 

Uzuri wake ni kwamba unaweza kutembea nayo kokote, kwenye mkoba au begi. Zipo za umeme na za kawaida, na hutunza joto kwa zaidi ya masaa nane.  

 

 

Ni kifaa gani unaona kitakufaa au kumfaa mtu unayemfahamu? Abite Nyumbani tunatoa huduma ya vifaa tiba vya aina mbalimbali vitakavyokusaidia kuleta auheni katika changamoto yako ya kiafya.  

 

Kwa msaada zaidi, wasiliana nasi kupitia 0767 226 702 au tembelea dula letu linalopatikana Sinza Mori, jengo la Azaria Plaza (Ofisi Na. 14), opposite kabisa na Kitambaa Cheupe Lounge. 

 

Usisahau pia kutembelea kurasa yetu ya Instagram kwa taarifa kamili ya vifaa tiba vyote vinavyopatikana Abite Nyumbani.

Leave a Comment

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

swSW