Uwezo na Faida za Kitunguu Saumu Mwilini 

Kitunguu saumu, garlic, ni mmea ambao umekua ukizungumziwa kuwa na faida mbalimbali mwilini; baadhi ya faida hizo ni kusaidia kushuka kwa shinikizo la juu la damu (high blood pressure), kusaidia afya ya mfumo wa moyo na mishipa ya damu, na mengine ambayo tutayaona hapo chini. 

 

Leo tutakiangalia kitunguu saumu katika mwanga wa kama kweli kinaweza kushusha shinikizo la juu la damu na kinatakiwa kutumiwa kwa kiasi gani hasa. 

 

 

Mimi ni mmojawapo wa watumiaji wazuri wa vitunguu saumu kwa sababu ya kuipenda ladha inayoletwa na kitunguu saumu katika chakula lakini pia kwa sababu kinakua na faida nyingi katika mwili wangu. 

 

Kwa kuanza tuiangalie historia ya kitunguu saumu. Je! Kitunguu saumu kilianzia wapi? 

 

Waandishi mbalimbali wamehusisha uanzilishi wa kiungo cha kitunguu saumu kutokea nchi ya China, na inasemekana ni kuanzia miaka ya 2600 BC. Mnamo mwaka 1548, kitunguu saumu kiliingia nchini Uingezera kutoka katika bahari ya Mediterranean. 

 

Faida za kitunguu saumu ni zipi?

Kuna faida mbalimbali zitokanazo na kitunguu saumu; faida hizi kwa asilimia kubwa zinachangiwa na compound ya allicin ambayo hupatikana katika kiungo hiki. Allicin hii pia ndo hukipa kitunguu saumu harufu yake ya kipekee. 

 

Zifuatazo ni baadhi ya faida za kitunguu saumu:

1. Kuimarisha afya ya mfumo mzima wa moyo pamoja na mishipa inayopitisha damu, na kuzuia magonjwa mbalimbali ya moyo na magonjwa yanayotokea katika mishipa ya damu. Shinikizo la juu la damu, au presha, pia inapatikana katika kundi hili la magonjwa.  

 

2. Mwaka 2023, tafiti iliyofanywa na Frontiers in Nutrition ikiongelea faida ya kitunguu saumu iliyoonyesha kuwa kiungo hiki husaidia kupambana na vimelea vya cancer katika tumbo. 

 

Walieleza kuwa namna hii ni kwa sababu watu wengi, nyakati hizi, wamekua wakitumia fast food na sio vyakula asilia ambavyo vina uwezo wa kuwekewa vitunguu saumu – ambavyo vinaleta faida hio ya kupambana na vimelea vya saratani katika tumbo. 

 

3. Kitunguu saumu pia kimeonekana kuwa na faida ya kupambana na vijidudu ambavyo husababisha magonjwa yanayoambukizwa 

Kama tunavyojua kitunguu saumu kilivyo kikali (kutokana na allicin) hivyo si rahisi kwa wadudu kukisogelea. Hii ni kwa sababu ya uwezo wake wa kupambana na wadudu mbalimbali ikiwemo microorganisms wanaoleta magonjwa mbalimbali kama vile kuharisha, kukohoa na kadhalika. 

 

4. Tafiti ilifanyika na kuonyesha kwamba kitunguu saumu kinaweza kuwa na faida ya kushusha kisukari mwilini. 

 

Hivyo basi matumizi yake yanaweza kuwa na faida ingawa tafiti hii haimaanishi kwamba kama umegundulika na kisukari basi usinywe dawa na ule vitunguu saumu tu!  Unapaswa kufuata ulaji mzuri wa chakula pamoja na kutumia dawa zinazosaidia kudhibiti sukari. 

 

Zingatia

Kitunguu saumu ni kikali sana hivyo kikiliwa katika ubichi, na kwa wingi, huweza kusababisha michubuko na matatizo mengine ikiwemo shida katika ini.  Hii itukumbushe kuwa chakula ni kama dawa hivyo tunapaswa kukitumia katika viwango sahihi.  

 

Namna salama ya kutumia kiungo hiki ni kwa kukiunga katika chakula kama tulivyozoea japo kinaweza kuwa kinapungua nguvu ya faida zake kama kitakaangwa kwa muda mrefu. 

 

Hivyo basi ni vyema kukiweka baada ya kuweka karoti au nyanya katika mboga ya mchuzi ili kisikaangwe na mafuta na kupoteza faida zake. 

 

Je ni kiasi gani cha vitunguu saumu unapaswa kutumia na kwa kiwango gani? 

Utumiaji wa kitunguu saumu kimoja kwa siku sio mbaya ila inapaswa kuwa unatumia pamoja na vyakula vingine mfano kukipika kwenye mboga au nyama. Namna ambayo kitunguu saumu kinatumika katika maeneo mengine ni kwa kutengenezea sauce (mchuzi) mbalimbali ambazo husindikiza vyakula vingine au kukiweka katika kachumbari.  

 

Hizo ndio faida za kula kitunguu saumu. Nikukumbushe tu kuwa ni muhimu kupanga machaguo mazuri pale unapotaka kula. Pia endelea kuchagua vyakula vilivyo na kitunguu saumu.  

 

Asante kwa kusoma makala hii , tukutane katika makala ijayoya lishe.  

3 thoughts on “Uwezo na Faida za Kitunguu Saumu Mwilini ”

  1. It’s а pity you don’t have a donate button! I’ԁ certаinly donate to tһis superb blog!
    I guess for now i’ll settle for book-marking and
    adding your RSS feed to my Google aсcount. I look forwɑrd to fresһ updates
    and will talk about this blog with my Facebook group.
    Chat soon!

  2. When sߋmеone writеs an post he/she maintains the
    thought of a user in his/her mind that hߋw
    a user can know it. Thus that’s why this paragraph is perfect.
    Ƭhanks!

Leave a Comment

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

swSW