Katika habari zilizozua gumzo duniani kwa sasa ni baada ya mitandao mbalimbali duniani kuripoti mpango uliodokezwa na kampuni ya Tesla inayomilikiwa na tajiri namba moja duniani – Elon Musk.
Kampuni hii imegusia mpango wa kutengeneza roboti aitwae Optimus Humanoid – ambaye atakuwa na uwezo wa kubeba mimba miezi 9.
Roboti hii ikikamilika itawafanya wazazi kuepuka na kazi nzito ya kubeba na kulea mimba. Watatakiwa kupeleka mayai yao na roboti hiyo itabeba ujauzito kwa miezi tisa huku ikiwaacha wazazi na muda wa kufanya mambo mengine; kuhudhuria masomo, kufanya biashara, na kadhalika.
Pia roboti hizi zinatarajiwa kupunguza hatari za mimba kwa mama kama presha, kifafa, kupoteza damu na uwezekano wa kupoteza maisha.
Changamoto inayooneka hapa ni gharama za kupata huduma hii ambazo zinatarajiwa kuwa kubwa na wengi kushindwa kumudu gharama.
…
Ikitokea roboto hii imekuja Tanzania, utakua tayari (pamoja na mwenzi wako) kuitumia? Niandikie maoni yako hapo chini.

Chief Content Officer (CCO) at Abite Afya
I’m responsible for overseeing the entire content strategy, ensuring that all published materials align with the blog’s mission, audience needs, and business goals.