Sababu 3 Kwanini Unapata Maumivu ya Mgongo  

Kama umefatilia, tatizo la maumivu ya mgongo ni moja ya matatizo sugu sana kwenye jamii yetu; kama sikosei, wewe pia limeshakukuta au unalo. 

 

Hauko peke yako, kutokana na ripoti za Shirika la Afya Duniani, takribani ya watu million 619 duniani wanasumbuliwa na maumivu ya mgongo. Hii ni sawa na asilimia 10% ya watu wote duniani!

 

Tatizo hili huanza kuwa kubwa kwenye umri kuanzia miaka 45 na kuendelea bila kujali jinsia; japo huwa kubwa kwa zaidi ya asilimia 10% kwa wanawake hasa baada ya kumaliza hedhi. 

 

Je, unafahamu kwanini maumivu yako ya mgongo hayaondoki?

1. Mikao na milalo isiyostahili 

Unafahamu kwamba jinsi unavyokaa, iwe kwenye kiti au kochi, ina mchango mkubwa kwenye maumivu ya mgongo? 

 

 

Kinachotokea ni hiki, uti wa mgongo una shepu yake ambayo ina mikunjo mitatu kuanzia juu mpaka chini; pia kuna misuli ambayo hushikilia uti wa mgongo kutoka pande zote  na misuli hiyo huwa ina’balance na ku’relax kama ukiwa umekaa kwenye mkao mzuri. 

 

Kwa kawaida mkao mzuri kwa ajili ya kulinda mgongo wako ni kukaa wima (upright position sitting). Hii inaitwa mkao wa usawa yaani neutral position.

 

Ukaaji huu hufanya misuli ya mgongo kupumzika na hivyo kufanya mgongo usiume. 

 

Tatizo liko wapi? 

Mikao yetu mara nyingi haiko kwenye neutral position kwasababu mbalimbali kama kukalia viti vifupi au virefu kupita size yetu, makochi ya kubonyea, pamoja na viti vingi vya maofisini kutokua na muundo unaoendana na muundo wa uti wa mgongo. 

 

Vingi unakuta vimenyooka sana hivyo mtu atakaa kwenye mkao wima kwa dakika chache, atachoka, na kuegemea mbele au pembeni. Unapoegemea mbele au pembeni hufanya misuli ya mgongo, hasa wa chini, kuvuta sana na kukaza kutokana na kukosa usawa.  

 

Hii ndio hupelekea mgongo wa chini kuanza kupata maumivu ya mara kwa mara hasa kwa watu wanaokaa maofisini muda mrefu. 

 

Kama wewe ni mdadisi utakuwa umegundua jambo moja: ukiwa na kazi ya kiofisi (au kazi binafsi) na unatumia computer kuifanya ukiwa umekalia kiti cha plastiki, kochi au kitanda, baada ya nusu saa tu utaanza kusikia maumivu ya mgongo, uongo? 

 

Sasa maumivu haya yanaweza kudumu muda mrefu kutokana na kutojua sababu na pia kutokuwa na uwezo wa kubadilisha mazingira ya kazi. 

 

Unafahamu pia namna unavyolala huchangia maumivu ya mgongo? 

Moja ya mlalo ambao husababisha zaidi maumivu ya mgongo ni kulalia tumbo. Mlalo huu hufanya uti wa mgongo, hasa sehemu ya shingo, kujikunja na hivyo kufanya misuli ijivute sana na mwisho wake hupelekea maumivu ya shingo na mgongo. 

 

proper sleeping position

 

Sababu nyingine ya maumivu ni matumizi ya mito midogo sana au mikubwa sana. Kwa kawaida mto mzuri ni ule unaofanya uti wa mgongo wako uwe katika usawa hivyo usiwe mkubwa sana na usiwe mdogo sana, uwe wa wastani tu!  

 

Pia inashauriwa kuweka mto katikati ya miguu hasa kama umelala upande ili kuzuia kuzungusha sehemu ya mgongo wako ukiwa umelalia ubavu. 

 

2. Kukaa muda mrefu 

Uti wa mgongo una pingili na katikati ya kila pingili huwa kuna sponji yenye ute ambayo husaidia kuzuia joint na joint kugusana. Sasa kukaa muda mrefu hupeleka presha kubwa kwenye uti wa mgongo na kuleta mgandamizo ambao husababisha maumivu kwenye mgongo.  

 

Watu wanaokumbwa na tatizo hili ni watu wa maofisini, madereva, mafundi cherehani, marubani, na kadhalika. 

 

Hali hii huleta maumivu makali kutokana na kutofahamu na kukosa namna ya kufanya kutokana na mazingira ya kazi yalivyo. 

 

3. Ugonjwa wa mgongo 

Umri unaposogea pingili za uti wa mgongo huanza kuchoka na ile juice ya katikakti hupungua sana. Hali hii hupelekea kupata ugonjwa unaoitwa osteoarthritis.

 

Hii ni hali ya pingili za mgongo kusuguana na hivyo kuvimba na kusababisha maumivu makali ya mgongo.  Tatizo hili lipo zaidi kwa wazee.

 

Magonjwa mengine ni kama Tb ya mgongo hasa kwa watu wenye kinga ndogo ya mwili (wagonjwa wa HIV, Cancer, etc.) 

 

Kama una maumivu ya mgongo yaliyoanza na hayaondoki, na hayausiani na namba moja au mbili, nashauri ufanyiwe vipimo kujua sababu. Usikae nayo nyumbani huenda ni jambo kubwa zaidi. 

 

Muhimu: Sababu nyingine za wazi ni ajali ya vyombo vya moto au kuanguka kutoka urefu wa juu. Hii husababisha pingili kuvunjika au kuchomoka na matibabu yake yanaweza kuchukua muda mrefu sana. 

 

Suluhisho la hayo yote ni nini?

Badili mikao yako: Epuka kukalia viti vifupi au virefu kupita urefu wako. Hakikisha walau uwiano wa meza unayotumia inafika kwenye kitovu chako.

 

Badili kiti unachokalia, kama una kazi za muda mrefu nunua office chair ambayo utaweza kuongeza au kupunguza urefu na kufikia pale panapostahili.  

 

proper office chair as a relief solution to back pain

 

Epuka kutumia kiti cha plastiki kufanya kazi za muda mrefu. Epuka kukalia viti vinavyobonyea chini kwasababu hukulazimisha kupinda mgongo. 

 

Kama una shida ya mgongo na unapaswa kusafiri umbali mrefu basi jaribu kununua ile mito maalumu ya kukalia au kuegemea ambayo unaweza kuicheki dukani kwetu, Abite Nyumbani. 

 

Pia epuka kulalaia godoro lililoisha sana au linalobonyea sana. Sifa ya godoro inabidi liwe gumu kiasi kwa ajili ya kunyoosha mgongo vizuri. 

 

Ulishagundua kwanini ukilala kwenye kochi usiku mzima unaamka mgongo unauma? Kochi linafanya uti wa mgongo upinde  na hivyo misuli ya mgongo huvutika sana na kupelekea maumivu. 

 

Kama unafanya shughuli zinazokulazimisha kukaa muda mrefu basi jaribu kujipa break katikati ya mikao na kutembea kidogo au kusimama. Hii husaidia kupunguza presha kubwa kwenye uti wa mgongo na kupunguza hatari ya kupata shida ya mgongo. 

 

 

Kama unasumbuliwa na changamoto yoyote ya maumivu ya mgongo, basi usisite kutembelea duka letu la vifaa tiba (physiotherapy and rehabilitation medical equipment) ambapo utapata nafasi ya kuongea na daktari wetu pamoja na kupatiwa kifaa kitachokusaidia kutatua changamoto yako.

 

Duka letu linapatikana Sinza Mori, jengo la Azaria Plaza (ofisi namba 14), opposite kabisa na Kitambaa Cheupe Lounge. Karibu Sana!

Leave a Comment

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

swSW