Njia 2 za kutengeneza unga wa lishe kwa ajili ya mtoto wako na familia

Unga wa lishe, katika jamii yetu, umezoeleka kuwa ni unga ambao unatumiwa na watu kwa ajili ya kupikia uji ambacho ni chakula kinachotumiwa na watu wengi – asubuhi au jioni.

 

Au kama kutakua na mgonjwa, basi hutengenezewa uji ili aweze kupata chakula kinacholika kwa urahisi hasa kwasababu chakula hichi huwa katika hali ya kimiminika.

 

Vyakula vya hali ya kimiminika ni vizuri sana kwa wagonjwa kwani hurahisisha hali ya matumizi hasa katika kumeza na umeng’enywaji wa chakula hichi kwasababu hakitumii muda mrefu kutafunwa.

 

Lakini pia watu wengi hupendelea kutumia uji kwasababu ni chakula kinachochukua muda mfupi kutengeneza na hauhitaji gharama kubwa kukipata.

 

Je wajua!

Unga wa uji wa lishe unapaswa kuwa na nafaka chache kwani uwepo wa nafaka nyingi huleta changamoto katika kutayarisha chakula hicho kwasababu kuna nafaka zingine huchukua muda mrefu kuiva kuliko nyingine.

 

kwa mfano uivaji wa kawaida wa mahindi ni tofauti na ule wa maharage ihali zote ni nafaka.

 

Pia kuna baadhi ya vyakula kama karanga ambazo huhitaji umakini mkubwa katika kutengeneza kwasababu huwa zina tabia ya kuoza na hivyo hushauriwa kuchaguliwa kwa umakini kama zitakua zina ulazima wa kutumika katika unga wako wa uji.

 

Karanga zako zinatakiwa kuwa nzima zisizo na weusi kwani weusi wa karanga huashiria sumu kuvu ambayo ni aina ya sumu inayotolewa na fangasi anayepatikana katika mimea iliyoshambuliwa ikiwemo karanga.

 

Hawa fangasi huweza kuhatarisha maisha kama mtu atatumia vyakula vyenye sumu kuvu.

 

Jinsi ya kutengeneza Unga wa Lishe kwa urahisi

Vitu vya kutumia

  1. Mahindi ya njano (unaweza weka kilo mbili): Mahindi haya yameongezewa virutubishi vya vitamin A kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili
  2. Mbegu za maboga (nusu kilo): Hutakiwa kuwa nzima na zisizo na weusi kwasababu weusi huu huashiria kuharibika kwa mbegu.

 

Lakini pia ukipenda unaweza kusaga mahindi peke yake na ukaweka mbegu za maboga na viungo vingine pale ambapo unapika na sio kuchanganya wakati wa kwenda kusaga.

 

Mbegu za maboga ni chanzo cha kirutubishi cha protini ambacho hujenga mwili pamoja na kuwa na mafuta ambayo husaidia kuupa mwili joto .

 

Tuingie jikoni…

Katika siku ya pishi unaweza kukoroga unga wako wa mahindi jikoni mpaka utakapoona umekua tayari.

 

Ukachanganya mbegu zako za maboga viko viwili au kimoja kutokana na kiasi cha uji na kuendelea kukoroga.

 

Halafu ukaweka karanga yako, mfano kwenye kiasi cha robo lita ya uji unaweza kuweka kijiko kimoja. Unaweza pia ukaweka kijiko kimoja cha mafuta ya alizeti kama ukipenda.

 

Binafsi huwa sipendelei kutumia mafuta ya alizeti kwenye uji kutokana tu na mazoea yangu ya kutumia karanga, yaani peanut butter, kwasababu karanga zina mafuta tayari.

 

Kama sitatumia peanut butter, nitatumia siagi kijiko kimoja kidogo kwenye kikombe cha uji pamoja na sukari kijiko kimoja pia. Mara nyingi ninapendelea kuunga sukari wakati uji ukiwa jikoni.

 

Namna nyingine ambayo imezoeleka na watu katika upikaji wa uji ni uwekaji wa maziwa; inaweza kuwa maziwa fresh au maziwa mtindi.

 

Yote ni machaguo sahihi. Hutegemea tu na mapendeleo ya mtu binafsi.

 

Unaweza ukawa unajiuliza kuna aina ngapi za unga wa lishe?

Hapo juu nimeonyesha aina ya unga wa lishe unaoweza kutengeneza utakaokua na virutubishi katika ulaji wa uji.

 

Kumbuka kwamba huu utakua mlo mmoja tu na unapaswa kuchanganya vyakula mbalimbali katika siku ili uweze kupata virutubishi vingine hasa vya madini na vitamini.

 

Muhimu: Sishauri kutumia nafaka nyingi katika kutengeneza unga wa lishe kwasababu ya usalama kwa watu wa rika zore ikiwemo watoto. Ndio maana katika makala hii nimetumia mfano wa nafaka moja yaani mahindi.

Usalama ninaouongelea hapa ni katika swala la umeng’enywaji wa chakula kwani nafaka zingine kama ulezi huweza kupelekea changamoto ya kupata choo hasa kwa watoto.

 

Kuna njia nyingine ya jinsi ya kuutengeneza?

Kama utakua ni mpenzi wa soya, basi unaweza kuweka mahindi yako ya njano kilo mbili pamoja na soya nusu kilo.

 

Soya hizi zinapaswa kuoshwa vizuri na kuanikwa; pindi zinapokauka zinakaangawa kidogo kwa kutumia sufuria isiyo na mafuta, na kisha kuchanganywa na mahindi tayari kwa ajili ya kusagwa.

 

Mwisho…

Mara nyingi huwa ninapenda kuwaambia wateja wangu kwamba unatakiwa ufurahie chakula unachokula na hii inawezekana kwa kupika vizuri.

 

Ili uweze kula chakula kitakachokusaidia kupata afya njema inabidi ukifurahie na huwezi kufurahia chakula kisichokua na ladha nzuri.

 

Hivyo jitahidi kuwa na ubunifu na kuongeza ujuzi katika uandaaji wa milo yako pindi unapokua nyumbani ili hata watumiaji wengine waweze kukifurahia.

 

Kwa upande wa watoto, ni muhimu kupika uji ambao una ladha nzuri na usio na sukari nyingi kwani inaaminika kwamba watoto wanapenda vitu vya sukari dhana ambayo sio kweli.

 

Hili naomba niliweke kwenye quote kabisa kwa ajili ya msisitizo:

Watoto hawapendi sKari nyingi katika vyakula, watoto huzoeshwa vyakula vya sukari nyingi na hivyo hujenga tabia ya kukataa vyakula vingine kwasababu hupatwa na kitu kiitwacho “Sweet tooth”

Sweet tooth inamaanisha watoto hujenga tabia ya kupenda kula sukari nyingi kwasababu ya kuzoeshwa kutumia vyakula vya sukari.

 

Nimeona niwekee msisitizo kwa upande wa watoto maana wao ndio watumiaji wakubwa wa chakula cha uji.

 

Nina imani utakua umejifunza namna nzuri na rahisi ya kutengeneza unga wa lishe kwa ajili ya matumizi yako ya nyumbani.

 

Kama una swali lolote linalohusiana na makala hii, usisite kuniandikia kwenye comments section.

8 thoughts on “Njia 2 za kutengeneza unga wa lishe kwa ajili ya mtoto wako na familia”

  1. Asante daktari… Elimu safi, tumezoea kuweka makolokolo mengi kwenye unga6, kumbe ni simpo tu

  2. Habari yako hellen ,kwa watoto wasiopenda kula huwa kunakua na utofauti wa mtoto na mtoto. Huwa ninapenda kuongea na wazazi au walezi kwa ukaribu ili niweze kubaini sababu za mtoto kutokupenda kula. Tabia ya kula (eating habit) ni swala linalohitaji mahojiano kitaalamu na huwa na mafanikio , ni rahisi kubaini sababu baada ya kuongea na pia kujaribu njia mbalimbali zinazohusisha uandaaji na utofoutishaji wa vyakula . Wasiliana nasi ili tuongee kwa kina . Nipo tayari kukusikiliza. Karibu sana sana

  3. Immanuel Makundi

    Habari doc. Sorry nilikua naomba unisaidie mchanganuo ws nafaka za kuandaa unga wablishe ya mtoto pia kwa njia ya kgs kwamaana ya ninapo taka tutumia let’s say kilo ya mahindi nitachanganya na nini na kwa kias gani kulingana na kiasi hicho tajwa cha mahindi,?

Leave a Comment

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

swSW