Mtoto Wangu Haongezeki Uzito, Nifanye Nini?

“Mtoto wangu haongezeki uzito, nifanye nini?”

 

Hili ni swali ambalo liko katika akili za wazazi wengi wanaojali afya za watoto wao, kipindi ambacho watoto wanakua wananyonya na katika kipindi ambacho watoto wanaanza kutumia vyakula mbadala. 

 

Muhimu ni kufahamu kwamba kipindi ambacho mtoto anakua kunakua na kiasi maalumu cha upandaji wa uzito huu. 

 

 Mfano, watoto kuanzia umri wa siku moja mpaka watoto waliotimiza kipindi cha mwaka mmoja huongezeka uzito kwa kasi kubwa zaidi ya watoto wenye zaidi ya mwaka mmoja.

 

Huwa ninapenda kuwaambia wateja wangu kwamba mtoto wako afikapo miezi mitatu baada ya kuzaliwa, anapaswa kuwa na mara mbili ya uzito aliozaliwa nao 

 

Hii inamaana ya kwamba kama mtoto wako alizaliwa na Kilogram 3, basi baada ya miezi mitatu tunategemea kwamba atakua na kilo kuanzia 6.  

 

Ongezeko hili la uzito mara dufu linatuonyesha ya kwamba mtoto anapata lishe bora na kwa wakati sahihi. Hii hutokana na kunyonyeshwa ziwa la mama (kwa watoto wale ambao mama zao wanaweza kuwanyonyesha) na kwa wale ambao wanapewa maziwa mbadala (chini ya usimamizi wa wataalamu), kwa usahihi. 

 

Vifuatavyo ni visababishi vya mtoto kutokuongezeka uzito:

1. Ubora hadhifu wa maziwa ya mama 

Maziwa ya mama, katika kipindi cha miezi 6 ya mwanzo, yanapokosa ubora kutokana na lishe duni ambayo mama anatumia kipindi cha kunyonyesha huweza kupelekea maziwa kutokutengenezwa kwa kiwango kikubwa na ya kutosheleza mahitaji ya mtoto.  

 

Mfano ambao napenda kuutumia ili kuwezesha uelewa mrahisi ni ufugaji wa ng’ombe na mbuzi. Wanyama hawa wanaonyonyesha huhitaji chakula cha kutosha ili kuwezesha utengenezwaji wa maziwa, na hivyo basi kama mama anayenyonyesha atashindwa kula ipasavyo hataweza kupata maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto wake. 

 

Hali kama hii ndio hupelekea utapiamlo kwa watoto wachanga , jambo mbalo linaepukika kwa asilimia 100.  

 

2. Namna ya kunyonyesha mtoto pia inapaswa kujulikana ili kuepuka mtoto kupungua uzito 

Sehemu hii nitazungumzia swala la muda na mkao katika kipindi cha kunyonyesha.  Nianze kwa kutambua kwamba katika miaka ya karibuni wanawake wengi wanajishughulisha na shughuli mbalimbali ambazo huwa zinatubana na kupelekea kupata muda mchache wa kuwanyonyesha watoto hawa chini ya miezi sita. 

 

Hii ni tofauti na vipindi vya zamani ambapo akina mama walibaki nyumbani kwa ajili ya malezi ya watoto na walipata muda mzuri wa kuwanyonyesha. 

 

Swala lingine la muda huhusisha muda gani mtoto anapaswa kunyonya. Binafsi hupenda kuwaambia wateja wangu kwamba mtoto anapaswa kunyonya kila baada ya masaa mawili na hupaswa kukaa katika ziwa kwa muda wa dakika 15 mpaka 20 

 

Na mama anapaswa kunyonyesha mpaka atakaposikia ziwa moja limelegea, ikimaanisha maziwa yameisha, ndipo ahamie ziwa jingine kwani hapo mtoto anakua amepata virutubishi vyote muhimu na vinavyoujenga mwili. 

 

Watoto wanaoanza kupatiwa vyakula vingine baada ya miezi sita ya kunyonya (kulikizwa)

Katika vipindi hivi vya kulikizwa mtoto anapaswa kula vyakula kutoka katika makundi yote ya chakula; vyakula asili ya wanyama kama vile kuku na samaki, vyakula asili vya mbogamboga, matunda, nafaka, mizizi yenye wanga na ndizi mbichi, pamoja na mafuta. 

 

Ingawa katika kumuanzishia unapaswa kuanza chakula kimoja kimoja ili kutambua kama kuna allergy ya chakula chochote. Hata hivyo haishauriwi kumpa mtoto maziwa ya ng’ombe mpaka atakapofika kipindi cha mwaka mmoja. 

 

Mtoto atakayekua anakula chakula kutoka katika makundi hayo mbalimbali ataweza kupata virutubishi muhimu vitakavyomsaidia katika safari yake ya ukuaji. 

 

Asante kwa kusoma makala hii, tukutane katika makala ijayo. 

Leave a Comment

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

swSW