Mnamo tarehe 20 October 2024, Shirika la Afya Duniani (WHO) liliipatia Nchi ya Misri cheti cha kufanikiwa kutokomeza Malaria (Malaria Free certificate).
Hatua hii imefikiwa baada ya taifa hilo kujizatiti kuweka hatua za kupambana na ugonjwa huu baada ya kushuhudia vifo vingi miaka mingi iliyopita – toka enzi za mafarao.
Hatua hii inaifanya Misri kuwa miongoni mwa nchi 44 duniani kupata cheti hiki ikiungana na nchi za Morocco na Falme za Kiarabu (UAE).
Miongoni mwa hatua walizozifanya kufikia mafanikio haya, kuanzia miaka ya 1920, ni pamoja na kupiga marufuku kilimo cha mazao mbalimbali karibu na makazi ya watu.
Pamoja na hayo, kufikia mwaka 1942 idadi ya watu wenye malaria ilipaa na kufikia milioni 3. Hivyo waliitangaza Malaria kama janga la taifa, na kuja na mbinu mkakati kama kufungua vituo 16 vya afya katika majimbo mbalimbali kupambana na malaria, kuajiri watumishi zaidi ya 4,000 kwa ajili ya kupambana na malaria.
Pia walianza kutoa huduma kwa wagonjwa wa Malaria bure nchi nzima bila kujali hali ya uchumi wa mtu binafsi hivyo kupunguza vifo vinavyosababishwa na malaria kwa kiasi kikubwa.
Mwisho uhusiano wao mzuri na nchi jirani kama Sudani umewawezesha kuweza kupima ipasavyo watu wote wanaoingia na kutoka nchini hivyo kufikia hatua ya kumaliza kabisa ugonjwa huu.
Hongera sana Misri.
…
Unadhani ni kwanini Tanzania hatujafikia hatua hii? Niandikie maoni yako kwenye comments section.

Chief Content Officer (CCO) at Abite Afya
I’m responsible for overseeing the entire content strategy, ensuring that all published materials align with the blog’s mission, audience needs, and business goals.
Tһis pߋst is w᧐rth eνeryone’s attention. How cаn I find out more?
Visit my web blog: Dewa77
Keep reading our blog for more information,
For more details about this news go to WHO news Page.