Unapenda Chipsi Mayai? Fahamu Mambo Haya

Wengi wetu tunapenda kiepe, chipsi zege, ama chipsi mayai. Na tena, kiepe ni love language kwa baadhi ya couples. Chipsi pia hupendwa sana na baadhi ya wagonjwa.

 

 

 

Kama umeamua kuchukulia afya yako serious, chipsi ni moja kati ya vyakula unavyopaswa kuviepuka au kubadili namna unavyoiyandaa.

 

Kiufupi chipsi sio hata love language, ni kiashiria kwamba unauchukia mwili wako kwa kuuongezea kiasi cha sumu ambacho ungeweza kukiepuka.

 

Chipsi ni sawa na sigara?

Moja kati ya jumbe zilizowafokea wengi mwaka 2023 ni huu ujumbe mfupi wa Dr. Boaz Mkumbo (mtaalam wa magonjwa yanayosababishwa na ulaji mbaya);

Sumu za chipsi na kuku wa kukaanga huitwa Reactive Oxygen Species (Free Radicals). Na sumu zinazotoka kwenye moshi wa sigara nazo huitwa free radicals. Ukila chipsi ni sawa mtu anayevuta sigara. Na madhara yake ni sawa katika mwili wa binadamu.

 Free radicals ni nini hasa?

Ni kemikali zinazozalishwa wakati wa mabadiliko ya molecules ndani au nje ya mwili. Kemikali hizi huwa zimebeba oksijeni ndani yake.

 

Free radicals zilizo kwenye chipsi na vyakula vingine vya kukaanga pamoja na sigara huitwa acrylamide. Japo sigara ina aina nyingi zaidi za free radicals na sumu nyingi.

 

(Kujua mengi kuhusu sigara, pakua kitabu chetu cha “Sigara, Jasusi Anayetabasamu!“)

 

Utafiti wa awali uliochapishwa mwaka 2009 katika The American Journal of Clinical Nutrition unatabainisha kwamba uvutaji wa sigara na ulaji wa chipsi kwa muda mrefu ni chanzo cha kemikali aina ya acrylamide.

 

Kwanini watu wamezoea chipsi mayai?

Ulaji wa chipsi na vyakula vingine vinavyokaangwa kwa mafuta ya mbegu katika joto la juu zaidi huhatarisha afya ya mlaji. Hizi ni namna ambavyo chipsi hugeuka kuwa rafiki wa wengi na kupelekea baadhi ya magonjwa;

 

1. Ni chakula cha haraka zaidi kuandaa

Hakihitaji muda mwingi. Kinabebeka na kinaptiikana muda wowote. Ni wewe kuwa karibu na location tu. Hivyo, chipsi ni kimbilio kwa watu wasio na muda wa kupika na ambao hawapendi usumbufu wa kuandaa chakula.

 

2. “Status symbol”

Sura ya pili ya ulaji wa chipsi ni chakula ambacho hutoa status symbol, kwamba mlaji ni mtu wa mjini au mjanja.

Anaweza kumudu walau ‘anasa’ ya kula chipsi. Ingawa unaweza kupata kiepe kwa gharama ndogo kuliko supu ya kuku. Haishangazi kuona mama anauza viazi vitamu, lakini kaketi na mwanae wanakula kiepe.

 

3. Kudhani ni kipunguza mawazo

Pia, chipsi pamoja na vyakula vingine vilivyochakatwa hutumiwa vibaya kwa watu walio katika hali ya mfadhaiko au msongo wa mawazo. Aina hii ya chakula hupelekea pia uteja, yaani addiction.

 

Kwanini chipsi ni mbaya kwa afya yako?

Mambo makuu matatu huifanya chipsi isiwe chaguo bora la chakula kinacholeta afya ndani ya mwili wako;

1. Matumizi ya kemikali katika ulimaji wake ni makubwa mno

Viazi ‘ulaya’ ambavyo ndio hutumika hasa katika kutengeneza chipsi hulimwa kwa wingi na wakulima ili kukidhi mahitaji ya soko kwa sababu zinahitajika karibu kila kona ya mji. Hivyo, hulazimu wakulima kutumia kemikali katika kuua wadudu na mbolea nyingine za kukuzia.

 

Kemikali aina ya glyophosate ni kiua vidudu kinachotumika hasa katika ulimaji wa viazi mviringo. Hii kemikali huhusishwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani na mvurugiko wa homoni mwilini.

 

2. Virutubisho vichache zaidi

Viazi ‘ulaya’ ni moja kati ya vyakula vyenye kiasi kikubwa sana cha wanga na kiasi kidogo cha virutubisho vingine muhimu. Vina uchache wa protini, madini na vitamini nyingine muhimu.

 

Kumbuka kwamba mara zote mahitaji ya zao yakiongeezeka, aina mpya ya mbengu hutengenezwa. Kama ilivyo katika ngano, mazao mengi katika wakati wetu yana kiasi maradufu cha wanga.

 

Hapa ndio tunapata ile dhana ya kwamba sisi ni kizazi ambacho tunakula sana, lakini bado miili yetu inakosa virutubisho vya msingi.

 

Kama msosi wako kila siku au mara nyingi ni chipsi zege, hebu fikiri utapata wapi vitamini kama B12, D, K2 na folic acid? Au utapata wapi madini kama manganese, selenium na zinki?

 

Unahitaji virutubisho vyote hivi ili chembe hai mwilini wako ziweze kufanya kazi vyema. Cha ajabu, ndo unakula wanga na mafuta ‘mabaya’.

Kumbuka wanga hugeuzwa kuwa sukari, na kisha kuwa mafuta na kuhifadhiwa mwilini. Hii husababisha kuongezeka kwa uzito na unene.

3. Mafuta yanayotumika kukaangia huzalisha kemikali hatarishi

Unaikumbuka ile hoja kwamba ukila chipsi zege, ni sawa na mtu anayevuta sigara. Unajiuliza kwanini sigara inasemwa sana na sio chipsi? Ni kwa sababu wengi wetu tunapenda kula aina hii ya chakula na tuko addicted.

 

Ukweli ni kwamba, ukiachana na sababu mbili za hapo juu, mafuta yanayotumika kukaangia viazi ni kihatarishi kingine. Fikiria wauza chipsi pale stendi ya Makumbusho au maeneo ya vyuoni. Hurudia kukaangia mafuta yaleyale kabla ya kubadilisha.

 

(Kujua mengi kuhusu mafuta ya kupikia, pitia chapisho hili)

 

Ukiachana na kurudia mafuta, matumizi ya mafuta ya mbegu au mimea sio salama kukaangia na kupikia chakula kwenye joto kubwa. Mafuta haya yana kiasi kikubwa cha asidi za fati ambazo siyo imara na stahimilivu kwenye moto. Hivyo, yakipashwa kwenye nyuzi joto kubwa kama ilivyo wakati wa kukaanga chipsi huzalisha free radicals.

 

Uzalishwaji wa kemikali sumu (free radicals) husababisha msongo wa sumu mwilini (oxidative stress), pamoja na shambulio ndani ya mwili (inflammation).

 

Hivi vyote huhusishwa na magonjwa mbalimbali kama vile shinikizo la juu la damu (presha), magonjwa ya moyo, pumu ya kifua na pumu ya ngozi, maumivu ya viungo (arthritis), maumivu makali wakati wa hedhi, kifafa cha mimba, shambulio katika kuta za tumbo (gastritis), na wakati mwingine hupelekea mvurugiko wa homoni unaosababisha kushindwa kushika mimba kwa wanawake.

 

Na zaidi, ulaji wa vyakula vilivyokaangwa kwenye aina hii ya mafuta hupelekea uchovu uliokithiri pamoja na upungufu wa nguvu za kiume.

 

Dk. Stephen Sinatra alihitimisha kwamba shambulio la kuta za mishipa midogo ya damu mwillini yaani Endothelial Dysfunction (ED) ni sawasawa na Erectile Dysfunction (ED) yaani upungufu wa nguvu za kiume.

 

Vyanzo vikubwa vya Endothelial Dysfunction ni oxidative stress na inflammation ambavyo husababishwa na sukari, matumizi mabaya ya mafuta ya mbegu na vyakula vilivochakatwa na msongo wa mawazo.

 

Watu walioathirika na magonjwa ya pumu na shinikizo la juu la damu hawawezi kupata nafuu kama bado wanaendelea kuongeza msongo wa sumu katika miili yao. Na wanakuwa hatarini kupata mashambulizi ya mara kwa mara ya magonjwa hayo.

 

Hauhitaji kuendelea kuwa store ndogo ya sumu mwili.

 

Bado ninatamani kula chipsi. Nifanye nini?

Kama bado unatamani kuendelea kula viazi vya kukaanga yaani chipsi, ni muhimu kuzingatia ushauri ufuatao;

Tafuta viazi ambavyo vina hali ya ubora na vimetumia kemikali kiasi kidogo au sufuri wakati wa ulimaji wake. Vikaange kwa mafuta mazuri kama ya nazi au ya wanyama. Usirudie matumizi ya mafuta.

 

Wakati wa kula, tumia pia protini na vyakula vya mafuta kama parachichi. Matumizi ya namna hii hupunguza ongezeko la kasi la sukari kwenye damu, hukufanya ushibe upesi, na pia kunatoa virutubisho vingine muhimu.

 

Yote hapo juu yanawezekana endapo utaandaa chipsi nyumbani kwako mwenyewe. Hakuna genge la chipsi litakalozingatia mambo haya kwa ajili yako. Jukumu ni lako mwenyewe.

 

….

 

Asante kwa kuendelea kuwa sehemu ya Abite Afya. Tunajivunia kuendelea kukuhudumia kupitia huduma mbalimbali kama makala na e-books za afya zinazopatikana katika tovuti yetu, na huduma ya ushauri wa daktari.

 

Tunapoelekea mwisho wa mwiaka, tunapenda kukutakia heri na fanaka ya sikukuu za Noeli na Mwaka Mpya.

 

Endelea kusalia nasi, kumbuka ku-subscribe ili upatae makala zetu moja kwa moja, kuandika maoni yako na kuwashirikisha wengine.

#!trpst#trp-gettext data-trpgettextoriginal=733#!trpen#2 thoughts on “<trp-post-container data-trp-post-id='1113'>Unapenda Chipsi Mayai? Fahamu Mambo Haya</trp-post-container>”#!trpst#/trp-gettext#!trpen#

#!trpst#trp-gettext data-trpgettextoriginal=11#!trpen#Leave a Comment#!trpst#/trp-gettext#!trpen#

#!trpst#trp-gettext data-trpgettextoriginal=723#!trpen#Your email address will not be published.#!trpst#/trp-gettext#!trpen# #!trpst#trp-gettext data-trpgettextoriginal=715#!trpen#Required fields are marked *#!trpst#/trp-gettext#!trpen#

en_USEN