Unafahamu mawe yanaweza kuundwa mdomoni?

Inawezekana hujawahi sikia kuwa mawe huwa yanatengenezeka mwilini, kwako ni jambo la kushangaza.

 

Au labda ulishawahi sikia mawe ya kwenye figo, mawe ya kwenye mfuko wa nyongo au hata mawe ya kibofu cha mkojo na sehemu nyingine za mwilini lakini sio ya mdomoni. Sasa leo tutaongea zaidi juu ya mawe ya kwenye tezi za mate (salivary glands).

 

 

Kitaalamu, kuundwa kwa mawe ndani ya tezi za mate huitwa sialolithiasis. Hali hii inayoweza kukushangaza sana mara kadhaa huweza pelekea maumivu katika afya ya mdomo.

 

Ningependa kukufafanulia kwa kina zaidi kwani ni hali inayohitaji uangalifu na uelewa wa ziada.

 

Hali hii hutokeaje?

Sialolithiasis hutokea kutokana na kemia tata ya mate. Ndani ya mate yetu kuna madini mbalimbali ambayo, chini ya hali fulani, yanaweza kuganda na kukusanyika, na kufanya mawe.

 

Mawe haya yanaweza kuzuia mtiririko wa mate ndani ya mianya ya tezi za mate na kusababisha uvimbe, maumivu na vile vile infection ya tezi hizo.

 

Mfano halisi wa hali hii ni sawa na kujaribu kupitisha maji kwenye bomba lililoziba, hivyo kupelekea presha kujengeka ndani ya bomba (mianya ya tezi), kuvimba na maumivu.

 

Dalili…

Kutambua ishara na dalili za sialolithiasis ni muhimu ili utafute matibabu mapema. Wagonjwa wanaweza kupata maumivu makali na uvimbe kwenye maeneo ya chini ya taya, haswa wakati wa milo ambapo uzalishaji wa mate uko katika kilele chake.

 

 

Tezi iliyokumbwa inaweza kuonekana kubwa na wakati mwingine hata kuuma inapoguswa. Baada ya chakula au ukiwa mbali na chakula, uvimbe unaweza kuonekana haupo na kufifia kabisa.

 

Mbali na hapo unaweza kushindwa kumeza, kuungua mdomo, kupatwa na hali ya ukavu mdomoni (xerostomia), mate yako yanaweza kuwa mazito sana, utengenezekaji wa usaa pale ambapo infection imeikumba tezi hiyo husika.

 

Wakati sialolithiasis inaweza kuathiri watu wa umri wowote, hujitokeza sana kwa watu wazima wa umri kati ya miaka 30 mpaka 60. Pia wanaume huathiriwa na hali hii kuliko wanawake, ingawa sababu za ubaguzi huu wa kijinsia bado hazijulikani.

 

Sialolithiasis hutokea sehemu gani mdomoni?

Kinywa cha binadamu kina tezi kuu na ndogo ndogo za mate. Tezi kuu zipo tatu, nazo kitaalamu huitwa tezi ya parotid (hupatikana mbele na chini kidogo ya masikio), tezi ya sublingual (hupatikana chini ya ulimu) na tezi ya submandibular (hupatikana chini ya taya).

 

 

Tezi za submandibular, zilizoko chini ya taya, ndizo maeneo kuu ya uundaji wa mawe. Sababu ya hii ni mbili:

  1. Mianya ya tezi hii ni mireu zaidi na ina mkondo uliojikunja sana, sio wa moja kwa moja mdomoni, bali umepinda pinda sehemu kadhaa mpaka pale unapoungukia mdomoni
  2. Pia ndiyo tezi ambayo hutengeneza mate mazito na yenye madini mengi zaidi mdomoni.

 

Hizi sababu kuu mbili hupelekea mate kukaa katika miaya yake kwa muda kadhaa kabla hayajatoka kinywani hivyo kufungua njia kwa uundaji wa mawe – ikilinganishwa na mianya ya tezi za mate zingine. Kwa hivyo, mianya hii ina uwezekano mkubwa wa kuzibwa.

 

Nini kitatokea kama hali hii ikiwa kubwa?

Katika hali ya kukithiri, sialolithiasis inaweza kusababisha shida kama vile:

  • Maambukizi ya tezi
  • Kutokea kwa kikohozi
  • Uharibifu wa tezi
  • Wakati mwingine mawe haya yanaweza kuwa makubwa sana na kutokea mdomoni na kukusababishia kukwaruzika ulimi au hata izi.

 

Hali hii inatibika?

Ndio! Mbinu za matibabu kwa sialolithiasis hutofautiana kulingana na athari kwa mtu na mtu. Daktari wa Afya ya Kinywa anaweza kukuagiza kufanya vipimo vya X-ray ya kinywa au ultrasound ili aweze kuona vyema mawe hayo na kuchagua matibabu sahihi ya kukufaa wewe binafsi.

 

Unywaji wa maji mengi na kukanda tezi hiyo inaweza kukusaidia kupunguza na kusaisha mawe madogo madogo na kuondoa hali unazojisikia.

 

Walakini, kesi kali zaidi zinaweza khitaji kuingilia upasuaji kurejesha utendaji wa kawaida wa tezi au kuiondoa tezi yote kwa pamoja. Yote haya yatalingana na hali yako  binafsi.

 

Moja ya mambo muhimu ya kuzingatia ni kwamba sababu za sialolithiasis bado hazijulikani kabisa. Ingawa inakubalika kwamba mawe hutokea kutokana na mabadiliko katika kemia ya mate, sababu zinazosababisha mabadiliko haya hazijathibitishwa kikamilifu.

 

Baadhi ya sababu zinazohusishwa hujumuisha ukosefu wa kutosha wa unywaji maji, mabadiliko katika muundo wa mate, na hali zingine za kiafya kama vile mate machache yasiyo kidhi mahitaji wa mwilini au mabadiliko katika utendaji wa tezi za mate.

 

Mbali na hilo, ni muhimu kuelewa kuwa sialolithiasis inaweza kuwa dalili za hali nyingine ya kiafya. Kwa mfano, watu wenye mdomo kavu (xerostomia) au maambukizi ya mara kwa mara ya tezi za mate wanaweza kuwa katika hatari kubwa ya kuunda mawe ya mate. Vile vile, watu wenye historia ya kurithi ya hali hii wanaweza kuwa na uwezekano mkubwa wa kuathiriwa.

 

Zaidi ya hayo, ni muhimu pia kuzingatia hatua za kuzuia. Kwa mfano, kuhakikisha unywaji wa kutosha wa maji, kuzuia au kupunguza matumizi ya vitu kama vile pipi zenye sukari nyingi, au vinywaji vyenye sukari nyingi.

 

Hii ni kwa sababu vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi vinaweza kuchochea uzalishaji wa mate na kusababisha mabadiliko katika kemia ya mate, ambayo inaweza kusababisha kuundwa kwa mawe ya mate.

 

Kwa hivyo, kujaribu kudhibiti ulaji wa vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi ni hatua muhimu ya kuzuia sialolithiasis. Aidha, kula vyakula vyenye asidi vinaweza kusaidia kupunguza hatari ya kuunda mawe ya mate.

#!trpst#trp-gettext data-trpgettextoriginal=733#!trpen#1 thought on “<trp-post-container data-trp-post-id='1288'>Unafahamu mawe yanaweza kuundwa mdomoni?</trp-post-container>”#!trpst#/trp-gettext#!trpen#

#!trpst#trp-gettext data-trpgettextoriginal=11#!trpen#Leave a Comment#!trpst#/trp-gettext#!trpen#

#!trpst#trp-gettext data-trpgettextoriginal=723#!trpen#Your email address will not be published.#!trpst#/trp-gettext#!trpen# #!trpst#trp-gettext data-trpgettextoriginal=715#!trpen#Required fields are marked *#!trpst#/trp-gettext#!trpen#

en_USEN