Ni Ukweli Unywaji wa Maziwa Unaweza Kupelekea Saratani ya Kibofu kwa Wanaume?

Leo asubuhi wakati  naelekea katika pilikapilika za hapa na pale nilipata wasaa wa kuperuzi katika kundi moja la WhatsApp ambapo nilikutana na mazungumzo yanayohusu makala iliyoandikwa na BBC ambapo makala hiyo ilisema maziwa yamehusishwa na saratani ya kibofu kwa asilimia 60.

Jambo hili lilishtua hisia zangu ambapo ilinifanya nitamani kufanya utafiti kidogo kisha niandike makala ya kile nilichokutana nacho katika tafiti yangu.

Swali la kwanza nililokua nalo kichwani ni Je! Ni kweli maziwa yanaweza kusababisha saratani na kama ni kweli, kivipi?

Makala hii iliyoandikwa mwaka 2022 na BBC inazungumzia kwamba maziwa yamekua yakihusishwa na saratani ya kibofu kwa asilimia 60 tofauti na wale wasiotumia maziwa.

Unaweza ukawa unajiuliza inawezekana kweli na tukizingatia maziwa ni mojawapo ya vyakula vinavyoonyesha kuwa na virutubisho muhimu kwa ajili ya mwili.

Tafiti zinasemaje?

Shirika la tafiti za saratani nchini Uingereza liliandika makala inayohusiana na swala hili na kusema kwamba linatambua kwamba watu wengine huamini maziwa yanasababisha hali ya saratani ya tezi dume kuwa mbaya zaidi kutokana na sababu mbalimbali.

Shirika hili la kiserikali la tafiti za Saratani liliendelea kusema kwamba hakuna ushahidi wowote unaosema kwamba maziwa ndio kichochezi kikuu cha saratani za tezi dume kwa sababu saratani huchochewa na vitu mbalimbali na hivyo basi tafiti mbalimbali zinapaswa kufanyika ili kuweza kufahamu zaidi kuhusiana na hili ila kwa sasa bado sio sahihi.

Hata hivyo shirika hilo la tafiti za saratani lilizungumzia umuhimu wa maziwa katika kuepuka saratani za utumbo na kusema kwamba nchini uingereza maziwa na bidhaa zitokanazo na maziwa zimependekezwa kutumiwa mara tatu kwa siku kwa viwango ambavyo ni kama ifuatavyo:

1. Glass moja ya mls 200 ya maziwa yaliyofyonzwa mafuta (semi-skimmed milk).

2. Maziwa mtindi kiasi cha gram 150, hii ni sawa na kopo dogo la maziwa mtindi, hapa kwetu Tanzania yanaweza kuwa yanapatikana kwa bei ya TShs 1,000.

3. Size ya box la njiti ya kiberiti ndio kiasi cha jibini au cheese inayotakiwa kutumika kwa siku.

Kwa tunaojiuliza jibini ni nini?

Jibini hutumika kutengenezea vyakula mbalimbali na hasa vyakula vya kigeni kama pizza pamoja na burger ambapo watumiaji wengine hupendelea kulipa pesa zaidi ili kupata jibini zaidi katika migahawa na mahoteli mbalimbali.

Swala la kukumbuka ni kwamba vitu vyote hivi hupaswa kutumika kwa kiasi. mfano mdogo maziwa mtindi nusu lita ni kiasi ambacho unapaswa kutumia kwa muda wa siku tatu. Na pia unapaswa kutumia  maziwa lita nzima  kwa muda wa siku tano na si  chini ya hapo.

Sababu za kukusisitiza utumie maziwa na bidhaa zitokanazo na maziwa kwa kiasi kidogo ni ili uweze kuepukana na ongezeko la uzito ambalo husababisha hatari mbalimbali za kiafya.

Ni vyakula/virutubishi gani vinavyoweza kupambana na saratani?

Vyakula vinavyopaswa kuliwa ili kupambana  na saratani ni pamoja na mboga mboga za majani na matunda pamoja na vyakula vyenye vitamini A, C na E ambavyo vina antioxidant zinazopambana na kemikali zijulikanazo kama free radicals ambazo zikizidi mwilini huweza kupelekea saratani.

Vitamini hizo hupatikana kwenye mboga mboga za majani, matunda ya citrus kama vile machungwa, matunda mengine kama vile maembe, nyanya, kiwi na kadhalika.

Hata hivyo kuna  vitamini E ambayo inapatikana kwenye vyakula kama parachichi, spinachi , maboga, karanga na kadhalika.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

en_USEN