- Asilimia 80 % ya visababishi vya kiharusi vinazuhilika – American Stroke Association
- Wanawake nao watajwa.
Taarifa hii imetolewa na taasisi ya utafiti wa ugonjwa wa kiharusi nchini Marekani (American Stroke Association) katika mwongozo wao mpya wa matibabu uliotolewa September mwaka huu 2024. Mara ya mwisho taasisi hii kutoa muongozo wa matibabu ya kiharusi ni miaka 10 iliyopita, mwaka 2014.
Akiongea katika uzinduzi wa muongozo huo wa matibabu, Mwenyekiti wa mabadiliko ya muongozo huo, Dr Chery Bushnell alisema kwamba
Mwongozo huu wa matibabu ya kiharusi umekuja kama mabadiliko kwa wakati muafaka. Tangu 2014 kumekuwa na tafiti na majaribio mbalimbali yaliyofanywa kuhusu kiharusi na kuonesha kuwa matibabu ya wagonjwa wa kisukari, uzito mkubwa, shinikizo kubwa la damu, kisukari, n.k. hayapaswi kuishia tu kwenye kutoa dawa bali na kuchunguza viashiria vilivyopo vya kiharusi.
Muongozo huu mpya umeainisha mambo makuu 2 kama ifuatavyo:
Kwanza, kiharusi kinazuhilika kwa asilimia 80%. Katika ujumbe huu taasisi hiyo imewahimiza watumishi wa afya kuhakikisha wanachunguza visababishi mbalimbali vya kiharusi hasa kwa wagonjwa wa kisukari, presha, na vitambi.
Imewaasa watu wa afya kutotoa tu dawa za kutibu maradhi haya bali kuwashauri wagonjwa kuhusiana na hatari ya kiharusi na kuwaelimisha kuhusu kubadili mitindo ya maisha na lishe.
Mtindo wa maisha kama kufanya mazoezi, usingizi wa kutosha, chakula bora, kutovuta sigara na uzito mdogo.
Pili, makundi yafuatayo ya wanawake wapo kwenye hatari kubwa ya kupata kiharusi.
Muongozo huu umeainisha kwamba wanawake wanaotumia vidonge vya uzazi wa mpango, wanaopata presha wakati wa mimba, wanaotumia homoni za Oestrogen kutokana na kuingia mapema menopause au ovari zao kufeli mapema (kabla ya miaka 40), pamoja na wanaovuta sigara wako kwenye hatari zaidi ya kupata kiharusi hivyo ni muhimu sana kuangaliwa kwa ukaribu sana na kupewa matibabu yanayotakiwa.
Aidha muongozo huu unatarjiwa kuwa na mabadiliko mbalimbali yatakayokuwa na msaada mkubwa kwa wagonjwa mbalimbali.
Muongozo huu umekugusa katika kipengele gani? Niandikie maoni yako kwenye comments section.

Chief Content Officer (CCO) at Abite Afya
I’m responsible for overseeing the entire content strategy, ensuring that all published materials align with the blog’s mission, audience needs, and business goals.