Kuhusu Sisi

Maneno Machache

Kuhusu Sisi

Wazo la kuunda tovuti ya kampuni lilikuwa katika mpango wetu tangu 2021, lakini mapema mwaka huu nilikuwa na majadiliano na wafanyakazi wangu, na pamoja tuliamua kuanza na blogu.

Hitaji la kutengeneza mtandao wa bure wa kujua afya kwa ajili ya ndugu, jamaa, wateja, na jamii zetu kiujumla ndo imesabisha Abite Afya kuzaliwa. Kwa mshangao, imekuja kuwa moja ya bidhaa bora za Abite LLC.

Blogu yetu inaangazia changamoto za kiafya za kila siku zinazowakabili vijana, akina mama na baba wa Kiafrika. Tunatoa suluhisho rahisi kwa shida zinazohitaji hospitali.

Tunafanya tuwezavyo kuhamasisha mabadiliko ya tabia kwa watu kupitia machapisho rahisi na uandishi rafiki.

Dk. Ansbert Mutashobya,
Mwanzilishi na Mkurugenzi

Sisi ni Mabadiliko

Mapambano ya kupata chanzo bora cha habari za Afya yamekuwa yakiendelea kwa vizazi. Tabaka la chini – ambalo linajumuisha asilimia kubwa barani Afrika – limekuwa likitegemea hospitali kwa kila kitu.

Asilimia kubwa ya watu hawa hufanya kazi zaidi ya saa 10 kwa siku, wanalea zaidi ya watoto 2, na bado wengi wao wanaishi bila bima ya afya.

Hivyo unaweza kufikiria hasara watakayopata ikiwa wataugua kwa sababu ya kutojua elimu sahihi kama vile lishe bora.


Ndiyo maana tumeunda blogu hii. Ili kumpa kila mmoja wetu chanzo cha bure cha maelezo ya afya, ambacho tunaamini kwa njia moja au nyingine kinaweza kubadilisha maisha yako.

 

Alicia Phillbert,

Mkurugenzi.

Screenshot_20230219-114447_WhatsApp (2) (1)
Kwanini Utusome

"Tumeirahisishia afya yako."

Ratiba za kazi za kila siku zimefanya iwe vigumu kuishi maisha yenye afya. Afya katika suala la vyakula, mazoezi, ukaguzi wa mwili, na usawa wa akili. Bila kutambua, hii inaweza kuathiri vipengele vingine vya maisha yako kama vile viwango vya ubunifu, ushirikiano kwenye jamii, na uendeshaji pesa.

Kupitia blogu yetu utaweza kufanya maamuzi sahihi ya kiafya ili kudhibiti hatari ya kupata majanga ya kiafya yanayoweza kuzuilika.

Itakufanya ujisikie vizuri kimwili na kiakili. Kwa uhakika.

Makala Zote za Afya
Zimeandikwa na madaktari wetu wenye leseni.
Maamuzi yenye kina
Uelewa mzuri wa hali yako ya afya utakusaidia kufanya uamuzi sahihi wakati wowote inapobidi.
Njia iliyonyooka
Utajuaje kama unachofanya ni cha afya au la? Elimu sahihi ya afya yako.
Utulivu wa Akili
Unapokuwa na ufahamu wa hali yako ya afya, utaelewa nini unaweza kufanya ili kujiweka imara bila kujali unapitia nini.
Kuishi muda mrefu
Kinga ni bora kuliko tiba, na ndicho tunachofanya.
Waandishi Wetu

Washauri Bora

Wanapenda wanachofanya na ndio maana tunawaita 'special'.

Kuna ukweli usiojulikana kuhusu waandishi wetu: wote ni madaktari na manesi katika hospitali mbalimbali. Wana majukumu mengine, lakini bado huchukua muda kuandaa maneno 800+ kwa makala moja.

Blogu hii inawakilisha shauku na ndoto zao za kuandika. Mapenzi yao ya kusema ukweli (ambayo huwezi kuambiwa hospitalini). Mapenzi yao kwa afya ya wengi katika jamii.

Maneno yetu yana nguvu. Maneno yako yana nguvu. Pamoja tuwe sehemu ya kitu hiki kikubwa – Abite Afya – kwa familia zetu, wapendwa wetu, na muhimu zaidi kwa nchi yetu.

0
Kategori za Blogu
0 +
Waandishi & Watunzi
0 +
Masaa Tuliyosomwa
0 +
Miaka ya Uzoefu
swSW