Nimetumia neno nyaya kwani ndivyo wengi huita vifaa hivi vya kurekebisha mpangilio wa meno yaani orthodontic braces. Inawezekana hata wewe ulishawahi kuziita nyaya za meno au ukadhani kuwa ni urembo wa mdomoni. Wengine huenda mbali hadi kuziita senyenge za mdomoni na majina mengine kadha wa kadha.
”Mh! Hizo nyaya umeweka huko mdomoni ni za nini? Au ndo urembo maana nyie wadada siku hizi!” Haya maneno yalinenwa na Uncle wangu baada ya kuviona vifaa hivi mdomoni mwangu.
Inawezekana si yeye tu, bali hata wewe pia una mawazo sambamba na Uncle wangu. Endelea kusoma makala hii hadi mwisho ili ujue vitu hivi ni nini na vina maana gani katika kinywa chako.
Kwa lugha rahisi, Orthodontic braces – vifaa vya kubadili mpangilio wa meno – ni zana zinazotumiwa na madaktari wa meno kusawazisha meno yako na kuleta mpangilio sawa na unaofaa. Lakini pia kuweka mstari mzuri ili kukusaidia kung’ata vyema.
Huu si urembo bali ni matibabu ya meno kama ilivyo kung’oa au kuziba meno. Mpangilio mzuri wa meno hukusaidia kuepukana na kuoza kwa meno, magonjwa ya fizi, kukuwezesha kung’ata vyema na kuongeza ujasiri wakati wa kucheka au kuongea na wengine.
Ni nani anastahili kupata matibabu haya?
- Zana hizi hupendekezwa katika hali tofauti tofauti kama vile katika meno yaliyopinda (misaligned or crooked teeth) au/na meno yaliyobana sana (overcrowded teeth).
- Hutumika kuondoa au kufunga nafasi katikati ya meno (teeth gaps). Ikiwa meno yako ya juu yanashikana sana na meno ya chini kwa mbele au meno yako ya juu yanashinikiza sana mbele (underbite/overbite).
- Vilevile ukiwa unapata shida ya kung’ata vyema ikiwa meno yako ya mbele hayakutani (open bite).
- Vifaa vya kurekebisha mpangilio wa meno hutumika pale ambapo jino halijajitokeza mdomoni mara nyingi jino liitwalo canine (impacted tooth) hii inaweza kupelekea kushindwa kung’ata vizuri au afya na mpangilio mbaya wa meno mengine.
- Vile vile, hizi zana huweza kutumika kuondoa mwanya yaani diastema kwa mtu asiyependa kuwa nao.
Lakini kikubwa kinachobidi kuambatana na haya ni wewe mwenyewe kutaka kufanya matibabu haya, yaani kuwa na motisha ya kutosha ya kuanza na kumaliza matibabu.
Naweza kupata matibabu haya kama nina changamoto nyingine za kiafya?
Mbali na hawa wanaostahili kupata matibabu haya, ni lazima kabla hujawekewa vifaa hivi, daktari wako wa meno akuchunguze kwa kina na kukupa ushauri wa jinsi ya kufanya mpangilio wa meno kulingana na afya yako kiujumla.
Kama una magonjwa ya muda mrefu kama vile kisukari ambacho hakijadhibitiwa, magonjwa ya akili, ugonjwa wa hemophilia, au kama hutunzi kinywa vizuri au una magonjwa ya fizi, au una utapiamlo au kama una motisha ndogo ya kufanya matibabu. Uwepo wa hali hizi unaweza kusababisha athari kwenye kinywa chako zaidi ya kukusaidia.
Kama sukari yako iko juu na haijazibitiwa basi matibabu haya yanaweza kupelekea magonjwa ya fizi.
Uwepo wa magonjwa ya akili husababisha ugumu katika kupata ushirikiano wako katika matibabu hivyo hayatafanyika vizuri.
Kama matibabu yatahitaji kung’olewa kwa meno – na wewe ni mgonjwa wa hemophilia – basi damu nyingi zinaweza kutoka.
Kama hutunzi kinywa chako vyema itapelekea uchafu kujazana kinywani na kusababisha kuoza kwa meno na magonjwa ya fizi.
Motisha ndogo itakufanya kushindwa kustahimili matibabu kamili na kupelekea kuachia njiani na kutopata matokeo chanya.
Kuwa na utapiamlo hupelekea kukosekana kwa madini yanayohitajika katika ukuaji wa taya (kwa mtoto) lakini pia katika kusogeza meno ili kutengeneza mpangilio mzuri.
Aina za braces
Vifaa hivi vipo vya aina tofauti tofauti na utahudumiwa kutokana na mahitaji yako na matamanio ya muonekano wako mdomoni.
1. Braces za kawaida (Metallic braces)
Hizi ni braces za chuma ambazo unaweza kuziona mara nyingi kwa watu wengi. Zinaundwa na brackets za chuma pamoja na waya.
2. Braces za Seramiki (Ceramic braces)
Hizi hufanana na braces za aina ya kwanza lakini zinamuonekano sawa na wa meno hivyo huwa hazionekani sana mtu akiwa nazo kinywani.
3. Braces za ndani (Lingual braces)
Hizi zinafanana na aina ya kwanza ila zenyewe huwekwa kwenye sehemu ya ndani ya meno.
4. Braces za kujiloki (Self-ligating braces)
Hizi pia ni kama za kwanza lakini zenyewe hutofautiana na braces za kawaida kwa jinsi zinavyoshikilia waya na namna yake ya kurekebisha meno.
5. Braces zisizoonekana (Invisible aligners)
Hizi ni vipande vya plastiki wazi, ambavyo vimeundwa kwa matumizi binafsi – kulingana na mahitaji ya mtu – na unaweza kuziondoa wakati wa kula au kusafisha meno.
6. Functional braces
Aina nyingine ambayo huonekana sana kwa watoto ambao bado taya zao zinakuwa ni aina iitwayo functional braces. Hizi huwekwa kwa mtoto ili kusaidia kurekebisha upungufu unaonekana katika taya zinazoshikilia meno yake na hata kupelekea muonekana mbaya wa uso (dentofacial discrepancies).
Hizi functional brace zinaweza kuundwa kwa namna mbili, ya kuvaa na kuvua wakati wa kula au kusaisha kinywa au katika muundo wa kuvaliwa moja kwa moja bila kuvuliwa mpaka mwisho wa matibabu.
Sababu za mapungufu ya taya kwa mtoto hutokea aidha kwa tabia za utotoni kama vile kunyonya vidole, kusukuma meno na ulimi, kung’ata ng’ata peni au penseli, na kupumulia mdomo.
Ni vyema kufanya uchunguzi mapema, kwa daktari wa meno, kwa mtoto kuanzia umri wa miaka 6 ili kujua kama anahitaji matibabu haya. Hii itamsaidia mtoto wako kuepuka matatizo ya baadae kama kushindwa kung’ata vizuri au mpangilio mbovu wa meno.
Umri sahihi wa kuweka braces
Braces huvalishwa mtu yeyote kwanzia umri wa miaka 10 mpaka 13 na kuendelea kulingana na ukuaji wake.
Hizi braces huwekwa ikiwa meno yako ya utotoni yametoka, na ya ukubwa yamekwishamaliza kutokeza.
Ni vyema kuanza kufanya matibabu haya mapema (teenage years, 13-18) kwani ndipo ufanisi na mabadiliko huweza kuonekana na kupatikana kwa haraka zaidi, kwani taya lako na meno yako yanakuwa bado katika ukuaji.
Lakini hii isikukatishe tamaa kwani matibabu haya hufanyika katika umri wowote na mpangilio wa meno yako kukaa sawa sawa.
Dhana potofu kuhusu braces
1. Braces ni kwaajili ya watoto na vijana tu.
Ukweli: Watu wazima pia wanaweza kupata braces! Hujachelewa kuboresha tabasamu lako.
2. Braces husababisha maumivu makali mno.
Ukweli: Maumivu huwapo mwanzoni lakini yanadhibitika ndani ya muda mfupi sana.
3. Braces hutumia muda mrefu kufanya mpangilio.
Ukweli: Muda wa matibabu hutofautiana kutokana na mahitaji ya mgonjwa, lakini kwa kawaida muda wa matibabu huwa ndani ya miezi 18 mpaka 24, ila kama daktari wako amekuchunguza na kujua kuwa matibabu yako yanahitaji muda zaidi, basi unaweza kukaa nazo hadi miaka 3.
4. Braces husababisha muonekano mbaya.
Ukweli: Kutokana na maendeleo mbalimbali katika tiba ya afya na kinywa, mtu anaweza kufanya uchaguzi wa muonekano wa braces ambazo angependa kutumia.
5. Braces ni kwaajili ya kuongeza uzuri tu
Ukweli: Ingawa uzuri ni faida kubwa ya matibabu haya, braces pia hufanya kazi ya kuboresha afya ya kinywa na utendaji wake kama vile kukuwezesha kung’ata vyema.
Mwisho
Mtaalamu wa kinywa na meno afanyae matibabu haya huitwa Orthodontist. Ni muhimu kuhakikisha kuwa daktari anayekufanyia matibabu haya amekidhi vigezo vya kufanya matibabu haya ili kuepusha athari kama mpangilio mbovu zaidi ya awali, meno kurudi hali yake baada ya kumaliza matibabu, kukatika au maumivu makali ya meno, na kupoteza muda na fedha.

“For the love of words”
Very informative and engaging. The author was very relatable.
Thank you
Elimu nzuri, watu wanapaswa kujua..
Haswaaaa umesema vyema
Thanks for the enlightenment
Karibu sana. Tuendelee kujifunza pamoja
Thank you for a very educative information
You are warmly welcome. Let’s continue learning together
Hongera na asante Kwa elimu nzuuri mungu akubariki na iendelee kutuelimisha
Asante kwa kutenga muda kusoma nakala hii. I hope tutaendelea kujifunza pamoja
Thank you so much for this informative education you have provided, It will be of help to many.
Karibu sana Mary. I am glad umepata nafasi ya kujifunza zaidi
Karibu sana Mary. I am glad umepata nafasi ya kujifunza zaidi
Leo nimeelimika vya kutosha, nami nilikua najua ni urembo tu. Nina maswali haya dakitari, je ni wapi “hospitali ” naweza nikapata huduma hii na huchukua muda gani? Na pia, kuna athari ambazo zinaweza kujitokeza wakati wa kutumia nyaya za meno?
Unapata huduma hii katika kliniki ya afya ya kinyuwa na meno yaani dental clinic. Dental clinic ipo katika hospitali zetu kubwa za rufaa au unaweza kwenda private pia. Braces huvaliwa kwa muda wa miezi 18 mpka 24 lakini ikiwa daktari kakuchunguza akaona unahitaji muda zaidi wa matibabu basi wengine huenda mpka miaka 3. Athari za kutumia nyaya hizi huweza kutokea kama wewe binafsi haupo tayari kufanya matibabu mpka mwisho au pale ambapo daktari anayekutibia hana vigezo vya kufanya matibabu hayo. Athari ni kama mpangilio mbaya wa meno zaidi ya awali, maumivu makali au meno kurudia hali yake hata baada ya kumaliza matibabu hivyo mtu kupoteza pesa na muda.
Leo nimeelimika vya kutosha, nami nilikua najua ni urembo tu. Nina maswali haya dakitari, je ni wapi “hospitali “naweza nikapata huduma hii na huchukua muda gani? Na pia kuna athari ambazo zinaweza kujitokeza wakati wa kutumia nyaya hizo?
Thanks i learned something new today
Gharama yake ni kiasi Gani
0682099659