Essie’s Products: Viungo Bora vya Kupikia Chakula

Nani yuko nyuma ya bidhaa za vyakula za Essie’s?

Kwa majina naitwa Ester Mndeme. Mimi ni mtoto wa kwanza katika familia yenye watoto watatu.

 

Baba yangu ni fundi seremala aliyejitahidi sana katika kazi za mikono na kufanikiwa kutusomesha mpaka tukafika elimu za juu. Hio ilikuwa ni ndoto yake ambayo ameifanikisha. 

 

Kitaaluma, mimi ni Afisa Lishe na mwandishi wa makala za lishe na uzito hapa Abite Afya.

 

Unaisi ulijifunzia wapi kupenda kazi za mikono?

Juhudi ya kazi nimejifunza kupitia kwa wazazi wangu, Baba alianza na randa za mkono mpaka kufikia kununua mashine baada ya miaka mingi na teknolojia kukua.

 

Alikua kijana mwenye wazazi wakulima kama familia nyingi za kitanzania, alitokea katika milima ya kusini ya Pare ambapo kunalimwa vitu mbalimbali ikiwemo tangawizi.

 

Mahusianao yako na mapishi yalianzia wapi?

Mapenzi yangu na kupika, yalianza shule ya msingi katika vipindi vya somo la stadi za kazi, Waalimu walitufundisha kupika na kutengeneza vyakula mbalimbali na tulipeleka ujuzi huo nyumban.

 

Mfano ninaoukumbuka sana ni  saladi ya matunda ambayo nilijifunza kutengeneza nikiwa darasa la tatu.

 

Penzi la kupendelea kupika liliendelea nilipokua shule ya Sekondari Ashira iliyopo Marangu – Kilimanjaro, ambapo nililichukua somo la upishi (ambalo tulipaswa kuchagua tunapofika kidato cha tatu). 

 

Hapa tulipaswa kuchagua kati ya upishi na ushonaji. Nilipenda sana kupika tangu nilipokuwa mdogo hivyo nilichagua kupika. Maisha yangu ya shule za bweni ndio yalionisaidia kufahamu stadi mbalimbali za maisha ikiwemo kupika.

 

Mimi na wanafunzi wenzangu tulifundishwa uandaaji wa vyakula mbalimbali katika somo lililokua linaitwa “cookery”.

 

Mapenzi yangu na mapishi yalishamiri sana na nilikuwa nikifurahia sana vipindi hivi kwa sababu, tulipata fursa za kujifunza aina mbalimbali za mapishi kutoka sehemu mbalimbali duniani na kujifunza namna ya kujipatia kipato kutokana na vyakula hivi ambavyo tulizalisha katika siku za jumamosi na kuuza kwa wanafunzi wenzetu ili kupata pesa za kununulia vyakula na mahitaji mbalimbali ya kujifunzia.

 

 

Binafsi, mimi ni mpenzi wa kupika na katika maisha yangu ya kila siku kwenye utengenezaji chakula, viungo kama vitunguu saumu na tangawizi vimekua sehemu ya mapishi yangu japo uandaaji wake huhitaji muda kidogo na sio wa urahisi sana.

 

Tamanio la kutengeneza bidhaa lilianzia hapa. Nilikua natamani kutengeneza bidhaa mbalimbali zinazokua na manufaa katika mwili wa binadamu na pia kunipatia kipato.

 

Mpaka hivi sasa nina bidhaa kuu aina 3 ambazo ni cooking pastes, hizi hutumika katika kuungia vyakula kabla ya kupika, meal prepping. Mfano, samaki au nyama inayotakiwa kuokwa huhitaji masaa katika viungo ili kuleta ladha inayopendeza sana na ya kufurahiwa. 

 

 

 

Vile vile cooking pastes hizi hutumika katika kuunga vyakula pale vinapokua vinapikwa. Mfano katika utayarishaji wa mboga za mchuzi na katika vyakula vya mchemsho na hata vyakula vya watoto kuanzia miezi sita na kuendelea. Hio ndio kazi kubwa ya Essie’s cooking pastes.

 

Jinsi gani unaweza kutunza bidhaa wakati wa kutumia na je zinadumu kwa muda gani?

Bidhaa zetu zinaweza kutumika kwa kipindi cha mwaka mzima pindi unaponunua bidhaa yetu na utunzaji huhusisha kuiweka ndani ya fridge mara tu unapomaliza kuitumia na pale unapohijati kutumia unapaswa kutumia kijiko kisafi katika kuichota.

 

Ni faida gani unazipata unaponunua bidhaa zetu?

Bidhaa zetu zina faida mbalimbali ikiwemo kurahisisha matumizi kwani unachota kiasi cha cooking paste na kuhifadhi nyingine kwa matumizi ya baadae hivyo kuokoa muda hasa kwa watu wenye shughuli mbalimbali.

 

Pia husaidia kuongeza ladha ya vyakula kwa watoto na watu wazima. Lakini pia kuna faida mbalimbali za vitunguu saumu pamoja na tangawizi mwilini ambapo tafiti mbalimbali zimeonyesha faida za kitunguu saumu na tangawizi katika kuimarisha afya ya mfumo mzima wa chakula na faida nyingine nyingi.

 

Kama utahitaji bidhaa hizi, njia pekee ya kuzipata ni kwa kupiga namba hii (au kutuma ujumbe kwa njia ya WhatsApp): +255 756 454 391

2 thoughts on “Essie’s Products: Viungo Bora vya Kupikia Chakula”

Leave a Comment

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

swSW