Maumivu ya kisigino na unyayo (plantar pain) ni moja ya changamoto kubwa katika jamii. Tatizo hili lipo sana kwa wanamichezo na wanawake wenye uzito mwingi na vitambi.
Husababishwa na nini?
1. Plantar Fasciitis
Hii ni hali ya utando wa chini wa sole ya mguu, fascia (utando mweupe ambao huunganisha kati ya kisigino na vidole), kuvimba na kuwa na maumivu hivyo kisigino na sehemu nyingi ya unyayo kuuma.
Inaweza kuwa maumivu kwenye kisigino tu au kusambaa mpaka sole nzima ya mguu wako.
Hii husababishwa na presha kubwa inayowekwa mguuni kutokana na kutumia miguu kupita kiasi mfano wachezaji wa mchezo kama kuruka, kukimbia au kutembea na miguu tupu au kuvaa viatu vyenye sole mbaya inayokandamiza miguu hasa katikati na kisigino.
Maumivu haya huwa kama mguu unawaka moto na isipotibiwa vizuri huwa kikwazo na kuharibu furaha kwa sababu ya miguu kuwaka moto na kuuma sana.
Watu wenye mguu flat pia wako kwenye hatari ya kupata tatizo hili.
2. Calcaneal Spurs
Hiki ni kimfupa ambacho huota kwenye kisigino; husababisha maumivu ya kuchoma hasa mtu akiwa anatembea, unaweza kuisi kama unachomwa na mwiba kwa ndani.
Hali hii ni maarufu zaidi kwa wanawake wanene na wenye vitambi. Chanzo chake hakijulikani ila inaweza kutokana na matumizi ya viatu vyenye visigino virefu hivyo kuweka presha kubwa kwenye kisigino.
Sababu zingine ni uzito uliopitiliza, asilimia 70% ya watu wenye tatizo hili ni wanene.
Maumivu haya yanatibikaje?
1. Dawa
Madakatari hutoa dawa za maumivu na steroids kuondoa uvimbe. Kwa baadhi, maumivu huondoka na kupona kabisa lakini asilimia kama 55% maumivu haya huwa hayasikiii dawa; na huja na kuondoka kila baada ya muda fulani.
2. Upasuaji
Tatizo la calcaneal spurs (kifupa kwenye kisigino) linaweza kuwa sugu na kuhitaji upasuaji ili kukiondoa.
3. Huduma ya vifaa tiba
Matumizi ya sole na visigino maalum vya kuchomeka kwenye kiatu vimekuwa na msaada mkubwa sana hasa kwa wale wagonjwa wa muda mrefu.
Sole na visigino hivi huwa na material ya Nta hivyo husaidia kuzuia maumivu kwa kupunguza makutano ya moja kwa moja kati ya kiatu na mguu.
Vifaa tiba hivi vimeleta nafuu sana kwa watu wengi.
Hali hii inazuilika?
Ndio! Kwa kuvaa viatu veye sole laini, kupunguza uzito kuwa wa kawaida.
Kama una kazi inayokulazimisha kusimama, kutembea au kukimbia muda mrefu unashauriwa kuvaa sole au visigino maalum kwa ajili ya kujikinga na changamoto ya unyayo kuvimba na kuuma.
Vifaa tiba kama Heel Protector na Foot Insole ambazo zina material ya Nta vitafaa kwa ajili ya kulinda miguu yako na hatari hii.
Utavipata wapi vifaa hivi?
Sio pengine zaidi ya Abite Nyumbani. Duka maalum kwa ajili vya vifaa tiba vya physiotherapy na rehabilitation.
Duka linapatikana Sinza Mori, jengo la Azaria Plaza (Ofisi Na. 14), Opposite na Kitambaa Cheupe Sinza.
Wasiliana nasi kupitia 0765 226 702 kwa maelezo zaidi. Usisahau pia kutembelea kurasa yetu ya Instagram kwa taarifa kamili kuhusu aina mbalimbali za vifaa tiba vyetu.

Chief Content Officer (CCO) at Abite Afya
I’m responsible for overseeing the entire content strategy, ensuring that all published materials align with the blog’s mission, audience needs, and business goals.