Tumbo Kukereketa/Kuvimbiwa: Visababishi na Vyakula vya Kutumia

“Hivi punde nimekua nikijisikia hali ya tumbo kujaa gesi na hali hii inaponikuta huwa napoteza hamu ya kula kwa sababu najisikia kua nimeshiba wakati wote . Na pia ninafikiria namna utumbo unaweza kuwa na mabaki ya chakula kinachokua kimemeng’enywa na kusababisha hali ya gesi tumboni.”  

 

Nini hutokea hadi kusababisha hali ya tumbo kujaa au kukereketa?  

Katika mazingira ya kawaida watu wengi tunakua katika maeneo ya mbali na nyumbani hasa mida ya asubuhi na mchana hivyo kusababisha kula vyakula ambavyo vimeandaliwa katika migahawa.

 

Na asilimia kubwa ya vyakula hivyo tunavyokula huwa hatufahamu namna vilivyoandaliwa na hatuna uwezo wa kupata vipimo vya chakula tunavyovihitaji.  

 

Unapokua umekula chakula kitakachokusababishia tumbo kukereketa na kujaa gesi na kupelekea kusikia hali ya kukaza kwa tumbo, fahamu kinachotokea ni kwamba: 

 

Chakula hichi kinakua kinavuta maji na kwenda kusababisha hali ya kuchacha (fermentation) kwa chakula ndani ya tumbo baada ya wadudu wa kawaida wakaao ndani ya tumbo (normal flora) kula chakula kile na kutoa gesi kama mabaki. 

 

Hivyo kunakua na hali ya chakula kukwama katika safari ya umeng’enywaji ambayo hupelekea kujisikia hali ya tumbo kujaa – ambapo wengi wetu tunaiita kuvimbiwa tumbo, hali ya kuharisha kusikotarajiwa au hata kukosa choo, kupata vichomi na kukosa hamu ya kula. 

 

Hizo zote ni mifano ya dalili za kukereketa kwa tumbo. 

 

Visababishi vyenyewe sasa: 

  • Vyakula vyenye mafuta mengi 
  • Bidhaa zenye maziwa, hasa kwa watu wenye hali inayojulikana kama lactose intolerance kwani tumbo linashindwa kuvumilia ile lactose iliyoko katika maziwa. 
  • Ulaji wa kabeji mfano zile zinazopatikana katika vibanda vya chipsi, ulaji huu wa kabeji umehusishwa na uwepo wa fibers (nyuzi nyuzi) nyingi ambazo zikiliwa kwa wingi huweza kupelekea kukereketwa kwa tumbo kwasababu maji huvutwa na kusababisha kuchacha baada ya wadudu wa kawaida wanaopatikana katika tumbo kula chakula kile.  
  • Unywaji wa pombe hasa beer kwasababu inakua imechachushwa na inapofika tumboni huweza kusababisha hali ya kujaa gesi. 

 

 “Nifanye nini sasa?” 

Hili ni swali ambalo litakua linafuata mara baada ya kujikuta na hali hii hivyo ili kuweza kupata unafuu, tutaangalia mambo yanayoweza kufanyika pamoja na baadhi ya vyakula  ambavyo vinaweza kuvumilika katika hali ya kukereketwa kwa tumbo. 

 

Vifuatavyo ni vyakula vinavyosaidia kuondoka kwa hali ya kukereketwa kwa tumbo: 

  • Strawberry – kwasababu zina nyuzi nyuzi, maji pamoja na potassium ambayo husaidia katika usogezwaji wa chakula katika utumbo.  
  • Mbegu za uwatu (Fenugreek) 
  • Blueberries 
  • Machungwa – kwa sababu yana nyuzi nyuzi pamoja na maji yanayoweza kusaidia msukumo wa chakula ndani ya tumbo. 
  • Unywaji wa chai yenye tangawizi  
  • Unywaji wa chai ya chamomile 

Jambo lingine la kufanya ni kutembea ili kuwezesha usogezwaji wa vyakula katika mfumo wa chakula. 

 

Vipi kuhusu Probiotics?

Katika nchi zilizoendelea kuna upatikanaji mkubwa wa vyakula pamoja na vidonge vya virutubishi vyenye kitu kiitwacho probiotics ambao ni bakteria walio na uswahiba na utumbo kwa kuufanya utumbo usikerekeye kutokana na vyakula ambavyo husababisha kukereketa kwa tumbo (irritable bowel syndrome). 

 

Hapa nchini kwetu Tanzania, sio mara nyingi unaweza kukutana na vinywaji vinavyokua na probiotics, walakini vinakuwepo kwa uchache hasa katika supermarkets kubwa.

 

Unaweza kukutana na vinywaji kama kombucha ambavyo hivi karibuni vimeongezwa katika maduka mengi ya shopping ya vyakula na maduka makubwa ya dawa ambapo utakuta wanauza supplements zenye probiotics.  

 

Mwisho kabisa ni muhimu kuepuka ulaji wa baadhi ya vyakula vinavyoweza kukupelekea kukereketwa kwa tumbo. Na pia kuzingatia hali ya usafi katika utayarishaji wa vyakula. 

Leave a Comment

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

swSW