Aina 2 za juisi zitakazoimarisha uwezo wako wa kuona

Katika vipindi mbalimbali vya maisha ya binaadamu kumekua na mafundisho mbalimbali ambayo tunapata na leo katika makala hii nitaongelea namna ambavyo lishe, hasahasa juisi, inasaidia katika swala la uono au kuona (eyesight).

 

Tulivyokua watoto, wengi wetu, tulikua tunakazaniwa kula mboga za majani kwa msisitizo kwamba zinasaidia katika kuona vizuri.

 

Kupitia makala hii utaelewa, kitaalamu, kwanini mama yako alikua anakusumbua kula matembele au spinachi muda wa msosi; na ningependa nianze kwa kusema sio tu mboga za majani, mboga zote husaidia katika kuongeza uwezo wa macho kwenye kuona vizuri.

 

Rangi za mbogamboga ni antioxidant zenye nguvu zinazokinga retina ya jicho na kuboresha muono.

 

Je! Retina ni nini?

Retina ni tabaka nyeti ya jicho ambayo ni kihisio cha muono cha kibiolojia kinachobadili miali ya mwanga kuwa katika mkondo wa umeme na kusababisha kuona.

 

eye retina

 

Kwenye retina kuna seli nyeti zinazojulikana kama koni na rodi; seli hizi zinahitaji rangi za mbogamboga ili kuzaliana zenyewe na kudumisha muono.

 

Muhimu: Uhitaji huu wa rangi za mbogamboga ndio sababu kubwa unashauriwa kupika mboga zako kwa muda mfupi na zisiwe na mabadiliko yanayopelekea kuharibu rangi hii kutokana na moto mkali wa jiko lako.

 

Unapoipika mboga yako kwa muda mrefu utasababisha hali ya uharibifu kutokea katika rangi za mboga na kupelekea kukosa virutubishi hivi muhimu kwa ajili ya afya ya macho yako.

 

Leo nitakufundisha aina mbili za juisi zitakasokusaidia katika kuongeza uwezo wa macho yako kwenye kuona.

 

Aina ya kwanza ningependa kuiita juisi ya karoti. Juisi hii ina virutubishi vitatu muhimu vifuatavyo:

  1. Beta Karotine ambayo inapatikana katika karoti; huwa na rangi ya machungwa.
  2. Lutein kutoka katika spinachi. Hupelekea kupatikana kwa rangi ya njano.
  3. Kirutubishi cha Anthocyanin kutoka kwenye blueberries zenye rangi ya bluu

 

Kutokana na virutubishi vinavyopatikana katika juisi hii, faida zifuatazo hupatikana kwa mnywaji:

  1. Huongeza muono mzuri
  2. Huboresha mtazamo wa rangi
  3. Hupunguza uchovu wa kuona baada ya miale ya mwanga hasa kwa wale wanaoishi katika maeneo yenye jua kali.
  4. Inaboresha kukabiliana na giza kwa maana ya uwezo mkubwa wa kuona gizani.
  5. Hulinda seli ya retina dhidi ya kuzorota.

Usilolijua: Makala mbalimbali zinaelezea seli hii ya retina kuwa sababu kubwa ya kukosa kuona katika nchi nyingi, hasi zile zilizoendelea.

  1. Kuzuia saratani kwani hizi antioxidant hupambana na radikali huru ambazo zinakuwepo mwilini na kupelekea kupatikana kwa saratani mwilini.

 

Namna ya kutengeneza juisi hii ni kama ifuatavyo:

Viungo vinavyohitajika

  • Vikombe 4 vya spinachi (baby spinach); kiasi cha gramu 30 kila kimoja.
  • Karoti 5 za size ya kati
  • Kikombe kimoja cha juice ya blueberries. Hii inapatikana baada ya kusaga blueberries mpaka utakapopata juisi yake.

 

Maandalizi

  1. Weka spinachi na karoti kwenye blender yako
  2. Ongeza juisi ya blueberries na changanya. Kama juisi haipo tengeneza smoothie kwa kikombe kimoja cha juisi ya blueberries.
  3. Unaweza weka kijiko kidogo cha sukari kwa ajili ya ladha.
  4. Tumia kwa milo mitatu.

 

Unywaji wa juisi hii ya spinachi, karoti pamoja na blueberries hupelekea upatikanaji wa virutubishi na madini mbalimbali kama vile Vitamini K, Vitamin A, Vitamin C , Vitamin E, Vitamin B2, Vitamin B6 , Folate, madini ya potassium, magnesium, calcium pamoja na zinc.

 

Kuzorota kwa seli za retina

Njia pekee ya kuzuia kuzorota kwa seli za retina yako ni kupitia virutubishi na madini mbalimbali kama vile vitamini, karotenoidi, antioxidants pamoja na zinki. Virutubishi hivi pia huboresha muono wa macho na kupelekea muono wa kipekee.

 

Waandishi wengine huuita muono wa tai (Eagle) kwa kuufananisha na uwezo wa macho ya tai. Ndege huyu huwa na uwezo wa kuona unaomuwezesha kupambanua wanyama wadogo wadogo kutoka umbali mkubwa mpaka wa kilometa moja.

 

Wewe na mimi hatuwezi kuwa kama tai, lakini tunaweza kuboresha uwezo wa macho yetu hadi kufikia umri mkubwa kwa kutumia juisi hii ya Embe-Chungwa yenye virutubishi vinavyozuia kuzorota kwa seli za retina.

 

Katika sharubati (juice) hii utahitaji embe, machungwa, spinachi pamoja na mbegu za ufuta – ambazo ni chanzo kikubwa cha madini ya zinc. Madini ambayo yanapatikana sana katika macho.

 

Namna ya kutengeneza

Viungo

  • Embe 1
  • Kikombe kimoja cha spinachi (gramu 30)
  • Kijiko kimoja cha chakula cha ufuta (gramu 15)
  • Kikombe kimoja cha juisi ya machungwa (mls 250)

 

Namna ya kuandaa

  1. Weka spinachi yako, ufuta pamoja na juice ya chungwa usage kwa pamoja mpaka vichanganyike vizuri
  2. Ongeza na embe lako moja lililotolewa vizuri kisha usage kwa pamoja mpaka mchanganyiko wako utakapokua laini.
  3. Unaweza kuweka kijiko kidogo cha sukari kwa ajili ya ladha.
  4. Tumia kwa milo mitatu.

 

Juisi hizi 2 zitahakikisha unapata virutubishi vyote kwa sababu hakutakua na mchakato wa upikaji ambao kwa kiasi fulani, kwa sababu moto unatumika, hutengeneza hali ya kuua virutubishi muhimu kwenye chakula.

 

Asante sana kwa kusoma makala hii hadi mwisho, endelea kufuatilia makala zangu zinazotoka kila wiki.

 

Kama ungependa kupata ushauri au utaratibu kamili kuhusu vyakula vitakavyokusaidia kupambana na hali au changamoto yako, usisite kufanya booking HAPA ili uweze kuongeza na mimi.

Leave a Comment

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

swSW