Msaada wa Afya nyumbani unaweza kuwa swala geni hasa katika mazingira yetu ya kiafrika ukizingatia maisha na uchumi wa nchi zetu kiujumla. Huduma hizi huwa ni kawaida kwa wazungu na baadhi ya waafrika walioendelea na ni moja ya tofauti kubwa kati yetu na wao.
Ulishawahi kufanyiwa delivery ya vitu au vifaa ulivyoagiza mtandaoni? Huwa unajiskiaje ukipokea? Muda na pesa uliookoa, usumbufu wa foleni barabarani n.k. Hakika kupata huduma nyumbani kuna namna inakupa furaha na uhuru.
Binafsi mara ya kwanza kupata huduma nyumbani ilikua niliponunua TV mtandaoni kutoka Kariakoo. Basi wakati nimekaa nyumbani sina hili wala lile nikaskia honi nje na kutoka nikaona vijana wanashusha TV yangu.
Wakaileta mpaka ndani na wakanifungia ukutani. Nilifurahi sana ukizingatia muda niliouokoa kwenda Kariakoo na risk ya kupoteza pesa kusafirisha TV kwenye Bajaji mpaka Kibaha. Ilikuwa experience nzuri sana.
Sasa unajua kwamba unaweza pia kupata delivery ya huduma ya afya nyumbani kwako? Ndio, watu wa Afya wanakuletea huduma unayoihitaji nyumbani kwako na kwa muda wako unaoupanga.
“Faragha, muda, pesa…”
Kupitia utoaji wa huduma mbalimbali za afya, nilifanya uchunguzi na kugundua kwamba baadhi ya maradhi sugu kama magonjwa ya lishe, saikolojia na akili ni ngumu kutibika na ni miongoni mwa magonjwa ambayo wagonjwa wake huwa hawaponi vizuri.
Sababu ni ugumu katika maudhurio ya kliniki. Wagonjwa hawa huwa hawapendi kusubiria muda mrefu kumuona Daktari; na pia huwa hawapendi kuonwa na watu wengine wakiwa katika hali zao kama kukonda, msongo wa mawazo, au matatizo ya akili.
Sababu hii hufanya waanze kukwepa kuja hospitali kuonwa tena na hivyo hubaki nyumbani bila kuonwa muda mrefu (na daktari) na mwisho wake afya zao zinakuwa mbaya.
Wakati mwingine ndugu, kwa sababu ya majukumu, husahau kuwaleta hospitali au huwakwepa kwasababu ya hali zao za ukorofi na usumbufu wa kuwapeleka kliniki.
Watu hawa wakifuatwa na kuonwa nyumbani, inakuwa kazi rahisi kuwasaidia kumeza dawa na ufatiliaji wa mapema.
Hizi ni faida ambazo mgonjwa anazipata akipewa huduma aya afya nyumbani:
1. Kuonwa muda wowote katika mazingira anayopenda mgonjwa au ndugu wa mgonjwa
Mfano wagonjwa wengi akili huwa hawapendi kuonekana adharani hivyo wanapoonwa nyumbani, kwa vipindi tofauti, huwasaidia kukaa muda mrefu bila maradhi ya akili kutokea au kujirudia.
Hii pia humsaidia mtoa huduma kuona uhalisia wa mazingira ya mgonjwa, watu waliomzunguka na kuweza kutoa ushauri au tiba inayoendana na uhalisia.
Mazingira ya hospitali au clinic huwa muda mwingine ni magumu kwa mhudumu wa afya kufahamu na kutoa ushauri wa kutosha kwasababu wagonjwa ni wengi.
2. Kupunguza usumbufu wa kwenda hospitali au kuhudhuria clinic
Mgonjwa anapoonwa nyumbani ni rahisi Afya yake kukaa sawa. Hakuna jambo linalowakera wagonjwa, mfano wa akili au tatizo la saikolojia, kusafiri umbali mrefu kwenda hospitali.
Wakipatiwa huduma hii nyumbani basi inakuwa ahueni. Kuogopa foleni hospitali ni moja ya changamoto inayofanya wagonjwa wa magonjwa sugu kukwepa kurudi kliniki.
3. Kuokoa upotevu wa muda na pesa
Hakuna jambo linaloleta shida kwenye familia kama kuwa na mtu mwenye ugonjwa sugu unaohitaji kwenda kliniki. Mfano, baadhi ya wagonjwa wenye kiharusi au tatizo la bipolar hawawezi kupandishwa kwenye boda au usafiri wa uma kwenda clinic, ni lazma taxi au gari binafsi itafutwe.
Wanafamilia hutakiwa kuchanga hela ya usafiri na matibabu; hali hii inaweza kupelekea kugombana na wakati mwingine mgonjwa kutopelekwa hospitali kabisa.
Kupitia huduma hii ya afya nyumbani, changamoto hii huondoka kwasababu wataalam wa afya huja na kutoa huduma nyumbani kwa mgonjwa.
Pia mgonjwa wako atafatiliwa kwa ukaribu na daktari, na nyinyi kama ndugu wa mgonjwa mtaweza kuendelea na majukumua yenu ya kila siku. Kazi itakayobaki kwenu ni kulipia tu huduma hiyo huduma kwa mwezi.
4. Huboresha afya ya mgonjwa
Mgonjwa anayeonwa nyumbani kwa muda wake binafsi ana asilimia kubwa ya kuwa sawa kiafya kuliko anayeenda clinic au hospitali. Akiwa nyumbani atapata wasaa wa kuongea na mtaalamu kwa muda wa kutosha na yeye kupatiwa elimu bora ya afya itakayomsaidia kuishi vizuri na ugonjwa wake.
Pigia picha unatembelewa na daktari aidha nyumbani au ofisini kwako, kwa muda wako, unapata sessions zako bila hata kuangaika na foleni za mjini na unaendelea na shughuli zako kama kawaida. Ni changamoto ngapi utakua umezikwepa? Ni faida ngapi utakua umezipata?
Mgonjwa mmoja anayeenda kliniki hupoteza takriban masaa 4 mpaka 6 kwa kusubiria tu kumuona daktari na masaa 2 kusubiria dawa. Hii ndio huwafanya wagonjwa waende maduka ya dawa kununua dawa tu na wasije kliniki.
Una mgonjwa mwenye ugonjwa sugu wa lishe, saikolojia na akili? Basi fikiria kuingia katika huduma ya afya nyumbani upate faida zote hapo juu. Unaweza ukalipa gharama ya juu kidogo lakini utafaidika kwa vingi sana.
Hivi karibuni…
Abite Nyumbani tumeanza kutoa huduma ya Mpangilio wa Mlo kwa wagonjwa wa kansa, Mimba, Kisukari na Presha,madonda ya tumbo na magonjwa mengine sugu.
Lakini pia huduma hii inapatikana kwa watu wenye changamoto na mahitaji mbalimbali ya lishe kama wanaotaka kupunguza uzito, wajawazito, wamama waliojifungua, na wanamichezo.
Una shida ya kupunguza uzito na imekuwa ngumu?
Kupunguza uzito ni moja ya swala gumu sana kwa watu wenye uzito wa juu. Sababu ni kukosa mwongozo wa Lishe. Ulishawahi kuona Jinsi ilivorahisi kwa mabondia kushusa na Kuongeza uzito wao? Sababu ni moja, wanakuwa na wataalamu wa Lishe na mazoezi. Wanafuata maelekezo fulani.
Wewe uzito wako haubadiliki kwa sababu hauna mwalimu wa Lishe ndio maana ni vizuri kupata huduma hii binafsi ili utimize malengo yako mapema.
Una watoto nyumbani na unahangaika wale nini ndani ya wiki?
Afisa Lishe wetu atakupatia mpangilio wa Lishe kiasi kwamba utakuwa unanunua na kuweka tu.
Dada wa kazi anaangalia mpangilio na kupika na watoto watakuwa na afya nzuri; wakati huo wewe unaendelea na majukumu yako.
Wewe ni mgonjwa wa kisukari na haujui ule nini, uache nini?
Lishe ni jambo muhimu sana kwa mgonjwa wa kisukari. Asilimia kubwa ya wagonjwa wa sukari wanameza dawa kila siku lakini sukari yao inagoma kushuka. Inaleta mawazo sana, lakini tatizo kubwa kwao ni ulaji.
Asilimia 80 ya wagonjwa wa sukari hawajui wale nini na kwa wakati gani. Sababu ni elimu ndogo. Daktari hana lisaa lizima kukushauri kuhusu vyakula ila kupitia Afisa Lishe utafunguliwa upeo na sukari yako haitabaki juu tena.
Pamoja na huduma hizo, unaweza pia kupata daktari wako binafsi kutoka Abite Nyumbani. Daktari huyu atakuwa kiongozi na mshauri wako kuhusu changamoto mbalimbali za afya ulizonazo, za watoto wako, au hata ndugu zako wa karibu.
Afya yako ndio mtaji wako, hakikisha unapata huduma ya afya ya kiwango cha hali ya juu.

Chief Content Officer (CCO) at Abite Afya
I’m responsible for overseeing the entire content strategy, ensuring that all published materials align with the blog’s mission, audience needs, and business goals.
Nakalaaaa ni nzuri kwa mfumo wa maisha kwa sasa
Karibu sana Mr Frank.