Meal plan: Maana, faida, jinsi na gharama

Leo nitaongelea swala la meal plan, au kwa lugha rahisi ya kiswahili ratiba ya chakula ya siku/wiki.

 

Tuanzie hapa…

Je, unajua tatizo sio vyakula vya sukari au wanga unavyotumia, tatizo ni wewe!

Chakula chochote hutakiwa kutumika kwa kiasi na kwa mpangilio mzuri. Sukari ni muhimu sana mwilini kwani husaidia shughuli mbalimbali za mwili ambazo huhitaji nguvu.

 

Tatizo linakuja katika ulaji au mtumiaji wa sukari hiyo au chakula hicho chenye asili ya wanga. Hii pia inahusu makundi mengine ya vyakula kama vile protini, madini na vitamini.

 

Mfano, unaweza ukakuta chai imepikwa na kuwekwa sukari nyingi na kumbe ingepaswa kuwekwa sukari kidogo tu.

 

Au chai inaweza ikawa imewekwa sukari kiasi kwa ajili ya ladha lakini mtu akawa anaongeza sukari mpaka ikawa ina ladha tamu inayokaribiana na soda ya dukani.

 

Hapo bado kuna ulaji wa maandazi au chapati ambavyo vikimeng’enywa hubadilika kuwa sukari mwilini na mtu huyu huyu bado anaweza kunywa soda baridi baada ya hapa.

 

Hasa hii ni tabia au tamaduni binafsi ya chakula ambayo mtu anaweza kujitengenezea, na wala sio kwamba sukari au maandazi ni mbaya kwa afya!

 

Chakula kinaenda sambamba na tamaduni na katika tamaduni zetu, kama watanzania au waafrika kiujumla, tumezoea kwamba kula chakula kingi ni tabia nzuri, sahihi kiafya na ya kupendeza katika jamii.

 

Mtu akichota chakula kidogo huwa kuna kawaida ya kuambiwa “ongeza, chakula kipo!’’

 

 

Desturi ya chakula nyingine inaweza kuonekana pale ambapo mtu anakwenda katika nyumba ya mtu mwingine na akatamani kula sana kwa sababu ya njaa ama mazoea ya kula chakula kingi kwa sababu tu ya desturi ya chakula alichozoea inayohusisha ulaji wa chakula kingi.

 

Mifano hapo juu inatuonyesha tabia mbalimbali zinazohusiana na chakula, yaani feeding habits, ambapo asilimia kubwa ya waafrika hula vyakula kwa mazoea bila kuzingatia namna mwili unahitaji kutumia chakula hicho.

 

Mfano, kama utakula ugali mwingi inabidi uwe na kazi ngumu ya kufanya kama kubeba zege ili ugali huo ukupe nguvu unayohitaji.

Kwa lugha rahisi, kila gari lina size ya engine inayohitajika kwa ajili ya kuendeshea gari hilo. Gari yenye kazi kubwa huhitaji engine kubwa kuliko gari yenye kazi ndogo!

Ili kuelewa namna ya kula kwa viwango sahihi, basi utahitaji muongozo wa ulaji – kwa lugha ya kingereza hujulikana kama meal plan.

 

So hii meal plan ni nini hasa?

Kwa lugha rahisi, muongozo wa chakula unahusisha mchakato mzima wa kupangilia vyakula ambavyo vinatumika na mlaji kwa muda wa siku moja mpaka wiki nzima.

 

Umewahi kwenda hospitali ukaambiwa una ugonjwa wa kisukari, au pressure, ama vidonda vya tumbo au cancer kisha kuambiwa uzingatie unachokula na kutajiwa vyakula au vitu mbalimbali kama chumvi, sukari, maharage, nyanya, na kadhalika?

 

Mbaya zaidi hapo unakua hukumbuki vizuri baada ya kuonana na mtaalamu huyo wa Afya – mara nyingi inakua ni daktari.

 

Daktari huyu ambaye pamoja na kazi kubwa anayoifanya lakini swala la kumpangia mgonjwa aina za vyakula vya kutumia na kutotumia ni swala lililoko nje ya taaluma yake hivyo utahitaji Afisa lishe kwa ajili ya kukusaidia kupata miongozo ya chakula kutokana na changamoto yako kiafya.

 

Unaweza kufikiria muongozo huu wa chakula una faida gani, kutambua hilo nimekuweKea hapo chini faida 4 kupatiwa muongozo huu na Afisa Lishe.

 

Faida za Meal plan

  1. Itakusaidia kuokoa muda wa kufikiria chakula unachoweza kula kwa muda huo kutokana na changamoto uliokua nayo
  2. Itakusaidia kuimarisha hali yako kiafya na kupunguza maudhi yanayotokana na kula vyakula vinavyosababisha hali za kudhoofika zaidi kiafya.
  3. Itakusaidia kufahamu namna sahihi ya kula chakula ili uweze kufikia malengo uliojiwekea kiafya kwasababu kila muongozo wa chakula wa mteja huwa una malengo.
  4. Utakua na uwezo wa kuwasiliana na mtaalamu kama kuna maswali kipindi cha kutumia muongozo huo wa chakula.

 

Vitu vitakavyohitajika kabla ya kutengenezewa meal plan yako

Ili mtaalamu wa maswala ya lishe aweze kukusaidia kupata muongozo huu wa namna ya kula kila siku, kuna mambo ambayo atahitaji kuyafahamu kama:

1. Uzito

2. Urefu

3. Umri

4. Jinsia

Wanaume na wanawake wana mahitaji tofauti; pia wanawake wajawazito na wanaonyonyesha huwa na mahitaji makubwa ya virutubisho tofauti na wanawake wasionyonyesha au wasiokua na ujauzito.

 

5. Vyakula ambavyo hauvitumii

Inawezekana ni kwa sababu ya uzio yaani “allergies” au/na imani binafsi.

 

6. Kazi unayofanya

Hali ya ulaji hutofautiana kwa watu wanaofanya kazi za kutumia nguvu kubwa ya mikono, wanaofanya kazi za kutumia nguvu kiasi na wale ambao hawatumii nguvu za mikono katika kazi zao.

 

7. Uwepo wa magonjwa ya muda mrefu au magonjwa mengine

Hii itatusaidia kupanga mkakati wa mlo utakaosaidia kuboresha hali ya mteja anayeishi na ugonjwa huo.

 

8. Aina za dawa anazotumia mteja kwani kuna baadhi ya dawa ambazo husababisha muingiliano katika shughuli ya umeng’enywaji wa chakula fulani (“food drug interaction” hii inategemea mteja ana tatizo gani)

 

9. Vyakula vinavyopatikana katika maeneo anayoishi mteja

Hii ni kwa sababu kuna baadhi ya vyakula ambavyo havipatikani kwa urahisi, mfano kuna maeneo watu wana asili ya uvuvi na hivyo wanaweza kuwa na urahisi wa kupata samaki kuliko sehemu ya watu wenye asili ya ufugaji.

 

The “process”

Kwa tamaduni zetu watanzania, sio rahisi sana kukuta watu wanachukulia serious swala la kusaidiwa kupanga chakula na mtaalamu.

 

Ni vizuri ifahamike kwamba katika wakati wa kupanga chakula, mteja anahusika kwa ukaribu na ni muhimu sana kuhusisha vyakula ambavyo mteja huwa anapenda kula.

 

Mchakato huu unahusisha mazingira ya kupeana ushauri wa nini kifanyike na sio kuambiwa katafute chakula hiki na hiki.

 

Mfano, mimi binafsi hupenda kukaa na mteja pamoja na ndugu wa karibu ambaye mara nyingi anahusika katika kuandaa chakula cha mteja huyu, na huwa tunapanga kwa majadiliano na kuja na orodha ya vyakula ambavyo vitaonekana katika mpangimimosa chakula.

 

Kitu ambacho nitaongeza kama mtaalamu wa maswala haya ni kiwango cha chakula ili uweze kufikisha kiwango cha virutubisho kinachohitajika katika mwili kwa muda wa siku moja.

 

Kwa kingereza hujulikana kama Recommended Dietary intake/Recommended Dietary allowance (RDI au RDA).

 

Mwisho wa siku wewe kama mteja inabidi ujisikie kwamba umekua sehemu ya mpango mkakati ule.

 

Mwisho

Gharama zetu za kupata meal plan hii ni TShs 50,000 tu ambapo utapata muongozo wako wa namna ya kula kwa muda mrefu pamoja na ushauri wa bure mara 2 kwa mwezi.

 

Afya ni mtaji, wekeza upate matunda. Karibu tukuhudumie!

4 thoughts on “Meal plan: Maana, faida, jinsi na gharama”

Leave a Comment

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

swSW