Asusa ni aina gani ya chakula hasa?

Inawezekana hili neno likawa geni kidogo masikioni mwako hivyo ukawa unajiuliza ni nini maana ya neno Asusa?

 

Taasisi ya Chakula na Lishe nchini Tanzania imetoa tafsiri ya neno hili kwa kusema:

“Asusa ni kiasi kidogo cha chakula ambacho sio mlo kamili, kinachoweza kuliwa bila ya matayarisho makubwa.”

 

Kama Asusa ni mlo mdogo (ambao sio mlo kamili), Je! ninatakiwa kula milo mingapi kwa siku? Na Asusa hii inaliwa wakati gani?

 

Najua haya maswali yanaweza kupita akilini mwako baada ya kujua maana halisi ya neno Asusa, ambalo kwa lugha ya Kiingereza limezoeleka kama “Snacks”.

 

Jibu la swali hili ni kwamba mtu anaweza kula milo mitano mpaka sita kwa siku ambapo milo miwili huunganisha milo mitatu mikubwa ambayo inategemewa kuwa milo kamili kwa maana ya kwamba inakuwa na makundi yote ya vyakula.

 

Na tukumbuke kwamba katika milo hii mikubwa tunatumia kipimo cha sahani inayofaa ya mlo kamili katika kupakua kila mlo kwenye sahani.

 

Katika milo mitatu midogo, hii itahusisha Asusa ambazo ni nzuri na sahihi kwa ajili ya afya yako. Mara nyingi Asusa huliwa katikati ya mlo mmoja na mwengine.

 

Mfano wa ratiba ya ulaji ambayo inaonyesha muda wa kula Asusa

1. Kifungua kinywa kwa asubuhi, “Breakfast”, ambapo makala mbalimbali zimeshauri kula kifungua kinywa muda wa saa 12:00 asubuhi mpaka saa 3:45 asubuhi na hakipaswi kuvuka saa 4:00 asubuhi.

 

2. Asusa ya kwanza inapaswa kuliwa saa Moja mpaka Mbili kabla ya kula mlo unaofuata. Inaweza kwanzia saa 4:00 mpaka saa 5:00 asubuhi.

 

3. Chakula cha mchana kinapaswa kuliwa kuanzia saa 6:00 mchana mpaka saa 8:00 mchana. Chakula hichi kinapaswa kuwa mlo kamili unaohusisha makundi yote ya vyakula.

 

4. Asusa ya pili inaweza kuliwa saa moja mpaka saa mbili kabla ya kula chakula cha jioni. Hii inaweza kuwa kwanzia saa 9:00 mchana mpaka muda wa saa 11:00 jioni.

 

5. Chakula cha jioni kinaweza kuliwa saa 12:00 jioni mpaka muda wa saa 3:00 usiku. Chakula hichi kinapaswa kuwa mlo kamili unaohusisha makundi yote ya vyakula.

 

Zingatia…

Asusa zenye faida katika mwili ndio zinazopaswa kutumiwa. Asusa hizi ni zile zinazopaswa kuupatia mwili virutubisho vya kutosha kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimwili.

 

Asusa hizi hazipaswi kuwa zenye mafuta mengi ama sukari nyingi kwani hupelekea ongezeko la mafuta mwilini ambayo husababisha mtu kupatwa na magonjwa yasiyoambukizwa kama vile Kisukari, Shinikizo la juu la damu (Presha), pamoja na kiharusi ama “stroke”.

 

Asusa hatarishi kwa afya ni zipi?

Asusa hatarishi kwa afya ya binaadamu ni kama vile keki, pipi, biskuti , donati au maandazi na vyakula vingine vinavyotumia mafuta mengi na sukari nyingi katika kutengeneza.

 

Unhealthy snacks

 

Snacks hizi hupelekea ongezeko la sukari na mafuta mwilini ambalo hupelekea hali hatarishi ya kusababisha magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari, shinikizo la juu la damu na kadhalika.

 

Asusa zinazoongeza ubora wa Afya yako

Asusa zisizo hatarishi katika afya ya binadamu ni kama vile matunda ya tufaa (Apples), korosho, karanga, zabibu, ufuta, mbegu za maboga ambazo watu wengi hutafuna kama wanavyotafuna karanga, n.k.

 

Healthy snacks to have before lunch and dinner.

 

Asusa, kama vyakula vingine, mara nyingi hutegemea ni aina gani ya chakula ama tunda lililoko kwenye msimu katika eneo lako la kuishi au makazi.

 

Mfano kipindi cha mananasi, embe, chungwa, matunda damu, tikiti, fenesi huamua aina gani ya Asusa kutumika kutokana na upatikanaji wake.

 

Mambo ya kuzingatia katika utumiaji wa Asusa

1. Kiasi cha mlo wa asusa hakitakiwi kuwa kipimo kikubwa, japo ni vyakula vyenye kiasi kidogo cha mafuta ama sukari kulinganisha na vyakula vilivyochakatwa viwandani yaani “processed foods”.

 

Vikitumika kwa kiwango kikubwa, vyakula hivi huweza kusababisha mkusanyiko mkubwa wa sukari mwilini ambayo katika mchakato mzima wa umeng’enywaji wa vyakula mwisho wa siku hugeuka kuwa mafuta.

 

Hivyo basi ni muhimu kukumbuka yote haya tunapotumia asusa hizi. Mfano pale unapotumia korosho au karanga, hakikisha kukumbuka kwamba kuna mlo wa mchana ama jioni unakusubiria.

 

2.. Kama ni karanga, korosho, zabibu au mbegu za maboga unaweza kupima kiasi cha kiganja kimoja cha mkono, ndipo utumie hio kama asusa yako. Kama ni Apple au chungwa, unaweza kutumia moja tu kwa siku.

 

3. Kama ni ndizi iliyoiva, tumia ndizi moja kubwa au mbili ndogo, ama moja na nusu kwa size ya kati.

 

Yote haya yanawezekana kama utakua umekula mlo kamili asubuhi na mchana.

 

Ujumbe wa Leo

Ni muhimu kufanya machaguo sahihi na yenye afya pindi unapokua unachagua vyakula vya kutumia kama Asusa.

 

Hasa katika vipindi ambavyo unakua na hamu ya kula vyakula vya aina flani mfano, pipi, ice-cream au maandazi. Vipindi hivi kwa lugha ya kingereza hujulikana kama “craving periods”.

 

10 thoughts on “Asusa ni aina gani ya chakula hasa?”

  1. Very interesting Esther, nutrition imekutana na mtaalamu Sasa,
    Hii ya snacks nimeipenda.
    Asante sana.

    1. Ester Mndeme

      I am glad umefurahia somo. Nutrition is indeed a very interesting field. I am glad i get to share what i know with other people.

  2. Congratulations Esther Mndeme, for a well written website.
    Snacks are very crucial in human being life stages.
    I am really happy for you and this beautiful milestone you have made.

  3. Tunashukuru kwa ushauri mzuri sana juu ya lishe Bora. Mara nyingi imekuwa shida hasahasa kwa wali walio na ugonjwa wa kisukari kutafuta lishe inayo wafaa.

    1. Karibu sana , ni matumaini yangu tutaendelea kujifunza pamoja na ni lengo letu kuelemisha jamii juu ya maswala mengi muhimu yanayohusiana na lishe.

Leave a Comment

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

swSW