Unawekeza kwenye Hospitali au Kituo cha Afya? Fahamu Nyaraka 6 za Kukulinda Kabla ya Kununua Vifaa Tiba
Katika uwekezaji wa sekta ya afya, ununuzi wa vifaa tiba ni mojawapo ya maamuzi yanayohitaji umakini mkubwa. Baadhi ya wawekezaji huzingatia bei, muonekano wa kifaa na ahadi za muuzaji, huku wakisahau nyaraka zinazothibitisha kuwa kifaa kinafaa kwa matumizi yaliyokusudiwa, kinaweza kusakinishwa kwa usalama na kina uwezo wa kufanya kazi kama inavyotakiwa. Kifaa kinaweza kuwa kipya


