“Lisaa la Dhahabu”: Siri ya Kuokoa Maisha Unapopata Dharura ya Kiafya

Sekunde chache zinaweza kutofautisha kati ya kupona na kupoteza maisha. Wakati unapokabiliwa na dharura kama ajali, kiharusi (stroke), au shambulio ghafla la moyo, kuna muda muhimu unaoitwa “Saa la Dhahabu”.

Hizi ni dakika 60 za kwanza tangu tatizo linapotokea, ambapo mwili unahitaji msaada wa haraka wa kitaalamu ili kuzuia madhara makubwa au ulemavu wa kudumu.

Unapopatwa na dharura, uamuzi unaoufanya ndio utaamua mustakabali wa mgonjwa wako atakapofika hospitali. Hapa wengi wetu hudhani swala ni kumpeleka hospitali tu, lakini lengo sio tu yeye kufika hospitali bali anafikaje? Na anafika ndani ya muda gani?

Changamoto za Kutumia Usafiri wa Kawaida

Katika hali ya taharuki, wengi wetu hukimbilia kumpakia mgonjwa kwenye gari binafsi, bajaji, au bodaboda tukiamini tunafanya jambo sahihi na kwa nia njema ya kutaka kuwahi.

Ukweli ni kwamba, hata kama nia ni njema, hatua hii mara nyingi huwa ni mtego ambao watu wengi tunaupata, na ni kosa ambalo hata mimi nimewahi kulifanya huko nyuma, vilevile huwa na hatari ambazo hatuzifikirii kwa wakati huo.

Usafiri huu si salama kwa dharura ya ghafla kwa sababu unakinzana na umuhimu wa lisaa la kwanza:

1. Kukosekana kwa huduma njiani: Mgonjwa hubaki bila msaada wowote wa kitaalamu mkiwa njiani kuelekea hospitali. Hii ina maana kuwa hali yake ikibadilika ghafla, hakuna anayejua nini cha kufanya kwa wakati huo.

2. Kukwama kwenye foleni: Tofauti na ambulance, gari la kawaida halina kipaumbele barabarani. Unaweza kujikuta umekwama kwenye foleni huku dakika muhimu za “Saa la Dhahabu” zikiendelea kupotea.

Kwanini Ambulance ni Zaidi ya Usafiri?

Watu wengi wanaamini ambulance ni gari la kubeba wagonjwa tu, lakini ukweli ni kwamba ambulance ni hospitali inayotembea. Unapopiga simu ya dharura unafaidika na hivi hapa:

1. Maelekezo yanaanza hapo hapo: Wataalamu wa kutoa huduma ya afya ya dharura wanakuelekeza hatua za kwanza na muhimu za kuchukua kabla Ambulance haijafika.

2. Huduma inaanza ndani ya gari: Ndani ya ambulance kuna vifaa na wataalamu wa afya ambao wanaanza kumpatia mgonjwa matibabu ya haraka na muhimu wakati mkiwa njiani. Hii inamaanisha lile lisaa la kwanza la dhahabu linatumika vizuri kuokoa uhai.

3. Kufika hospitali haraka na salama: Ambulance ina king’ora ambayo husaidia kupata kipaumbele barabarani, hivyo Saa la Dhahabu linatumika kikamilifu na mgonjwa anafika mapema hospitali.

Unawezaje Kuita Gari la Dharura Ukipatwa na Tatizo?

Dharura ya kiafya haibishi hodi wala haikupatii muda wa kujipanga. Ukipatwa na hali ya ghafla, fanya yafuatayo:

  • Ingia kwenye simu yako: Kagua haraka namba uliyohifadhi ya dharura.
  • Wapigie simu: Elezea kwa ufupi kuwa mgonjwa ameanguka ghafla au amepata ajali.
  • Taja eneo mlipo: Toa alama inayojulikana karibu nanyi, kama msikiti, kanisa, au mtaa fulani.
  • Sikiliza maelekezo: Fuata hatua utakazopewa huku gari likiwa njiani kuja kufuata mgonjwa.

Chukua Hatua Mapema

Umeona sasa umuhimu wa kuwa na namba ya dharura, hasa gari la dharura? Usiwe kama watu wengi wanaanza kutafuta namba za msaada wakati dharura tayari imeshatokea.

Kama bado huna namba hiyo, mimi nakupendekezea City Ambulance Tanzania. Hii ni kampuni kwa ajili ya msaada wakati wa dharura ya kiafya ambayo itahakikisha unapata huduma ya dharura ndani ya muda muafaka.

Unaweza kunakili namba yao ya dharura hapa, 022 260 0120 au +255 747 366 334, ili uwe tayari wakati wowote.

Lisaa la kwanza ndio huamua kufa au kupona. Lithamini kwa kuita gari la dharura badala ya kutumia gari lako, kwani uwezekano wa hali kuwa mbaya njiani bila uangalizi wa wataalamu ni mkubwa.

Endelea kusoma makala zetu kuifahamu huduma ya ambulance kwa undani zaidi.

Leave a Comment

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

swSW