Erick Myenda, PT

Erick Myenda ni mtaalamu wa physiotherapy (physiotherapist) na mwelimishaji wa afya mwenye shauku ya kuongeza uelewa wa jamii kuhusu physiotherapy, urekebishaji wa uwezo wa mwili na afya ya jamii kupitia elimu inayozingatia ushahidi wa kisayansi.   Maeneo yake ya kuvutiwa kitaaluma ni pamoja na afya ya misuli na viungo, udhibiti wa maumivu, urekebishaji wa uwezo wa mwili, afya ya uzee na uhamasishaji wa afya. Kupitia makala zake, analenga kuunganisha maarifa ya kitaalamu ya afya na maisha ya kila siku kwa kuwasilisha taarifa sahihi kwa lugha rahisi, inayoeleweka na inayoweza kutumika katika vitendo.   Kama mtaalamu wa physiotherapy na mwelimishaji wa afya, Mr. Erick analenga kuwasaidia watu na jamii kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya zao, kutambua changamoto zinazoweza kuhitaji tathmini ya kitaalamu na kuelewa mchango wa physiotherapy katika kuboresha uwezo wa kufanya shughuli za kila siku na ubora wa maisha.

Maumivu ya goti baada ya kufanya mazoezi

Je, Unasikia Maumivu ya Magoti Baada ya Mazoezi? Hapa Ndipo Unapokosea!

Watu wengi huanza safari ya mazoezi wakiwa na ari kubwa ya kujenga afya bora, kupunguza uzito, au kuimarisha miili yao. Lakini, kwa baadhi yao, furaha hii hupotea pindi tu wanapomaliza mazoezi na kuanza kusikia maumivu makali au kuuma kwa magoti yao. Kama umewahi kukutana na hali hii, haupo peke yako.   Hili ni moja ya

Je, Unasikia Maumivu ya Magoti Baada ya Mazoezi? Hapa Ndipo Unapokosea! Read More »

Plantar Fasciitis

Maumivu ya Kisigino Baada ya Kukaa Muda Mrefu au Kuamka Asubuhi: Chanzo & Tiba

Je, umewahi kuamka asubuhi na ulipoweka mguu chini kupiga hatua ya kwanza, ukasikia maumivu makali ya kuchoma kwenye kisigino chako? Au labda baada ya kukaa kwa muda mrefu unaposimama unahisi kama unakanyaga kigingi au sindano chini ya kisigino?   Katika jamii yetu, watu wengi wakipatwa na changamoto hii wanakimbilia kuamini kuwa ni maumivu ya “asidi

Maumivu ya Kisigino Baada ya Kukaa Muda Mrefu au Kuamka Asubuhi: Chanzo & Tiba Read More »

Coughing which result in back pain

Kwa Nini Mgongo Unaweza Kukuuma Unapokohoa au Kupiga Chafya?

Umewahi kupata maumivu ya mgongo unapokohoa, kupiga chafya au kujikaza wakati wa kwenda chooni? Huenda ulijiuliza kwa nini kitendo cha kawaida kama hiki kinaweza kusababisha maumivu makali. Maumivu haya yanaweza kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo changamoto za misuli, diski za uti wa mgongo au neva. Wakati mwingine, yanaweza kuashiria tatizo linalohitaji uchunguzi wa kitaalamu.  

Kwa Nini Mgongo Unaweza Kukuuma Unapokohoa au Kupiga Chafya? Read More »

swSW