Jinsi Ukosefu wa Elimu ya Dharula Unavyogharimu Maisha ya Watanzania
Kila mtu atakufa, hilo halina ubishi kabisa. Swali ni kwamba, utakufa lini? Utakufaje ? Katika mazingira yapi? Je, unaamini kuna vifo vinavyosababishwa na ukosefu wa elimu? Leo hii ukipatwa na dharula ya mtu wako kuanguka ghafla au ukikutana na mtu amedondoka ghafla utachukua hatua gani? Kuwa mkweli, utaita gari ya dharula au utamuitia bajaji? Katika familia nyingi za kitanzania, mgonjwa akianguka au kuzidiwa ghafla huwa hawakumbuki gari ya dharula (ambulance) bali watampakia haraka kwenye gari au boda na kumkimbiza hospitali. Kulingana na makadirio ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa mwaka 2025/2026, takriban watu 10,000 hupoteza maisha kila mwaka nchini Tanzania kutokana na ajali za barabarani. Ripoti ya World Bank na UN Road Safety Fund (2024) inaonyesha kuwa idadi kubwa ya vifo hivi hutokea kabla ya kufika hospitalini (pre-hospital deaths). Wagonjwa wengi husafirishwa kwa kutumia bodaboda, taksi, au magari ya polisi ambayo hayana vifaa vya kuimarisha hali ya mgonjwa (resuscitation equipment) wala watumishi wenye ujuzi. Udhaifu mkubwa wa mpango wa dharula kuanzia kwenye elimu kwa jamii, mpango mzima wa kuchukua hatua za mapema, ukosefu wa elimu ya huduma ya kwanza (First Aid) kwa madereva na miundombinu kama barabara ambayo sio rafiki kwa dharula ni vyanzo vikubwa vya vifo hivi. Tanzania imechukua hatua gani katika kuongeza ufanisi wa huduma za dharula? Tanzania kupitia Wizara ya Afya inafanya juhudi kubwa kuhakikisha inaboresha kitengo cha dharula lengo likiwa ni kupunguza idadi ya vifo nchini. Baadhi ya mambo ambayo Wizara ya Afya inafanya kazi kubwa kuboresha katika idara ya dharula ni kama ifuatavyo: […]
Jinsi Ukosefu wa Elimu ya Dharula Unavyogharimu Maisha ya Watanzania Read More »



